Tungeanzisha special economic zones au export procesaing zones kwenye mikoa ya mipakani -- Kagera, Kigoma, Mbeya na Songwe

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Special economic zone ni eneo ambapo wawekezaji huzalisha kwa gharama nafuu na hupata upendeleo kwenye kuzalisha ili kuvutia uwekezaji.

Sheria za maeneo haya na kodi kwenye maeneo haya huwa tofauti na sehemu zingine. Hata gharama za kuingiza malighafi na mashine huwa chini.

Mara nyingi bidhaa ambazo huzalishwa hapa huwa ni kwaajili ya kuuza nje.

Tanzania tumepakana na nchi nyingi sana. Sasa badala ya nchi hizi kufuata vitu China na Dubai wavipate kwenye maeneo hayo.

Kama uzalishaji haufanyiki basi tuanzishe masoko kwenye haya maeneo kwaajili ya kuexport tu. Mtu wa Zambia, Malawi au Congo akitaka kitu basi akipate soko la Mbeya au Songwe. Gharama ya usafiri tu ndiyo iongezeke. Mtu aone bora kununua Songwe kuliko kwenda China. Kwenye maeneo haya watu wapate dawa, vipuri, nguo, electronic nk

Hivyo hivyo mtu wa Rwanda, Burundi na Congo wapate vitu Kagera na Kigoma.

Tuna advantage kubwa sana ya kijiografia, tuitumie. Au nakosea ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom