Tuntemeke Sanga: Mbunge aliyekuwa na elimu ya Shahada 7, aliyechachafya miaka ya zamani

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
49
Ndugu wana mtandao wa JF, nimekaa na kumkumbuka huyu mzee Tuntemeke Sanga ambaye nasikia alikuwa na degree saba (km ni kweli) na mbaye alikuwa matata sana bungeni enzi zileee.

Je kuna mtu nafahamu habari zake atujuze?
*******

FAHAMU HAYA MACHACHE KUHUSU MZEE TUNTEMEKE SANGA
Asubuhi ya Jumatatu, tarehe 8 Desemba 1930 huko Lupaso, Kijiji cha Bulongwa, Njombe, alizaliwa mtoto wa kiume mwenye afya tele. Mtoto huyo, ambaye alikuja kuweka historia ya kipekee nchini, si mwingine bali ni TUNTEMEKE MESAKA NNUN'GWA SANGA

1.jpg

Tuntemeke Mesaka Nnun'gwa Sanga

Wazazi wake, Bw. na Bi SANGA, walikuwa ni watoto wa Chifu. Watoto wengine wa wazazi hao walikuwa ni RWIJISO, ANNA, GEOFREY na ALFRED (Mwenyekiti wa Simba SC 1979-1982).

Tunte alianza shule ya msingi mwaka 1942 huko Njombe akiwa na miaka 12 kama ilivyokuwa kwa Mwalimu J.K. Nyerere.

Alifanya mtihani wa darasa la 4 na kufaulu na hivyo akaendelea "middle school" hadi 1946 alipofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi huko na kufaulu. Alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mwaka 1947 na kumaliza mwaka 1950 ambapo alifaulu vizuri sana. Kidato cha tano na sita alisoma shule ya "Tabora Boys" kuanzia mwaka 1951 hadi 1952.

Baada ya hapo akasomea ualimu(kazi iliyokuwa na heshima sana enzi hizo kwani hata Mwalimu Nyerere alikuwa mwalimu pia). Tunte, baada ya kupata cheti cha ualimu, akaenda kufundisha shule ya sekondari ya Ilboru.

Akiwa kijana mdogo wa miaka 26, alikuwa mmoja wa Watanganyika wa kwanza kwenda kusoma Marekani kwani alipata fursa hiyo mwaka 1956. Alikuwa kijana mwenye IQ ya kipekee na malengo yasiyo ya kawaida ambapo alidhamiria kusoma fani mbalimbali kwa kadri itakavyowezekana.

Dhamira hiyo ilimfikisha katika vyuo mbalimbali nchini humo vya Gustav Adolphus, Chicago, Columbia na Princeton.

Dhamira hiyo hiyo ya aina yake ndiyo iliyomuwezesha kuwa Mtanganyika wa kwanza na pekee kupata shahada 7 za fani za Biashara, Uhusiano wa Kimataifa, Utawala, Sheria, Kilimo, Sayansi ya Jamii na Dini. Kuhusu dini alikujakusema mwenyewe bungeni tarehe 24.8.1993 - "Nikiwa Marekani nilijifunza na nayajua sana masuala ya dini kwa upande wa Wakristo, Waislamu na Bhuda"

Tunte pia alikuwa akifundisha na kutoa mihadhara kwenye vyuo mbalimbali nchini humo na alikuwa na uwezo mkubwa wa lugha akiongea kwa ufasaha Kiingereza, Kiswahili, Kijerumani na Kifaransa. Mwaka 1962, alianza masomo ya PHD huko "Yale University". PHD hiyo ilihusu maendeleo ya utendaji vijijini. Kozi hiyo ilimpasa kwenda pia chuo cha Nuffield, UK na Chuo Kikuu cha Dsm.

Alirejea nchini mwanzoni mwa mwaka 1964 akawa Afisa Uhusiano wa kampuni ya Riddoch Motors (1964-1965). Aidha, kwa mikono yake, akajenga nyumba kijijini Bulongwa.

