Tungekuwa na Marais wengine wenye uthubutu na ujasiri kama Hayati Magufuli tungekuwa wapi kimaendeleo hii miaka 60?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Hayati JKN siwezi kumlaumu sana maana wakati akitawala enzi hizo nchi nyingi zilikuwa bado hazijajitambua na mkono wa mataifa ya nje ulididimiza mataifa ya kiafrika.

Chukulia tu kwa awamu tatu zilizopita kila moja ingethubuti kutekeleza miradi mikakati mikubwa ya maana ya kimaendeleo leo tungekuwa wapi?

Sgr hii ambayo leo hii tunaihangaikia ingeanza wakati wa Mzee Mwinyi leo tungekuwa hatujamaliza? JNHP ingeanza wakati wa Mzee Kikwete tungekuwa hatujamaliza?

Taifa letu linahitaji viongozi wenye uthubutu ili tujikwamue.

20220216_033148.jpg
 
..SGR isingeweza kuanza wakati wa Mzee Mwinyi kwasababu barabara zetu zilikuwa na hali mbaya sana.

..wakati wa Mzee Mwinyi, majira ya mvua kusafiri kwenda mikoa ya kusini ilikuwa ni mtihani mkubwa sana.

..Magufuli na Kikwete ndio Maraisi ambao waliingia madarakani nchi ikiwa ktk hali nzuri ya kiuchumi hivyo ni sahihi kwao kufanya mambo makubwa kuliko watangulizi wao.
 
Pia tusipoteze muda na kesi za kisiasa za michongo mahakamani kama za Sugu, Lema, Msigwa n.k
 
Tunahitaji Katiba mpya zaidi kuliko kitu kingine chochote.
 
Hayati JKN siwezi kumlaumu sana maana wakati akitawala enzi hizo nchi nyingi zilikuwa bado hazijajitambua na mkono wa mataifa ya nje ulididimiza mataifa ya kiafrika.

Chukulia tu kwa awamu tatu zilizopita kila moja ingethubuti kutekeleza miradi mikakati mikubwa ya maana ya kimaendeleo leo tungekuwa wapi?

Sgr hii ambayo leo hii tunaihangaikia ingeanza wakati wa Mzee Mwinyi leo tungekuwa hatujamaliza? JNHP ingeanza wakati wa Mzee Kikwete tungekuwa hatujamaliza?

Taifa letu linahitaji viongozi wenye uthubutu ili tujikwamue.
View attachment 2120610

Tungeuzwa kwa madeni. Siasa zile za kishamba zilishapitwa na wakati.
 
Ogopa sana kinywa ambacho hakikiri udhaifu!

Udhaifu na kushindwa kwetu, upon mikononi mwetu, aonavyo MTU nafsini, ndivyo alivyo

Endeleeni kukiri Tanzania ni nchi masikini badala ya watanzania ndio masikini na wanahitaji mtu wa kugeuza utajiri wa nchi yao kuwaondolea umasikini wao!

Tanzania siyo nchi masikini

Pumzika kwa amani Mwamba wa Africa JPM
 
Watakupinga.
 
Back
Top Bottom