Tundu Lisu kweli kiboko amchana Kikwete kuhusu kuingilia Idara ya Takukuru

Hahahahaha! Natazama TBC mwenyewe niko hoi. Yaani mpaka mtangazaji mwenyewe akawa anaogopa kumwachia aongee mara amkatishe kuzungimza na ameona ni noma ile mbaya. Masikini mkurugenzi wa TAKUKURU, hana hamu. Kesi 18 Tanzania nzima? Yaani wagombea uraisi walikuwa zaidi ya 3, wabunge nafasi zaidi ya mia tatu na wagombea zidisha mara 3, nafasi za madiwani elfu moja piga mara 3 na unatuambia mumefanikiwa kufungua kesi 18? Basi Tanzania tumeshinda vita vya rushwa atiii? Mmh! Inatia shaka.

Kwani kesi huwa zinafunguliwa vipi............?
 
tundu lisu anawachana live takukuru, anawaponda ile mbaya. Huyu mkuu mimi namkubari kwa vubaya mno. Bunge zima hakuna kama yeye.

Kawachana kivipi.........hebu tupeni yaliyojiri.............maani hii kwenye koo haipiti...........
 
Tundu Lissu kiboko, kwanza alianza kutoa takwimu jinsi pesa za serikali zinavyogawanywa kiupendeleo akitolea mifano ya Lindi, Singinda sijui na mkoa gani inavyopunjwa kila mwaka. Ilifikia hata wabunge wa Magamba wanaotoka mikoa hiyo wakaanza kumshangilia. Mfano mmoja ninaoukumbuka alitolea mfano mgodi wa Geita Gold Mining (GGM) kwamba ni mgodi wa nne kwa ukubwa Afrika, (kwa kutoa dhahabu) lakini Geita ni mojawapo ya wilaya masikini Tanzania. Yule MB wa Geita CCM ilibidi ainamishe kichwa chini.

Na ndipo zilipobaki dk 5 akaamua kuongelea TAKUKURU akasema bila kumung'unya aki-quote mazungumzo ya Hosea na US ambassador to Tanzania yaliyonaswa na wikileaks kwamba tatizo kubwa la kupambana na rushwa nchini ni JK anawakingia kifua watuhumiwa wakubwa wa ufisadi. Kuna MB mmoja alinguna Lissu akasema anaguna nini huo ndio ukweli.

Baada ya hapo ndiyo akamu chanachana Chenge kwamba mkataba aliongia na BAE haukuwa na masilahi kwa TAIFA according to SFO. Akaomba suala la la rada lijadiliwe bungeni. muhusika ajulikane, anyooshewe kidole, azomewe kabla ya sheria haijachukua mkondo wake.

Believe me wabunge wote wa magamba walikuwa kama wamenyeshewa mvua ya mawe, hakuna aliyezomea wala kuomba mwongozo. Ni ukweli usiopingika kwamba Tundu Lissu ni sawa na wabunge 30 wa CCM nao CCM wanafahamu. Tena sio wale wa viti maalumu maana wa viti maalumu, CCM sijui huwa inawaokota kwenye guest houses maana hao hawasitahili kabisa kulinganishwa na Tundu Lissu hata kwa ujumla wao.

VIVA TUNDU LISSU
 
Lakini sina mkumbuka hata mmoja wao alisema ni afadhali CDM ipate uraisi kuliko Tindu Lisu kuwa mbunge .
 
Nashukuru sana Bwana Tundu lisu kwani hata Geita na Kahama ametusemea Hasa kuhusu migodi mikubwa tuliyonayo lakini tunaongoza kwa umasikini. Sijui ni vipi walimpa kura huyo mbunge wetu maana hajawahi hata kuchangia japo swali la nyongeza. Maana ya vikao vyote vilivyo pita kama vile hana matatizo jimboni kwake.
 
Tundu Lisu mchungu na nchi big up have long life.Hakuna kurudi nyuma baba komaa hadi magamba yawatoke,hiyo ndio kazi tulio kutuma.
 
Safi sana Lissu.............................. Wabunge wa CCM wanatuharibia meza kazi yao kuzipiga kila kukicha kwa kutetea uozo.

Nimewashuhudia wabunge wa ccm, wakichomoka usingizini wakawakuda wenzao wakigonga meza nao wanaanza kugonga meza bila kujua kinachoongelewa. Kama mazezeta vile!
 
JK anaogopa chain ya rushwa ilivyo hadi yeye atshikwa pabaya mwisho wa siku..takukuru inatakiwa kiwe chombo huru ambacho hakiwajibiki kwa yeyote..isipokuwa mahakama tu.
 
Naunga mkono kabisa ili kuwe na usimamizi mzuri wa hichi Chombo PCCB ni vizuri kiwajibike kwa Bunge moja kwa moja ili kiweze kufanya kazi zake kwa wasaa
 
Hata Maralia Sugu aka Tambwe Hiza analijua hili.

loh! kumbe ndo huyo? nina mpango wa kumshtaki kwa kutumia jina la kigosi wkt yeye sio mgosi, hata makamba sio mgosi, wagosi hawafikirii kwa kutumia viungo vingine vya mwili isipokuwa ubongo.
 
Lakini sina mkumbuka hata mmoja wao alisema ni afadhali CDM ipate uraisi kuliko Tindu Lisu kuwa mbunge .

lissu alitiwa ndani na JK enzi hizo za mikataba ya bullyankhulu (sijui inavyoandikwa) akiwa na cheo cha membe, ulikuwa mkataba wa kifisadi na watu walifukiwa na mwekezaji, baada ya jamaa lissu kulipambanua hilo ndo chuki za msela zikaanza, hapo ungetegemea akubali huyu jamaa afike bungeni?
ila nina imani angetaka asifike wala lissu asingefika mjengoni japo ongembidi atumie nguvu kubwa sana.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom