Tuombe kwa ajili ya chanzo cha tatizo, na si kwa ajili ya tatizo

Benmpo

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
450
424
Kumekuwepo na maombi mbalimbali nchi nzima kwa Mhe Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Singida Mashariki, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, na Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), aliyepigwa risasi kadhaa na kujeruhiwa vibaya mjini Dodoma na kuhamishiwa katika Jiji la Nairobi kwa ajili ya matibabu. Lakini jeshi la Polisi nchini lilionya kuwa mkusanyiko wowote ambao utafanyika kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, utadhibitiwa. Haikuishia hapo, hivi karibuni lilikamata vijana wawili katika viwanja vya TIP, katika kitongoji cha Sinza, Jijini Dar es Salaam mkusanyiko uliokuwa na dhamira ya kufanya maombi kwa ajili ya Mhe Tundu Lissu. Hivyo ni dhahiri kabisa Jeshi la Polisi liko ‘serious’ katika hili na watakao kiuka watachukuliwa hatua.

Lakini pia Jeshi la Polisi halijatoa zuio juu ya kuliombea taifa letu juu na matukio yanaoendelea kutokea. Ni wakati sasa kwa wananchi wenye mapenzi mema na taifa letu la Tanzania kujikita katika maombi kwa ajili ya chanzo kinachosababisha matukio yote haya kutokea. Kwa sababu tukiwa tunaomba tu pale matukio yanapotekea itakuwa haina maana, inabidi tutafute kinga ya haya yote. Je endapo wote tukipigwa risasi nani atamwombea mwenzake?

Hatukumlilia Mungu vya kutosha kwa mauaji yaliyokuwa yanaendelea Mkoa wa Pwani katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji na kwingeneko nchini. Ni wakati sasa wa kuliombea taifa letu bila kuangalia sehemu mtu alipotoka, wadhifa wake, dini yake, kabila lake n.k, ni wakati wa kumwambia Mwenyenzi Mungu yatosha kwa matukio ya kinyama yanayoendelea nchini kwetu.

Maombi yangu kwa taasisi zote za kidini na wananchi wote kufanya maombi kwa ajili ya taifa kwa ujumla, kukemea maouvu yote yanayoendelea, kutokutumia madhara aliyopata mwingine kama mtaji wako wa kisiasa, kuwa wazalendo na kutunza amani tuliyopewa na aliyetuumba.
 
Back
Top Bottom