Tunu ya taifa: Majuto ni mjukuu; mimi, wewe na yule tuchukue hatua, tusijilaumu!

James Lupondo

Member
Sep 22, 2015
11
2
TUELIMISHANE,TUKOSOANE,TUJIBIZANE,TUSHAWISHIANE,TUSHABIKIE,TUHOJIANE KWA HOJA,UPENDO,USIKIVU,HESHIMA,UTU,UBINADAMU...


AMANI NI MSINGI WA MAENDELEO YA WANANCHI WA JAMII,NCHI,UKOO,FAMILIA,MTU MMOJA MMOJA...
Tuna kila sababu ya kuienzi kwa namna yeyote huku kila mtanzania mzalendo akishiriki kwa akili,mwili,roho,ufahamu hali na mali kuilinda na kuhakikisha inasimamiwa kikamilifu na wenye dhamana kimamlaka.

Ipo mitazamo na tafsiri nyingi juu ya mapana ya amani yetu,mfano kuwa imejengwa kwa misingi ya uvuilivu,woga,upole,ujinga,kukubali yaishe n.k. Hata hivyo amani ni amani na amana pia tunu kuu la taifa lolote linalokuwa au kuimarika kisayansi,kijamii,kiuchumi,kiutamaduni na kisiasa.Ni kweli nchi yetu imepika katika mipevuko mbalimbali ya kimaendeleo inayopelekea chachu chanya za kuendelea zaidi na zaidi hususani maboresho ya mifumo ya utoaji huduma,usimamizi wa rasilimali,uwajibikaji,uadirifu na ushiriki uliotukuka wa utatuaji wa kero nyingi za wananchi zikiwemo ajira,umaskini,njaa,afya,nishati n.k.

Sababu kuu zinazopelekea nchi nyingi kupoteza amani na mshikamano ni Kugombea madaraka,kughaghania madaraka,ukoloni mamboleo,uporaji wa rasilimali ,udini,uagaidi,ukabila n.k zimekuwa sababu kuu za ukosefu wa amani ya kimaendeleo ktk vipindi fulani kwa nchi ndugu na jirani za kiafrika.Mataifa mengi yanayotuzunguka ama kwa bahati mbaya au makusudi ama kwa kugombanishwa la kwa chuki zilizoshindwa kudhibitiwa walijikuta ama wamejikuta kwenye machafuko,vurugu,vita n.k

Madhara ya vurugu,machafuko ya kisiasa pindi yatokeapo ni makubwa mno na hudumu kwa muda mrefu sana yakiathiri sekta mtambuka na hususani wananchi kwa ujumla.Ukosefu wa huduma,uharibifu wa miundombinu,uporaji,fujo,ukatili,Vifo, kukatika mawasiliano,kufungwa kwa vituo vya huduma,wananchi kushindwa kujihusisha na shughuri za kuingiza kipato [kilimo,biashara,uvuvi,uzalishaji],athari za kisaikolojia,kiafya,kiimani n.k

Kila mtanzania anayo haki ya kumkemea,kumpinga,kumkosoa kwa nguvu na ujasiri yeyote ambaye kwa makusudi anadiriki kuchochea uharibifu wa amani tulionayo..awe baba,mama,kaka,shangazi,binadamu,mwalimu,mwanahabari,kiongozi,mtemi,mfalme,chifu,katibu,mjumbe,mwenyekiti,mchungaji,sheikh,imamu,askofu,Rais,waziri,mgombea,mwanajeshi

Tunazo fulsa lukuki za kudai haki zetu kwa amani,kupigania haki zetu kwa amani,Kushawishi matakwa yetu kwa amani,Kupaza sauti zetu kwa amani....

TUITUNZE AMANI YA NCHI YETU,TUSHIRIKI KUHUBIRI AMANI,TUWE CHACHU YA AMANI....AMANI IKIKOSEKANA POPOTE IWE KWENYE MAHUSIANO,NDOA,KIKUNDI,FAMILIA,UKOO,BIASHARA,TAASISI HAKUNA LINALOWEZA KUFANYIKA,KUBORESHWA,KUENDELEZWA...TUELIMISHANE,TUKOSOANE,TUJIBIZANE,TUSHAWISHIANE,TUSHABIKIE,TUHOJIANE KWA HOJA,UPENDO,USIKIVU,HESHIMA,UTU,UBINADAMU...
 
Watanzania kwa asili ni wavumilivu. Kwa hali ya maisha ilivyo, nchi nyingine pangekuwa hapatoshi. Chezea njaa wewe. Ukiwa na njaa kisha uniambie una amani, ni kutojua maana ya neno "amani"
 
Back
Top Bottom