Tunu Pinda kamuuliza Mh. Mizengo Pinda swali kwenye mkutano wa hadhara

Maisha ya maigizo kwa viongozi wakubwa wa TZ niliyaona mapema tangu kuzaliwa, shikilia ulipo, nchi ni ya wenyewe ambao wamejipa UmUnGu.
 
Na uhakika huwa wanatembea tu kuona tz lakini wakija wanauliza maswali wanatuacha na shida zetu wanarudi kwenye viyoyozi dsm.
nilimuona kule ukerewe eti anamuuliza maswali mkurugenzi mtendaji hadharani ....utafikiri hawana ofice huu mtindo pia alikuwa nao jk yeye kesha usahau

Huu si mtindo mzuri kwani pale PM yupo ziara ya kiofisi anavyofanya vile kumuuliza maswali Mkurugenzi wakati vitu vingine vinahitaji evidence toka kwa wataalamu wake anakuwa hamtendei haki na mdio maana kukawa na kikao cha majumuisho ili kama kuna kero wanazungumza pindi panapokuwa na tatizo hapo sasa inawekwa public ili kila mtu ajue kuna uchakachuaji hapa lakini kwa mtindo huu wanawadhalilisha watumishi wa serikali kiasi kwamba wanaonekana si kitu mbele ya viongozi wa kitaifa wakati wao ndio majembe muhimu (wao wakiulizwa maswali mengi kama ni magumu na yanaonyesha kero za wananchi hazijajibiwa wanakuja juu utasikia "UMETUMWA WEWE"
 
Huko ndo kujitekenya mwenyewe afu unacheka. Waacheni wahangaike tu. very soon wataanza kujifinya wenyewe afu wanalia!

h Teh teh teYou made ma day comrade...... Yanga waliniharibia week end yangu kwa ku draw na kibonde prison. Angalau wewe umenipa fya ya mapafu.
 
Usanii usanaii tuu.
Ni sawaawa na Pinda angejiuliza swali alafu angelijibu yeye mwenyewe.
 
Ndiyo siasa ya nchi yetu, usanii mtupu. Bila shaka, pinda na mkewe walichokifanya walipanga kabla ya tukio.
 
Alikuwa hajasikia swali aliloulizwa na mmoja ya waliopo mkutanoni, Tunu kalirudia tu.

Mkuu kwani PM hana wasaidizi???? Ilikuwa ni muhimu kutumia mic????

Mapenzi ya aina hii kwa viongozi huwaharibu.......kwa hili amechemsha na aambiwe wazi kuwa ile haikukaa sawa
 
ni MAGU alikuwa na msafara wa magari kama mia na kitu. Pia aliulizwa swali na mama mmoja kuhusu serekali kutangazia wananchi huduma za kujifungua ni bure ili hali hospt hakuna hata glovis na pamba,Pinda hakuweza kumjibu

Isije ikawa ni Gamboshi huko! Yaani PM akashindwa kujibu kabisa hilo swali? Basi si mwanasiasa manake mwanasiasa hawezi kukosa majibu kwa kil swali.

Sasa na hii ya Mama Pinda kuuliza swali nayo mbona haiingii ubongoni? zomba anasema ati alikuwa akirudia swali; hivi kulikuwa hakuna waongoza hiyo shighuli ama hata wataalamu au viongozi wa eneo hilo ambao walitakiwa kulirudia hilo swali? Kuna vitu vingine vinasababisha utata usiokuwa na lazima yoyote.
 
Last edited by a moderator:
...POST DELETED....
Paw

Uhusiano na maswali yangu???? PM hana msaidizi wa kumkbusha maswali ya wananchi??? Na kama ni kumkumbusha ilikuwa ni lazima iwe loudly????? Ndo tunaanza kupata maswali mengi sasa yeye kauliza kama nani .........mpaka wake uko wapi......companion.....mke au msaidizi????

Wapemba husema ukupigao ndo ukufunzao...............................
 
cdm ni ngoma ivumayo,...
Kazi yenu ni kuponda kila lifanywalo na serikali ya ccm.
Mmekua kama waimba taarabu, wazee wa vidole juu, wazee wa mipasho.
 
Nimeona maajabu sana. Katika ziara za Waziri mkuu wa Tanzania kanda ya ziwa kaambatana na mkewe. Baada ya kuona Raia hawamuelewi waziri mkuu, Tunu Pinda ikabidi aulize swali kwa niaba ya wakazi wa sehemu husika.
Aliuliza;
Sisi wanawake wa hapa tunapata tabu sana katika kuchota maji hadi nywele za katikati hazikui sababu ya kujitwisha chungu, je serikali itatusaidiaje?.
Waziri akajibu;
Nimeambiwa zinahitajika mil 200 kuondokana na tatizo, hizo mil 200 nitawapeni bila tatizo.
Hii imekaaje?. mia

We ulitaka ikaeje, amesema kaambiwa zinahitajika mil. 200, inamaanisha viongozi wa serikali wa eneo husika wamesha mueleza matatizo ya wananchi wa eneo husika.
Huo ni unafiki!! Kurukia kauli za watu na kupotosha maana.
 
Uhusiano na maswali yangu???? PM hana msaidizi wa kumkbusha maswali ya wananchi??? Na kama ni kumkumbusha ilikuwa ni lazima iwe loudly????? Ndo tunaanza kupata maswali mengi sasa yeye kauliza kama nani .........mpaka wake uko wapi......companion.....mke au msaidizi????

Wapemba husema ukupigao ndo ukufunzao...............................

Hivi huyo si msaidizi wa Slaa wa kumkumbusha? Kama jibu ni ndio, kwanini iwe mwao kwa Pinda?

Mkewe hana haki ya kumkumbusha? mbona mkitaka michango mnamtumia? au umesahau, alivyopigania michango ya timu ya netiboli ya wanawake Tanzania?

Hivi wewe una mke au mume nyumbani? au bado hujaoa au kulewa? kama huna na bado, basi ukikuwa utayajuwa majukumu ya mke kwa mume ni yepi.
 
tatzo viongoz wana wafanya watz kama MIFUGO.....na hl ni kosa kubwa kwa wananch
 
Back
Top Bottom