Tungekuwa na Katiba inayotaka Mawaziri wasiteuliwe, Mwigulu Nchemba angetufanyia dharau namna hii?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Msomi wa hadhi ya Phd ya uchumi bila aibu anaongea mbele ya luninga ya taifa kuwa serikali ikilipa madeni kutakuwa na mzunguko wa pesa hivyo mzigo wa tozo za miamala ya simu utakuwa stahimilivu. Hii ni dharau kubwa.

Mkandarasi akilipwa madeni na serikali kweli pesa inaingia kwenye mzunguko. Lakini ndio sababu ya kuondoa mzigo wa kodi? Je huo mzunguko wa pesa utamfikia kila mwananchi kwa usawa?

Kwa namna ya dharau aliyonayo Mwigulu kwa watanzania ipo haja kuwa na katiba inayotaka mawaziri kuwa na ajira za mikataba akileta dharau na upuuzi wananchi wanamtimua.

Ndio maana watu kama akina Mwigulu hawataki katiba mpya.
 
Sidhani kama unastahili kujibiwa
Anastahili kujibiwa akimanisha jino kwa jino lakini sini kweli kabla ya sim banking nini ilitumika hakuna mwananchi anataka kurudi huko tufanyaje kama serikali inataka kutufikisha huko au wewe unaona ipi njia mbadala ya kumpunguzia mwananchi makato makubwa kiasi hichi?
 
Acheni kutumia simu kelele za nini ,watanzania ni wajinga sana kwani kabla ya simbank hamkutuma pesa


USSR
Kwa vile mababu zetu walivaa magome ya miti hivyo sasa turudie huko kwa vile bei za nguo ziko juu siku hizi,huna adabu kabisa kuwaita Watanzania wajinga.
 
Wewe ndiye mjinga na ukoo wako wote,kwa vile mababu zetu walivaa magome ya miti hivyo sasa turudie huko kwa vile bei za nguo ziko juu siku hizi,huna adabu kabisa kuwaita Watanzania wajinga.
Lipa sasa utakaaunapiga kelele na mmeo mpaka lini?

USSR
 
Msomi wa hadhi ya Phd ya uchumi bila aibu anaongea mbele ya luninga ya taifa kuwa serikali ikilipa madeni kutakuwa na mzunguko wa pesa hivyo mzigo wa tozo za miamala ya simu utakuwa stahimilivu. Hii ni dharau kubwa...
Wazo lako inaweza kuwa ni jema, ila ningependa kuelimishwa ni wapi huko ambako Mawaziri hawateuliwi?
 
Malalamiko mengi akati simu si zaserikali simu ni zenu
Achaneni na biashara ya pesa kwanjia ya simu.
 
The current administration imekumbatia mfumo wa kibeberu wa kiuchumi.

Tax relief ipo Kwa matajiri ambao ni wachache majority wakiwa maskini ambao walifaidi awamu ya tano.

Sasa matajiri nao wanashangilia.

Rais aliposema Kodi ikusanywe kwa akili alimaanisha wale matajiri wasibugudhiwe.

Lakini anasahau kuwa anapoteza support ya wengi ambao ni maskini.

Sijui Kwanini Rais anafanya Kila jitihada za kukataliwa na majority??

Yaani Kila maamuzi yanalenga kuumiza wengi.

Totally unfair.
 
The current administration imekumbatia mfumo wa kibeberu wa kiuchumi.

Tax relief ipo Kwa matajiri ambao ni wachache majority wakiwa maskini ambao walifaidi awamu ya tano.

Sasa matajiri nao wanashangilia.

Rais aliposema Kodi ikusanywe kwa akili alimaanisha wale matajiri wasibugudhiwe.

Lakini anasahau kuwa anapoteza support ya wengi ambao ni maskini.

Sijui Kwanini Rais anafanya Kila jitihada za kukataliwa na majority??

Yaani Kila maamuzi yanalenga kuumiza wengi.

Totally unfair.
Alimaanisha au wewe umemaanisha?
 
Kwa namna ya dharau aliyonayo Mwigulu kwa watanzania ipo haja kuwa na katiba inayotaka mawaziri kuwa na ajira za mikataba akileta dharau na upuuzi wananchi wanamtimua.
Unachokisema hapo juu hakiwezekani kwa setup ya serikali. Hakuna nchi yenye kipengele cha katiba unachosema wewe? Hujiulizi kwanin? Taja nchi ambayo mawaziri hawateuliwi? Tunachotaka ni mawaziri wasiwe wabunge na pia wathibitishwe na chombo kingine kama seneti baada ya uteuzi wao (check and balance). Rais lazima aunde serikali ambayo atafanya nayo kazi. Sema tunatakiwa kuhakikisha aliyemteua anafit kwenye hiyo nafasi kwa kutumia vyombo vya uwakilishi. Kama hafai uteuzi unakataliwa anatafutwa mtu mwingine. Hicho kitu hakipo kwenye katiba kwa sasa na ndo kinafanya madaraka ya Rais yaonekane makubwa, sababu hakuna anayeweza kuzuia uteuzi wa Rais. Nchi kama Kenya kipo hicho kipengele
 
Tumeingia uchumi wa kati wa chini, nadhani muda si mrefu tutakuwa uchumi wa juu wa kati. Na lugha yetu tutaongea vizuri zaidi badala ya kusema "nirushie buku", tutasema "nitumie shilingi elfu moja tafadhari".
 
Tumeipenda wenyewe chaguo letu milele.. ndindiii wacha waisome namba eeeh ccm mbele kwa mbelee
 
We si uko ccm wewe??mwigulu nae si ccm?!sema KIMEUMANA.Mlifikiri watalipa wapinzani tuu???na bado tulieni mnyolewe bila maji
 
Back
Top Bottom