Tarehe 20.9.1964, alifunga ndoa na Bi. BETTY ANN FITZGERALD, Mmarekani mweusi aliyezaliwa Marekani mwaka 1939. Ndoa hiyo ya kukata na shoka ilifungwa huko Bulongwa baada ya Tunte kulipa mahari iliyojumuisha ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku. Kwa hakika ilikuwa harusi ya aina yake ambapo watoto 122 waliovalia nadhifu waliwarushia maua maharusi hao, waliokuwa wamevaa nguo maridadi za kiafrika zilizotengenezwa nchini Ghana, na kuwaimbia nyimbo kedekede za Kikinga na Kizungu.

Wazee kwa vijana, kwa wiki nzima, walisheherekea ndoa hiyo huku wakila beche lililopikwa kwenye mapipa 15 na pombe ya ulezi iliyokuwa "ya kumwaga". Ilikuwa ni harusi ya kihistoria ambayo, hadi leo, haina mfano wake Bulongwa! Aidha, harusi hiyo iliweka rekodi ya kuwa harusi ya kwanza Tanzania kuandikwa, kwa mapana na marefu, kwenye gazeti maarufu la Marekani (The New York Times la tarehe 1.11.1964 chini ya kichwa cha habari: "Pittsburgh Girl's Wedding in African village")!.

Alimuona kwa mara ya kwanza Bi. Betty alipoenda kutoa mhadhara huko Pittsburgh, Marekani mwaka 1960 ambako ndio kwao Bi. Betty, msomi mwenye shahada ya uzamili. Baada ya uchumba wa miaka 4, wawili hao ndipo walipooana.

Tunte akaanza kufanya shughuli mbalimbali za biashara, kilimo, sheria na pia akajiingiza kwenye siasa ambayo ilikuja kumletea matatizo makubwa na Mwalimu Nyerere.

Kwa kusoma Marekani kwa muda mrefu, aliamini kwamba siasa ya Ujamaa ni feki na haiwezi kuleta maendeleo na hakuwa akificha msimamo huo licha ya kuwa mwana-TANU iliyokuwa ikiamini katika Ujamaa.

Alieleza kwamba yeye ndio anafaa kuwa Rais hivyo Mwalimu Nyerere ampishe ili ailetee nchi maendeleo kwa falsafa za ubepari na abadili "mentality" ya wananchi wa Tanzania ambao wengi ni wavivu wapendao kujirusha na kuoneana wivu. Alidai shahada zake 7 zilimfanya awe na fikra sahihi za kuleta maendeleo kuliko Mwalimu aliyekuwa na shahada mbili tu na muumini wa ujamaa aliouona "unailostisha" nchi!.

Hiyo ilimkera mno Mwalimu ambaye, kwa kutumia "The Preventive Detention Act, 1962", alimsweka mara moja Tunte kizuizini kijijiji kwake Bulongwa na kumuamuru kutotoka kijijini hapo hadi apate kibali maalumu.

Tunte alikuwa kizuizini Bulongwa kwa miaka mingi na hii ilipelekea ashindwe kumaliza kozi yake ya PHD ambapo miaka ya baadae alipenda kutania: "Mimi ni PHD Candidate. Nilirudi nchini ili nifanye utafiti kuhusu PHD yangu lakini nikawekwa kizuizini kwa miaka mingi hivyo nikashindwa kuikamilisha ndio maana najiita "DR. MTAHINIWA"!.

Mwalimu Nyerere, baada ya miaka mingi, alimsamehe Tunte ambaye aligombea ubunge jimbo la Makete mwaka 1980 na kushinda kwa kishindo. Akiwa bungeni, alikuwa mtata sana huku akiwapeleka puta mawaziri na hata maspika.!

Siku moja Bunge lilipokuwa pale Karimjee Hall, Dar Es Salaam, Tunte alitinga na suruali ya "jeans" na shati la kitenge. Maofisa wa bunge hawakumruhusu kuingia ndani kwani hilo halikuwa vazi rasmi la bunge. Tunte akaondoka lakini akarudi na shati zuri lilishonwa kiwanda cha Nguo Urafiki lakini akiwa amevaa kaptura! Walinzi, kwa mara nyingine, wakamzuia lakini hakukubali hivyo ukazuka mtafaruku wa "kufa mtu"!. Spika, Adam Sapi Mkwawa alipoingilia kati, Tunte alimjia juu na kutaka amuoneshe Kifungu cha kanuni alichovunja. Hatimaye ilibidi arudi nyumbani!.

Kuna wakati Tunte alipewa dakika 15 tu na Spika Pius Msekwa aongee lakini akazidisha na kutumia dakika 30. Msekwa alipomtaka akae, Tunte aliyemzidi Msekwa miaka 5 kiumri, alihamaki na kusema; "Hivi kwenu hakuna Wakubwa? Huoni mambo niyaongeleyao ni muhimu kwa wananchi wetu?" Ukumbi mzima wa bunge ulizizima kwa vicheko na hata Msekwa mwenyewe aliangua kicheko na hatimaye Tunte akakaa!.

Tunte alikuwa mtu wa msimamo mkali asiyeyumbishwa wala kuogopa kusema alichokiamini na aliheshimiwa sana na Wabunge wenzake na aliposimama bungeni hata waliokuwa nje walikuwa wakirudi ndani kumsikiliza kwani alipenda sana kujenga hoja baada ya kufanya tafakuri tunduizu !.

Wananchi wa Makete walimpenda sana na alishinda ubunge mara zote alizogombea. Aliweza kuongea Lugha za Kikinga, Kibena, Kihehe na Kinyakyusa kwa ufasaha.

Mwaka 1995 alikuwa mmoja wa wana-CCM waliochukua fomu kugombea Urais. Hii ni kwavile alitaka kutimiza azma yake ya kuliongoza Taifa hili kama alivyomwambia Mwalimu Nyerere ambae aliamua kumuweka kizuizini. Wengine waliochukua fomu walikuwa J. Warioba, N. Kasaka, M. Bomani, J. Malecela, C. Msuya, H. Kolimba, R. Lugendo, J. Kikwete, E. Lowasa, R. Fred, K. Malima na B. Mkapa aliyechaguliwa kuipeperusha bendera ya chama na hatimaye kuwa Rais wa awamu ya tatu.

Tunte alianza kupata matatizo ya macho muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha bunge mwaka 1996 Dodoma na akapelekwa hospitali ya Muhimbili ambako alilazwa. Mwezi Julai 1996, alipelekwa London, UK kwani aliishapoteza uwezo wa kuona kwa 95% ambako alifanyiwa operesheni ya macho.

Wizara ya Afya ikamrudisha nchini kwa kudai ilikuwa imemaliza fungu ililotenga kwaajili ya matibabu yake hivyo akalazwa wodi ya Mwaisela mwezi Septemba 1996 baada ya kurejea nchini mwezi Agosti 1996. Alikuwa hawezi kumtambua mtu kwa kumuona bali kwa sauti tu. Viongozi wa serikali, Mh Dkt. Omari na F. Sumaye walimtembelea wodini hapo kumjulia hali.

Mwanzoni mwa mwezi Octoba 1996, akatolewa hospitalini. Katikati ya Juni 1997, alikimbizwa hospitali ya Aga Khani ambako alilazwa ICU kwa wiki 2. Akafariki saa 7 usiku wa Jumatano, tarehe 2.7.1997 akiwa na umri wa miaka 66.

Aliyekuwa Naibu Spika, Phillip Marmo alilitangazia bunge kesho yake asubuhi kuhusu msiba huo mkubwa na kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na moyo. Simanzi kubwa ikashamiri bungeni.

