Tunduma: Ally Mwafongo na wenzake 57 watimiza siku 143 Gerezani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,586
217,977
FB_IMG_1608300347536.jpg


Aliyekuwa Meya wa Tunduma kupitia Chadema Mh. Ally Mwafongo alikamatwa na Polisi kwa tuhuma za kutengenezwa kiwandani za mauaji kabla ya uchaguzi na kuwekwa selo yeye na viongozi wengine lundo wa Chadema , lengo la unyama huo lilikuwa kumzuia kugombea tena udiwani ili kuirahisishia ccm ushindi .

Mwafongo pamoja na lundo la viongozi wa Chadema leo wanatimiza siku 143 gerezani kwa tuhuma za uongo kwa sababu za kisiasa , kwa vile Mungu si Athumani basi tunaamini Mwafongo na wenzake wataachiwa huru na kila aliyeshiriki kutenda unyama huu wa kishamba atalipwa kwa kiasi kile kile alichotenda .

Leo kuna watu nchi hii wanataka tufanye maridhiano na watu wenye roho za kishetani namna hii , hili jambo haliwezekani hata kwa mtutu wa bunduki .

Mungu ibariki Chadema
 
Unatetea watu wenye tuhuma za mauaji ? CDM mna unafiki na ubinafsi wa hali ya juu. Kaweka na tweet ya Kiingereza Twitter ili mabwana zenu waone mlivyo watupu.
 
Tuliambiwa "uchaguzi umekwisha" x3; Wahusika wajifunze Zbar kuondoa watuhumiwa wa siasa mahabusu kwa afya ya taifa.
 
Back
Top Bottom