Tungekomaa na Ujamaa bila kuikumbatia SAP labda sasa hivi tungekuwa mbali

Tanzania Revenue Authority (Mamlaka ya Mapato Tanzania)​

Government agency


Description​

Description​

The Tanzania Revenue Authority is a semi-autonomous Government Agency of the United Republic of Tanzania. It was established by the Tanzania Revenue Act, CAP. 339 in 1995 and started its operations on the 1st of July 1996. Wikipedia
Headquarters: Sokoine Drive, Dar es Salaam
Key document: Tanzania Revenue Authority Act, 1995
Jurisdiction: Tanzania
Founder: National Assembly
Founded: July 31, 1995
Kweli mkuu
Mpe 5 mzee mwinyi
 
Kosa kubwa tulilofanya kama nchi ni kuzikumbatia sera za kipuuzi na angamivu za SAP hizi ndo zilikua kaburi kwa nchi yetu

Labda tungekomaa na ule ujamaa wa nyerere bila kupinda popote labda leo tungekua tumepiga hatua

Wenzetu China walikomaa na ujamaa na walivyopata matokeo na kufikia mahali pazuri sasa wakaruhusu ubepari sisi tulianguka mapema sana

Sasa hivi hata hatujui tupo kwenye dira gani nashindwa kujua mwelekeo wa nchi yetu kiuchumi ni aibu sana hadi leo tunategemea misaada

Sera za kishenzi za SAP ndo zimetufikisha hapa, alaaniwe aliyeasisi SAP huu ulikua ndo mwisho wa uchumi wa nchi yetu

Imagine ndo anakuambia ushushe thamani ya hela yako ambayo ilikua sawa na dola ya marekani leo hii hiyo dola ndo tunatumia kuagiza bidhaa nje yaani wanatupiga mara 2305 kwa dola moja daaah

Hii nchi sijui kama itakaa iendelee
Uko sahihi kwenye hizo SAP

Lakini kwa uchina kidogo hapana. Siasa inayoongoza nchi ya china ni ujamaa fulani wa kikomunisti. Lakini uchumi wa kichina is pure ubapari. Wachina wameweza kutofautisha hapo, na kwa sasa ukiangalia china uchumi wa kibepari ndiyo unaongoza siasa ya kijamaa, tofauti na sisi siasa isiyojulikana imesimamia wapi, siasa ya ccm ndiyo inayovuruga uchumi. Kila baada ya uchaguzi mkuu lazima uchumi uvurugwe, kisa amechaguliwa rais mwingine
 
Azimio la Arusha liliposhindwa ilikuwa ni kwa sababu ya SAP.Hivi China ni nchi ya kijamaa au ni taifa lenye chama kimoja tu kinachoendesha nchi kitemi.

Hakuna mtu aliyemuwekea kamba shingoni mwenzake kwamba ikubali SAP.Ukweli ni kwamba ni uzembe wa Nyerere kushindwa kujua maigizo ya siasa za kidunia ndio anguko letu.Kwani sisi si ndo wale tunadai tulipambania uhuru wetu 1961.Kama ndio, huo uhuru ulikuwa ukimanisha nini na SAP inakuwaje iwe shida kwa watu walio huru?Anyway,hakuna chochote cha maana tulifanya ata huo uhuru ni chenga tu hakuna cha Bibi Titi wala Mwalimu, ni muda tu ulikuwa upande wetu na mahesabu mabovu ya wakoloni basi.
No nyerere hakutaka kukubaliana na mpango wa Structural Adjustment Program (SAP),shida ni kuwa baada ya vita vya nduli, nchi ilifulia kwerikweri,,, kipindi hicho kighoma malima ndo waziri wa fedha,, Nyerere na malima hawakutaka kukubaliana na IMF,, so wazungu wakabana kutoa fedha,
Mambo yakawa magumu kwelikweli,, njaa, ukosefu wa ajira, madawa, etc
Nyerere akagoma,,,
Hali ikakaza zaidi, ikafuata na njaa ya 1984,, Nyerere amekaza tu, duh,, hatimae akang'atuka asee,
Ruksa alikuta hali mbaya kwerikweri,,, ,hakuwa na jinsi akakubalianana mpango wa SAP.
Yaani structure ya uchumi ibadilishwe, pawepo na uchumi huru, Private sectors iruhusiwe, pawepo na cost sharing katika huduma za elimu, mashule, watu wajiajiri, waanzishe makampuni, viwanda serikali ijitoe katika kufanya biashara, ibaki kukusanya kodi, etc.
Baada ya hapo ukafuata mpango wa kufufua uchumi National Economy Recovering Programme,,
Ambayo mashariti ya kufanya biashara yakarahisishwa, mipaka ikafunguliwa,, haikuwa kosa tena kukutwa na sabuni ya Emperial, kwanga wala Rexona,
Mtu yeyote aliruhueiwa kuagiza vyombo vya usafiri, Tv, etc
 
Kosa kubwa tulilofanya kama nchi ni kuzikumbatia sera za kipuuzi na angamivu za SAP hizi ndo zilikua kaburi kwa nchi yetu

Labda tungekomaa na ule ujamaa wa nyerere bila kupinda popote labda leo tungekua tumepiga hatua

Wenzetu China walikomaa na ujamaa na walivyopata matokeo na kufikia mahali pazuri sasa wakaruhusu ubepari sisi tulianguka mapema sana

Sasa hivi hata hatujui tupo kwenye dira gani nashindwa kujua mwelekeo wa nchi yetu kiuchumi ni aibu sana hadi leo tunategemea misaada

Sera za kishenzi za SAP ndo zimetufikisha hapa, alaaniwe aliyeasisi SAP huu ulikua ndo mwisho wa uchumi wa nchi yetu

Imagine ndo anakuambia ushushe thamani ya hela yako ambayo ilikua sawa na dola ya marekani leo hii hiyo dola ndo tunatumia kuagiza bidhaa nje yaani wanatupiga mara 2305 kwa dola moja daaah

Hii nchi sijui kama itakaa iendelee
Kama China iliutupa ujamaa ndo ikafanikiwa sisi tungeendeleaje sasa.
Toka lini mswahili ashawahi fanya lenye tija, jiulize kwa nn kandarasi nyingi za ujenzi upewa watu wa nje na sio kumpa mswahili.
 
Huyu mzee ndo maana Mungu kampa uhai mrefu tena namuomba Mola amfikishe miaka 200.Yeye ndo alikuja wakomboa watz na utumwa wa sera za ujamaa zilizowafanya watz wawe mali binafsi ya mtawala kama ilivyo North Korea.Na watz wakaanza angalau kuvaa nguo,kupigia mswaki dawa,kuoga kwa sabuni,kuanza kwenda nchi ya nchi.
 
Kosa kubwa tulilofanya kama nchi ni kuzikumbatia sera za kipuuzi na angamivu za SAP hizi ndo zilikua kaburi kwa nchi yetu

Labda tungekomaa na ule ujamaa wa nyerere bila kupinda popote labda leo tungekua tumepiga hatua

Wenzetu China walikomaa na ujamaa na walivyopata matokeo na kufikia mahali pazuri sasa wakaruhusu ubepari sisi tulianguka mapema sana

Sasa hivi hata hatujui tupo kwenye dira gani nashindwa kujua mwelekeo wa nchi yetu kiuchumi ni aibu sana hadi leo tunategemea misaada

Sera za kishenzi za SAP ndo zimetufikisha hapa, alaaniwe aliyeasisi SAP huu ulikua ndo mwisho wa uchumi wa nchi yetu

Imagine ndo anakuambia ushushe thamani ya hela yako ambayo ilikua sawa na dola ya marekani leo hii hiyo dola ndo tunatumia kuagiza bidhaa nje yaani wanatupiga mara 2305 kwa dola moja daaah