Jijini Dar es Salaam, shughuli za mazishi ziliendeshwa na Brigedia Jenerali Peter Ligate na msiba ulikuwa mtaa wa Mansfield kwa mdogo wake, Alfred Sanga

Mwili wake uliagwa Muhimbili jumamosi ya tarehe 5.7.1997 ambapo Rais Mkapa aliongoza mamia ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho ambapo alisema:

"Kifo cha Sanga kimetuondolea kiongozi mashuhuri ambaye ametoa mchango mkubwa wa maendeleo si tu Makete bali nchi nzima kwani alikuwa Mzalendo mwenye uchungu mkubwa na nchi yake. Hakuwa mwoga bali alikuwa mkweli daima. Nafasi aliyoiacha itakuwa ngumu sana kujazwa na kwamba mchango wake katika taifa hili utaandikwa katika historia ya nchi yetu".

Mwili wake ulisafirishwa kwa ndege na akazikwa kijijini Bulongwa Jumapili tarehe 6.7.1997. Wakati huo alikuwa ameachana na mkewe Bi Betty. Msiba huo ulihudhuriwa na watu wengi huku Wabunge 4 waliwakilisha wenzao. Wabunge hao walikuwa T. Nyimbo, J. Makweta, M. Kibassa na J. Nhunga aliyekuwa Katibu wa Wabunge wa CCM.

Huyo ndiye TUNTEMEKE MESAKA NNUN'GWA SANGA aliyeacha historia ya kipekee nchini!.
*********

Pia soma: Tuntemeke Mesaka Nnnung'wa Sanga na Hoja ya Muungano mwaka 1993 - JamiiForums
 
Namfahamu hadi kwake na baadhi ya watoto wake, wake zake wawili wote nawajua. Wa kwanza mzungu alichapa kona baada ya kumlazimisha aende kuchota maji kama kilomita 12 hivi tena mlimani, huyo ni black American. Wa pili ni chotora wa kijerumani; huyo alimpa talaka baada ya kuona ana_do pembeni na vijana wenzie.

TUNTE alisoma shule za mission akapata skolaship kwenda Marekani, huko amesoma digrii nyingi sana za sheria. Inasemekana IQ yake ni juu mno.

Vs Nyerere na TZ

Akirudi toka USA, alikuwa tayari ni bepari kiitikadi, Nyerere siku hizo alikuwa tayari amefuatilia na kumjua vizuri, hiyo ni miaka ya 70 hivi.

Kumbuka Nyerere ailkuwa ni mjamaa wa kufa mtu.

Aliporudi TZ, Nyerere aliwaza sana kazi ya Kumpatia lakini alishindwa kutokana na jamaa kuwa na itikadi ya kibepari live. Ndipo alimuacha mtaani kwa muda,

KOSA

Ndipo Tuntemeke Sanga akiwa anakaa Mwenge alianza kujulikana kama yeye ni msomi kuliko Nyerere na habari zikasambaa TZ yote.

Muda huo kulikuwa na tetesi kuwa Nyerere amemuuliza kazi gani anataka yeye TS akasema URAIS. Ndio mana hakupewa kazi kama wenzake.

Ukweli ni kwamba, kulikuwa na habari za kijasusi kuwa weupe walitaka kumtumia yeye na wenzake kusababisha machafuko kusini ya TZ ili ijitenge na iwe nchi ya kibepari, wenzake wakasepa kabla ya dili kubumbuluka; yeye alikamatwa na kuhojiwa sana na Nyerere mwenyewe. Kwa kuwa alikuwa vizuri upstairs, alimshinga Nyerere kwa hoja.

Adhabu

Nyerere alimwambia atakaa kijijini Bulongwa na asifike Njombe wala Mbeya. Hakuona LAMI mpaka 1980.

Hapo habari ni ndefu tena, ila kifupi ni kwamba,
baada ya wazee kuomba Wilaya ya Makete ndio Makweta alikwenda kwa Nyerere kutoa ripoti kuwa jamaa amechenji sana hata ni mwenyekiti wa kijiji cha ujamaa, Nyerere akaona jinsi kijiji kilivyoendelea akamkubali agombee ubunge na akapita. hiyo ni miaka ya 80 hivi.

Kuanzia apo akapewa ruksa kutembea TZ yote na dunia nzima.

Baada ya hapo habari zake zote zimerekodiwa kwenye hansadi, kumbuka aligombea URAIS mwaka 1995 na akina Mkapa.

BBC news, Mbunge wa Makete akiwa amevaa kinadhifu kuliko wote na Kujibu maswali kiufasaha ameshindwa kwenye kinyanyiro cha kumpata mgombea wa CCM kwa kiti cha urais katika duru ya kwanza, matangazaji akiongea kwa huruma

Tuntemeke alizikwa Bulongwa, William Lukuvi aliiwakilisha serikali kwenye mazishi yake.

MY TUNTE
 
ANKOJEI

Naona kunaupotoshaji wa habari hapa. Tuntemeke sanga alizaliwa Bulongwa 1926 ndugu yake aliitwa Alfred Sanga aliyewahi kuwa kiongozi wa Yanga katika miaka ya 70.

Alisoma Bulongwa PS nakuendelea na masomo ya seko huko Malangali na Ilboru. Alionyesha weledi na uwezo mkubwa katika masomo na wakati akirudi likizo aliweza kuhubiri kwa ufasaha neno la Mungu, hivyo kanisa likampa scholarship kwenda Uingereza kusomea uchungaji-theolojia ili akihitimu aje awe mCHUNGAJI lakini alipofika ughaibuni alikata kona na kuingia mtini kuelekea Marekani ambako alijisomea digrii nane katika nyanja mbalimbali kama uchumi, siasa na sheria kwa miaka saba kuanzia 1956 hadi 1962.

Kinachoshangaza watu ni kwanini hakuamua kusomea PhD na badala yake akasomea digrii zote ambazo apparently zinaonekana zilikuwa bachelor degrees. Kwa hakika hakuna anayejua labda nduguze.

KUHUSU MKEWE MNIGA, NI KWELI ALIOA MWANAMKE KUTOKA MAREKANI LAKINI SIYO KWELI KUWA ALITEMBEA KM 12 KWENDA KISIMANI HUU NI UONGO MKUBWA KWANI WILAYA YA MAKETE KUNA MITO NA VIJITO VINGI NA ENEO ANALOTOKA LA KITONGOJI CHA LUPASO VJITO VIKO JIRANI TU HATA MTO LUHANGA AMBAO NI MKUBWA UKO TAKRIBANI KM 2.5 HIVI KUTOKA LUPASO.

SASA HUYU BWANA ANAPOSEMA ANAMFAHAMU MPAKA NA ANASEMA UONGO MAJI YANAKOPATIKANA NAONA ANATIA CHUMVI KATIKA HABARI SIYO KWELI. UKWELI NI KUWA HUYO MWANAMKE HAKUWEZA KUMUDU KUFUATA MAJI KISIMANI KWANI KWAO WAMEZOEA TAPE WATER TENA JIKONI NA SIYO KISIMANI
 
NASIKIA eti alimwambia nyerere kwamba anataka kazi yake,na alikuwa na shamba pembeni ya jkt mafinga,akikuta footprint ya boot ya jeshi shambani kwake anakimbilia mahakamani kudai hela-amepiga kitabu na ex president wa sudan Nimery
 
Asili yake ni Bulongwa-Makete. Mbunge wa kwanza jimbo la makete,alitetea "zao" la bangi kuwa ni mboga ya kawaida. Kimsingi,inapatikana kwa wingi maeneo ya kikondo-makete!

mkuu... hili ni zao la biashara au chakula ..kwa mujibu wa Tuntemeke Sanga
 
Wazee kama hawa inabidi waenziwe umesahau jina moja hapo Nungwa wazee wa kinga ndilikinga lakini ndiliva huborn town
 
  • Thanks
Reactions: A2G
Hivi huyu si ndo tuliambiwa alikuwa msomi kuliko watanzania wote nchini? Elimu yake (kama kweli) imetusaidia vipi wana Makete na Tanzania kwa ujumla?

