Tunduru: Mtatiro awafunda Viongozi kwenye Iftari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,796
11,959
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro, ameendelea kukemea tabia ya viongozi kutotumia dhamana walizonazo kupigania haki za wananchi na badala yake wanageuka kuwa mabosi.

DC Mtatiro ameyaeleza hayo alipokuwa anafuturisha mamia ya wananchi wa Tunduru walioalikwa Ikulu Ndogo mjini Tunduru Jumanne 11 Mei 2021.

Mtatiro ameeleza huchukizwa sana na baadhi ya tabia ya watumishi wa umma kushindwa kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kuanza kuwapiga kalenda bila sababu.

Mtatiro amewakumbusha watumishi wa wilaya yake kuwa, utumishi ni dhamana inayopita haraka, kama siyo kuondolewa, kujiondoa au kustaafu, ziko sababu nyingine nyingi - kwa hiyo amewataka watumishi wote wakipata nafasi na dhamana ya kuwatumikia watanzania, wafanye hivyo kwa nguvu na uwezo wao wote kwa sababu wananchi wana haki ya kuhudumiwa na kutatuliwa matatizo yao kwa wakati.

Idd Mohamed,
Tunduru.
 
Huyu Jamaa kuna mahali nimesikia Malalamiko dhidi yake kuwa amejigeuza Mungu mtu, Wafugaji wanamlalamikia sana kukamata mifugo yao na kuwalazimisha wamkatie fungu kubwa ili awaachie..
 
Duuu! Amakweli ule usemi kwamba ukiuwa na usipate matibabu ya kisaikolojia, lazima utajitaja.
Wabaya Sasa wanajiweka bayana.
Angalia mwonekano wake tu kweny3 video, ni wa jeuri na sio staha.

Anatafuta hurumaaa. Hapana

Anatusanifu waisilaamu huyooo

Tuhuma dhidi yake:-
1.Jamaa alikuwa anakusanya mabango pale viongozi walipotembelea wilaya yake
2. Jamaa aliingiza diri kwenye mbaazi za wakulima ili ajinufaishe
3. Jamaa aliandaa mizani ya kupimia mizigo ya korosho kutoka vyama vya msingi ili apate chake ili awe tajiri
3. Jamaa ilikuwa ukiingia ofisini kwake anakusikiliza wakati anafanya Mambo take na kwa jeuri
4. Amewanyanyasa wananchi waliokuwa wanatoa elimu ya jadi kwa watoto wao na kuzuwia kabisa shughuli hizo
5. Amejiingiza kwenye timu ya mpira na kulazimisha wakulima kukatwa pesa kwa kila kilo ya korosho wanayouuza.
6. Nguvu nyingi, akili kidogo, busara zero.

Huyu nae ni walewale na ni wa kushughulikiwa.
 
Back
Top Bottom