Tuombe kampeni hizi ziongezewe muda ili hii Serikali iendelee kupeleka maendeleo kwa wananchi

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
459
1,000
Wakuuu, kwa sasahivi zimetolewa hela nyingi sana kwenda mikoani kwa ajili Ya Maendeleo Ya wananchi, pesa zinatumwa kila kukicha miradi Ya Maji, inafuguliwa, barabara hela zinatumwa, huko mahospitalini kumenoga mambo yanarekebishwa, wakuu kumbe serikali hiii ina hela nyingi hivyo?

Tuombe tume Ya Uchaguzi iongeze angalau miezi miwili wakuu, Magufuli atazitoa zote, nimeshangaa hadi Mtwara Jana serikali ikatangaza kutuma bilioni 20 Kwa ajili ya miradi Ya Maji Ya kule, huyu Magufuli kumbe alitufanya mabumunda kutokanaa na sisi kukosa watu wa kupasa sauti, Lissu MUNGU akulinde, yaani Magufuli alivyokuwa anawatukana wananchi kwa dharau alihisi kuwa ameishaipata nchi hahahahahahhaha nimecheka sana.

Huyu mzee alikuja kuwa yeye ni jiwe kweli kweli kumbe watu walikuwa wanamchora na kumcheka khaaaa! Na afahamu kuwa hapo ndio anapomuongezea nguvu Lissu na kuwaonesha wananchi wazi kuwa kumbe Lissu ndio mkombozi wao, na asingekuwa Lissu hayo mapesa yangekuwa yanaendelea kumiminika kule Chato tu, na Kwa sasa Hakuna cha Chato wala cha jiwe, mijitu imekaaa na kujitoa unaham na kumsema Lissu vibaya wakati ndani ya mwezi mmoja tu kakomboa watu mamilioni na mamilioni Kwa kupasa tu Sauti.
 

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
3,285
2,000
Ngonja kampeni ziishe, hizo pesa zitatokea Mahal popote palipo wazi

Magufuli ni katiri sanaa

Mtalimia meno akirudi madarakan huyu mzee
 

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
754
1,000
Magufuli hana lake Nov ya mwaka huu, ajiandae kurudi Chato
Watu wa mjini ndio wanazingatia uwepo wa upinzani lakini huko waliko wengi ndanindani huko wao wanachojua ni kuweka tiki penye maandishi CCM na kwamba viboma vilivyobaki ni watu wasiojulikana.

Shida inaanzia hapo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom