Tunu za taifa letu zilindwe

LUCAS KISIMIR

Member
Sep 11, 2012
29
4
SURA YA KWANZA
Tanzaniani nchi yetu sote tuliozaliwa humu (wazawa) pamoja na waliojiandikisha kuwaraia. Sisi sote kwa mchanganuo huo tunalo jukumu la kuiendeleza na kuilindanchi yetu kupitia uzalendo uliotukuka na wenye kujipambanua wazi wazi kila wakati,hususan kwenye masuala ya mustakabali na ustawi wa nchi yetu. Masuala yamustakabali wa nchi na ustawi fanisi wa watu wake hutawaliwa na mfumo ambaosehemu zake ndizo TUNU za taifa husika. Tunu za taifa ni masuala ya msingiambayo hulitambulisha taifa na utaifa wa watu wake, nayo yakipungua,yakikorofishwa, yakitiwa dosari na ama kukosekana, nchi huingia matatani. Kwaumuhimu wake huo, siasa potofu hazipewi mwanya wala fursa ya kuvuruga tunu zanchi husika hata kama ikiwa ni kwa jina la demokrasia. Viongozi wa juu katikautawala wa nchi, ndio wasimamizi na walinzi wakuu wa tunu za nchi yao.Mwananchi akizitambua, kuziheshimu na kuwajibika ipasavyo katika kulinda tunuza nchi yake, huingia katika daraja la uzalendo. Mzalendo ni mwananchi-mwajibikajikatika masuala ya mustakabaki wa nchi yake. Sote tunawajibika kuzifahamu TUNUza taifa letu kwa ukamilifu.

Tunapaswa kuzijifunza, kuzikariri, kuziheshimu,kuzilinda na kuzirithisha kwa vizazi vyote vya jamii yetu ili tunu hizo zipatekuwa historia inayoishi. Kamailivyokuwa katika kipindi cha uhuru na kipindi cha Azimio la Arusha hadi palelilipokuja lile la Zanzibar, Tunu za Taifa zilijulikana kwa wote nazo zilikuwazikitamkwa bayana na kwa sauti ya juu sana. Kwa bahati mbaya hatukuendelezautamaduni huo na kueneza kwa juhudi za wazi elimu inayomfunulia kila mmoja wetukuweza kupambanua ikiwa suala fulani ni tunu ya taifa au la.

Katika kipindinilichokitaja, hakukuweko na misamiati mingi isiyotamkika kama hii mipyatuliyonayo leo inayotufundisha kuitana kwa majina yasiyoitikika. Katika zamahizi, kama matokeo ya mwenendo mpya uliotuzukia, wengi wetu kwa nadra, hujikutatukichakura huku na kule tukisaidiwa na masalia ya historia katika fikara zetu,kujaribu kutafuta, kudadisi, kubuni na kujenga uelewa mpya katika kuchambua nakupambanua masuala yaliyo tunu, kati ya yale yasiyohitimisha vigezo vya sasavya kuwa tunu ya taifa letu. Elimu ya kutufumbua juu ya hili imeachwaikining’inia ili kila mwenye chembechembe ya uzalendo fikarani mwake na yulemwenye kujitolea kutumia muda wake kujishughulisha nayo, huchupa na kuchuma uelewakwa kadri ya majaliwa yake.

Kiladola yaani mamlaka na utawala katika kipande cha ardhi juu ya uso wa dunia kinachojipambanuakwa alama za mipaka yake na kwa kujumuisha watu wake, rasilimali zinazopatikanahumo, siasa ya utawala na uongozi, lugha, tamaduni, nembo, bendera, fedha naKatiba hujitambulisha kwa umma wake na ulimwenguni kupitia TUNU zake. Kilammoja miongoni mwetu anao ufahamu kwa viwango vinavyopishana kuhusu ukwelihalisi juu ya TUNU za Taifa letu. Hata hivyo, tunu ni masuala ya pamoja yawananchi katika nchi yao ambayo kimsingi hutajwa vile vile kwenye katiba yao nakutekelezwa kwa ufanisi, uaminifu na usimamizi thabiti kama msingi wa maishayao na sheria yao kuu.

Tunu hugusana moja kwa moja na maisha ya watu katikanchi yao na kwa ujumla hutawala mfumo wa maisha yao. Watu na tunu zao ni kamavipingili vinavyounda mnyororo-kila kimoja huingia ndani ya kingine na nje yautaratibu huo hakuna myororo wa kipingili kimoja. Nionavyo mimi, baada yakutafiti na kuchambua kusikohimiliwa na vigezo na masharti, najikuta katikamaelezo yafuatayo Kuhusu TUNU za Taifa letu. Baadhiya tunu ninazofahamu mimi ni hizi zifuatazo;-

  1. Kiswahili kama kiunganishio thabiti cha jamii zote kinachovuka mipaka dhidi ya ukabila,
  2. Haki za kibinadamu na usawa wa kijinsia,
  3. Amani, utulivu, kuheshimiana na kuvumiliana,
  4. Umoja wa kitaifa,
  5. Wimbo wa Taifa na Bendera ya Taifa,
  6. Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar,
  7. Usawa, wajibu, kutambua na kuheshimu utu,
  8. Uchaguzi wa viongozi kwa misingi ya kidemokrasia,
  9. Utawala bora, utii wa sheria na ulinzi wa mipaka yetu iliyo urithi wetu wa sasa na vizazi vijavyo,
  10. Mfumo bora na sahihi katika usimamizi na mgawanyo wa rasilimali za taifa ili kunufaisha umma kama kipaumbele muhimu,
  11. Haki ya kila raia kumiliki na kuendesha uchumi,
  12. Ushiriki sawa wa watu katika majadiliano, mipango na utekelezaji wa masuala ya umma,
  13. Kujitegemea kama msingi wa maendeleo ya watu,
  14. Azimio la Arusha nalo lilikuwa tunu muhimu mno.
Pamojana tunu zingine unazozijua weye na pengine sahihi zaidi kuliko hizi nilizotaja,nchi yetu imebarikiwa kufikia hapa ilipo kwa kuwa tunu hizo zilienziwa kwamujibu wa tawala za awamu nne tangu kipindi cha mapambano ya kupigania uhuruwetu. Kitendochochote cha kuhatarisha na kuziharibu tunu hizi ni kuitikisa nchi kunakoitianyufa za kimustakabali. Kwa leo naishi hapa. KARIBU TUJADILIANE
 
Back
Top Bottom