Hii nchi sijui kama itakaa iendelee

China walikuwa wakomunisti wenye mpango kamili wa kujitegemea kwa kazi ngumu na usimamizi madhubuti chini ya state party dictatorship. Viongozi walitumia majeshi ya ulinzi na usalama kuweka nidhamu nchini. Hata mavazi yalikuwa sare nchi nzima. Adhabu kwa wahalifu wa kijinai na kisiasa zilikuwa kali hasa. Pia, walikuwa makini sana kujenga kizazi cha wasomi wa teknolojia na mambo ya ufundi kwa ujumla kwa kuiba na kuiga teknolojia za magharibi na Japan.

Nyerere hakuwa na msimamo kamili wa kisera wala kiitikadi. Aliulizwa na Wachina kama mfumo wake ni socialism au communism ili wamsaidie kuufanikisha. Akakataa akasema ni “ujamaa” na hauna tafsiri. Ni itikadi ya kiafrika. Wakamwambia aelewe tu kuwa akitaka socialism ya kweli (communism) lazima atumie mabavu kudhibiti raia na kusimamia nidhamu ili watekeleze mipango ya kitaifa bila mjadala. Hakukubaliana na hilo. Alikuwa anataka kuongea na kupendwa na wananchi wake na “nchi rafiki” za magharibi hasa za Scandinavia.

Unaweza kuona jinsi Wachina walivyoweza kufanikiwa kujenga taifa makini kisayansi na kiteknolojia lakini kwa jasho na damu. Ukatili mkubwa ulitumika kutumikisha wananchi katika kazi za shurba na kuendeleza waliogundulika kuwa na vipaji mbalimbali: michezo, ufundi, utafiti, teknolojia, propaganda, n.k. Hakukuwa na mchezo. Chini ya Mao Zedong, Wachina waliburuzwa kama punda hadi nchi ikajengeka ingawa walipita vipindi vya dhiki kama njaa. Lakini walijifunza wakaanza kurekebisha sera mwishoni mwa miaka ya 1980s kuruhusu ubepari kidogo.

Huku kwetu, Nyerere aliendelea na itikadi yake ya kidhanifu (idealistic) ya ujamaa ambao ulijaa bla bla nyingi, matumizi makubwa, uzalishaji haba, ufanisi haba, n.k. Nyerere alikuwa genuine kwenye matumizi hasa kwenye kuhudumia wananchi kwenye afya, elimu na huduma nyingine kama maji, umeme, n.k. Lakini hakuwa makini kwenye kusimamia uchumi.

Tatizo likawa kuishiwa pesa na kufilisika kwa mashirika ya umma. Vita ya Kagera nayo ikapigilia msumari wa kufilisika. Misaada ya marafiki haikukidhi. Ikabakia kusaini mkataba na IMF ili kuwezesha Benki ya Dunia na wafadhili/wakopeshaji wengine waingie kuokoa jahazi. Nyerere akaachia ngazi; Mwinyi akakamata usukani na “kuweka dole” kwenye makubaliano na IMF na hatimaye SAP ikachukua hatamu.

KIFUPI, ujamaa wa Nyerere haukuwa makini. Ulikuwa kama mchezo wa kisiasa tu. Ilikuwa lazima ushindwe. Nyerere hakuwa realist. Kina Mtei walipomshauri arekebishe thamani ya shilingi kiuhalisia na kupunguza mashirika ya umma - kupunguza matumizi makubwa ya ruzuku aliwaona vibaraka wa mabeberu. Tungekomaa vipi na ujamaa wa aina hiyo?
 
Ndio maana TAIFA la TANZANIA limekuwa la watu wa ajabu ajabu kuanzia ngazi ya familia hadi huko SERIKALINI kwa SERA ZA UJAMAA ni falsafa za hovyo kabisa huzalisha watu wavivu na kutokuwa na uwezi wa kufikria........anzia kwenye ngazi ya familia mfano, ukiwa na kauwezo kadogo tu basi utabebeshwa RESPONSIBILITY ambazo hazikuhusu kabisa ktk maisha ya kawaida kuanzia wajomba,watoto wa BABA mdogo, wadogo zako sijui nani nani ni ujinga kwenda mbele. ...hizi ni athari za ujamaa huzalisha watu wavivu na tegemezi sababu wanaona ni haki yao kusaidiwa sio kutafuta njia au mbinu za kujikwamua na tatizo ulilo nalo.

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
 
Halafu ukiacha ujamaa tukakimbilia kujiunga na Non Aligned Movement (NAM) ambayo hatukujua maana yake ni nini tumebaki watembeza bakuli kama Malaya tu kisa hatufungamani na upande wowote wakati wenzetu waliingia NAM wakatumia siasa ya kujitegemea wakakuza uchumi wao vizuri kwa kutumia rasilimali zao na wataalamu wao sisi tunabaki na NAM kama mazuzu tu.
Hawa akina NAM si ndio akina Singapore,Malaysia,Indonesia....sasa sisi tulikwama wapi? mbona hawa wako mbali kiuchumi? au tulikuwa tunafuata mkumbo na kwenda kama Mazombi.!
 
Wenzetu China walikomaa na ujamaa na walivyopata matokeo
China walianza fanikiwa baada ya liberalisation not before. Unadhani wangebaki closed economy na kubana watu binafsi kumiliki rasilimali wangefika walipofika?
Imagine ndo anakuambia ushushe thamani ya hela yako
Yes mbona hata hyo China inashusha thamani ya pesa yake ili ipate advantage ya investors ama hujui kushusha thamani ya pesa kunavutia wawekezaji kama uchumi umedorora?
 
Hawa akina NAM si ndio akina Singapore,Malaysia,Indonesia....sasa sisi tulikwama wapi? mbona hawa wako mbali kiuchumi? au tulikuwa tunafuata mkumbo na kwenda kama Mazombi.!
Ni haohao, tulijiunga hatukujua wenzetu walikuwa na malengo gani! Walikomaa na wakapata wawekezaji wakubwa kutoka Korea, China, marekani nk. Leo wameendelea within 35 yrs wapo vizuri sana.

Kuna wakati huwa nataka kumlaumu Nyerere lakini nakuja kujiuliza akina Nani walikuwa wanamsaidia yule mzee ???? Mbona alikuwa na maono mazuri sana na akawasomesha watu bure Ulaya na kila sehemu, hao watu wamemsaidiaje au wamesaidia nini taifa letu?

Kama Nyerere aliwaza kujiunga NAM mbona watu hawakumsaodia kutekeleza malengo makuu ya NAM? kiukweli Leo tungekuwa mbali sana.
 
Ubepari una faida gn? Unaijua modern socialism lakini?
china wana apply mixed economy(which is more capitalist than socialist) wao wenyew ujamaa wao ulifeli na zaid ya watu milion 50 walikufa kwa njaa kutokana na kufeli kwa policy mbovu za kisocialist.alvokufa mao akaja rais mpya ambaye aka-liberalise uchumi (yani akau capitalise) kwanzia miaka ya 70 na kuanzia apo ndo CHINA ikaanza kureally develop.kiufupi socialism ni ABOMINATION SYSTEM ambayo at the end of day inapelekea ku-collapse kwa nchi husika mfano USSR ilicollapse kutokana na weakness kibao associated with the system.infact wat u claim to be modern socialism is 75% capitalism kwa mfano kweny socialism hakutakiwi kuwa na mabilionea ambao wanaonexha presence of income inequality but look at china na urusi wana more billioneaz after USA.na iyo ina prove absence of true socialism.
GENERALLY,nchi yoyote inayoapply true socialism (not like china na urus) itaixhia kucollapse mfano mzuri NORTH KOREA leo wananch wananjaa af kim ana kaz ya kuruxha mabomu angani
 
Back
Top Bottom