Nyerere nasikia alimchimba nmkwara hakuna kufika Dar yeye mwisho Moro na kuelekea Dom kwa hiyo elimu amekufa nayo.
 
Namkumbuka sana yeye na Njelu Kasaka walikua popular at one time. Sijui na Njelu Kasaka yuko wapi?

Ndugu wana mtandao wa JF, nimekaa na kumkumbuka huyu mzee Tuntemeke Sanga ambaye nasikia alikuwa na degree saba (km ni kweli) na mbaye alikuwa matata sana bungeni enzi zileee.

Je kuna mtu nafahamu habari zake atujuvye?
 
Tumtemeke Sanga aliwika sana enzi zake. Mzee alikuwa machachari huyo acha kabisa. Nyerere alionja joto ya jiwe enzi hizo. Teh teh teh kwa kusoma habari hii imenifanya nisahau kidogo machungu ya habari za Dowans, Mauaji Arusha na habari za mama sijui mnamwita Chitanda au Chiwanga what ever her name is anachafua hali ya hewa huyu mama. Hivi ameolewa au ni single maana hasira zake kama vile ana hasira ya kitu furaaaaaaaaaaaaaaaaani vireeeeeeeeeeeeeee!

Asante kwa aliyeanzisha habari ya huyu ndugu yetu Sanga mzee wa shughuli.

RIP Mzee wetu.
 
Teh teh teh kwa kusoma habari hii imenifanya nisahau kidogo machungu ya habari za Dowans, Mauaji Arusha na habari za mama sijui mnamwita Chitanda au Chiwanga what ever her name is anachafua hali ya hewa huyu mama. Hivi ameolewa au ni single maana hasira zake kama vile ana hasira ya kitu furaaaaaaaaaaaaaaaaani vireeeeeeeeeeeeeee!
Pakawa, Ni Mary Chatanda yeye ni Mke wa mtu Bwana mmoja somebody Chatanda wa Iringa yeye ni Katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Iringa ni mbena wa Njombe Lupembe.

Mary Mnyakyusa wa Kyela Mbeya ni Mamamwa watoto wanne, lakini hivi sasa kuna matatizo kwenye ndoa yao na ndio chanzo cha kutengana, wametengana kwa muda takriban miaka sita sasa kila mtu kivyake.
 
Pakawa, Ni Mary Chatanda yeye ni Mke wa mtu Bwana mmoja somebody Chatanda wa Iringa yeye ni Katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Iringa ni mbena wa Njombe Lupembe. Lakini Mary Mnyakyusa wa Kyela Mbeya ni Mamamwa watoto wanne. lakini hivi sasa kuna matatizo kwenye ndoa yao na ndio chanzo cha kutengana, wametengana kwa muda takriban miaka sita sasa kila mtu kivyake.

Hapa sasa tunaanza kupata Picha, hayo ya BLUU inaonyesha kuwa ana STRESS za maisha na jana niligusia kuwa huenda hapati HAKI YAKE.

Mara nyingi watu wa aina yake huwa wakali na hawapendi kabisa kusogelewa maana WAMEJERUHIWA KIMAPENZI.

Sasa angepatikana kijana wa kumliwaza asingekuwa na tabia hizi. lakini nahisi pia kuwa ni mgumu wa TABIA na ndio maana anaishi kivyake hadi sasa miaka sita imepita.
 
Back
Top Bottom