MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 714
- 1,137
Sijui kwanini Ujerumani walijigawia Tanganyika wakati wa kuligawa bara la Afrika. Lakini Wajerumani walikuwa wana akili sana na waliona mbali sana.
Tanzania ni nchi kubwa sana jamani lakini pia ina kila kitu.
Nimepata bahati ya kukaa kwa siku kadhaa katika mji wa Tunduma. Ni mji mkubwa sana kushinda miji mingi sana.
Tunduma ni mji wa harakati nyingi sana kulinganisha na miji mingine. Tunduma kuna hela sana kiasi kwamba karibia mabenki yote yana matawi hapa.
Pamoja na umuhinu wote wa mji wa Tunduma huduma za afya naona kama bado ziko chini ukilinganisha na idadi kubwa ya watu hapa lakini pia na umuhimu wake katika uchumi wa nchi yetu.
Hata kituo cha Polisi naona kama ni kidogo sana kwani hapa ni mpakani na uhalifu huwa ni jambo la kawaida sana.
Mji huu pia haukupangwa vizuri japo unakua kwa kasi ya ajabu. Sijui huwa tunashindwa nini kupanga miji yetu.
Tunduma Tanzania na Nakonde Zambia ni vigumu kutenganisha watu wa pande hizi mbili. Muingiliana usiofuata sheria ni mkubwa sana.
Mzambia kulala Tanzania na kumiliki nyumba Tanzania ni jambo la kawaida sana. Mtanzania pia kulala na kumiliki nyumba Zambia simple sana.
Na ukiwa mgeni huwezi jua kama uko upande mwingine wa nchi.
Kwa mfano ukiwa sehemu moja wanapaita BLACK utajikuta uko nchi nyingine kinachoweza kukushangaza ni vibanda vya simu za MTN ambazo huku Tanzania hatuna mtandao huo.
Magari ya Zambia hujikuta yapo Tanzania bila kutegemea, hivyo hivyo kwa magari ya Tanzania.
Watu wake wanaelewa sana kana kwamba wote ni wa nchi moja.
Hapa kwenye mambo ya usalama sijui inakuaje.
Vijana wa Tunduma wanafanya sana biashara ya fedha. Tunduma ndiko sehemu ya Tanzania ambako vijana wanaujua uchumi kwa vitendo kwa maana Exchange rate za fedha zote uzijuazo ziko vichwani mwao.
Lakini pia Tunduma kama kumeendelea sana kuliko Nakonde japo ni majirani. Population kubwa ya watu na majumba mengi yako Tunduma kuliko Nakonde.
Kuna sehemu wananchi wa pande zote walijenga mpaka mpakani na hivyo ikawa vigumu kujua mipaka ya nchi mbili za Tanzania na Zambia. Naona bomoa bomoa ilipita kidogo uwazi wa mpaka unaonekana kidogo.
Kabla ya bomoa bomoa hiyo Mtanzania aliweza kutumia umeme wa Zambia kama kawaida kana kwamba nae ni Mzambia.
Kuna mambo mengi sana Tunduma ukipata muda Tembelea Tunduma upate kujua mengi kuhusu nchi yako.
Na hapa ndipo ile dhana ya Diplomacy mbaya kati ya nchi majirani huwa zinatengenezwa na viongozi lakini wananchi wala hawana shida hata kidogo wanaishi kana kwamba kahuna mipaka.
TANZANIA THE BLESSED NATION.