Mume Wangu12
Member
- Mar 11, 2022
- 8
- 1
kudosUjamaa ulishindwa na Nyerere mwenyewe alikiri.
Ujamaa wa Nyerere aliutengeneza mwenyewe na hakuambilika juu ya namna ya kuuendesha. Ulikuwa ni Ujamaa wa kutafuta wahanga na watu wa kuwaangushia jumba bovu. Kuanzia Utaifishaji wa Mashirika na viwanda, Uanzishaji wa Vijiji vya Ujamaa, Operesheni maduka nk.
Ujamaa haukuwashirikisha Wadau Bali mtu mmoja au,kikundi cha watu ndiyo waliamua nini kifanyike. Hata pale wananchi walipoungana kuunda ushirika wao wa kijamaa walivurugwa kama ilivyotokea Ruvuma Development Association.
Sera za SAP hazikuwa mbaya na si kwamba ndiyo zimetukwamisha, zile zilikuwa sera za waliozitunga na ambao walitoa fedha. Tungekuwa na Uongozi wenye maono hiyo ingekuwa chachu ya kujikwamua zaidi.