Tunyanyue sauti:- MV LIEMBA (100 YEARS OLD) Isitishe huduma zake katika ziwa Tanganyikia

Hydrobenga

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,127
212
MV LIEMBA....huko ziwa Tanganyika is The Oldest operating ship in the World (100 Years Old)....na serikali wanajivunia
hili....subiri siku izame watu watakuja hapa...Ohh meli ya zamani sana

Tunyanyue sauti zetu labda serikali itasikia ...MELI chakavu katika bandari zote Tanzania zisitishe huduma ....

MV Liemba - Wikipedia, the free encyclopedia

attachment.php
 
watu wanaitafuta hiyo meli wakaiweke museums kwao huko,nafikiri serikali inatafuta mwanya wa kuiba ndo iuzwe kwa bei ya kutupwa.
 
Naipenda, iko fresh kwa makumbusho!!! Tukiipiga mnada wazungu watakuja kutupa pesa chafuuuuu

wajerumani walitaka walete mpya hiyo waende nayo,cjui mchakato uliishia wapi. Kwa akili ndogo inayoongoza nchi wakipewa wao mil 100 hata bure wanawapatia kwa kisingizio cha urafiki na kwamba ni moja ya wafadhili. Hii nchi vituko haviwezi kwisha.
 
MBONA BADO NZURI TU?? KAMA HAWAITAKI WATU WA KIGOMA BASI ILETWE UKU KIGAMBONI TULIPOAMBIWA NA MAGUFURI TUPIGE MBIZI ITATUFAA SANA Tu
 
Duh yaani tangia wakati wa MJerumani! Kuna wakati nilisikia kuwa inaegeshwa ufukweni pale Kigoma na kugeuzwa kuwa Hotel; hii iliishia wapi au inasubiriwa mpya kisha hiyo iegeshwe.

Miaka mia hata kiuchumi itakuwa imezalisha meli nyingine hata tano.
 
Swala la umri ni kweli ni tatizo lakini cha msingi ni matengenezo(maintanance) kama meli inafanyiwa matengenezo ya maana basi hakuna tatizo inaweza kutumika hata miaka mia. Suala ni gharama za matengenezo hayo na inavyozidi kuzeeka ndio gharama inazidi. Hii Meli kwa vile ina historia ndefu na nchi yetu ni muhimu ikistaafu ipaki kigoma na kugeuzwa makumbusho ili watu waweze kuona historia yake na kuithamini na isiuzwe au kuguezwa scrap, that will be a shame!
 
subutu sema imezalisha vitambi vya wachachhe
 
Sio the oldest in the world,,,nenda hapo Slip way kuna Mid-summer 1910 inafanya biashara ya kubeba watalii na wengine wanakwenda kufanya party ndani yake....
 
Nilikuwa nimezoea kuiona pale makao makuu ya kata yetu (kasanga). Wakat kuna jamaa walikuwa na kawimbo fulan kananaimbwa hiv..watu wa zambia wanataman meli,wanafikiri meli ni mali yao.

Watanzania tunazo meli 3, meli ya kwanza ni meli mwongozo,meli ya pili ni meli liemba na meli ya tatu ni meli sangara....nadhan serikal inapaswa kufanya kitu maana huwa inajaza watu sana
 
Ni kweli imezeeka sana. Nilipata bahati ya kuipanda mwaka 1981. Ninaamini hata uwezo wake wa kazi utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kwa sasa hivi.

Ninajua watanzania huwa hatuna utamaduni wa preventive maintanance,matengenezo hutokea tu pale inaposimama kufanya kazi.

Napata uoga kilichotokea kwa MV Skagit kinaweza kutokea kwa MV Liemba kama haitfanyiwa matengenezo stahili. Liemba inajaza sana sana yakija maafa yatakuwa makubwa kama MV Bukoba.

Tahadhari kabla ya Hatari.
 
Kama unaogopa kuipanda piga mbizi teh teh teh kauli ya kaka bwana...
 
Swala la umri ni kweli ni tatizo lakini cha msingi ni matengenezo(maintanance) kama meli inafanyiwa matengenezo ya maana basi hakuna tatizo inaweza kutumika hata miaka mia. Suala ni gharama za matengenezo hayo na inavyozidi kuzeeka ndio gharama inazidi. Hii Meli kwa vile ina historia ndefu na nchi yetu ni muhimu ikistaafu ipaki kigoma na kugeuzwa makumbusho ili watu waweze kuona historia yake na kuithamini na isiuzwe au kuguezwa scrap, that will be a shame!

kweli tatizo sio uchakavu bali ni matengenezo ambayo inatafanya kuimarisha uwajibikaji wake katika kigoma.
 
Nilikuwa nimezoea kuiona pale makao makuu ya kata yetu (kasanga). Wakat kuna jamaa walikuwa na kawimbo fulan kananaimbwa hiv..watu wa zambia wanataman meli,wanafikiri meli ni mali yao.

Watanzania tunazo meli 3, meli ya kwanza ni meli mwongozo,meli ya pili ni meli liemba na meli ya tatu ni meli sangara....nadhan serikal inapaswa kufanya kitu maana huwa inajaza watu sana

Una uhakika na hili nafikiri ujafanya utafiti wako vizuri kwani kuna meli nyingi sana zinazomilikiwa na watanzania binafsi ama na Serikali. Ni nyingi sana
 
Liemba pamoja na umri wake bado iko vizuri kuliko meli nyingi zinazo operate Dar - Znz, maji ya Tanganyika sio mabaya(fresh water) kwa hull. Wakizingatia matengenezo na service zinazotakiwa bado sio mbaya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom