Tundu Lisu azuiwa kufanya mkutano chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lisu azuiwa kufanya mkutano chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kada Deya, Feb 29, 2012.

 1. K

  Kada Deya Senior Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Waziri kivuli wa sheria na katiba Mh.Tundu lisu leo saa kumi kamili jioni amezuilgwa kufanya mkutano katika chuo kikuu cha mtakatifu agustino Mwanza. Anayedaiwa kutengeneza zengwe la zuwio hilo bila sababu za msingi ni mkuu wa idara ya sheria chuoni hapa anayefahamika kwa jina la Kirangi ambaye anadaiwa kuwa kada wa CCM.
  Mkutano huu ulitarajiwa kufanyika leo baada ya kupata baraka za makamu mkuu wa chuo hapo jana, hadi sasa umma wa wanafunzi unatawanywa kwa nguvu ili kuzuwia mkutano wa mwanasiasa huyo.
   
 2. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siku zote tunasema ila hatusikilizwi ila ukweli ni kuwa amani ya nchi yetu itavurugwa na ccm wenyewe. Kwanini mtu olofata taratibu azuiwe kufanya mkutano? Kwanini wanafunzi wanyimwe haki yao kikatiba ya kupewa taharifa mbalimbali za nchi yao ikiwemo uelewa wa katiba iliyopo? TUTASHINDA MUNGU YU NASI.
   
 3. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  endeni nje ya chuo si lazima kufanyia hapo........
   
 4. M

  Mchakatoh JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani ni lazima afanyie mkutano uwanja wa Laila Odinga?..nendeni nyamalango bana uwanja wa kutosha achana na kibaraka wa magamba!
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,088
  Trophy Points: 280
  Ni bora kumwacha Lissu akahutubia kuliko ukamzuie kwani madhara yake ni makubwa zaidi ya kumwacha na watawala wanaweza kuona wameweza kumbe ndo wamehamusha hasira zaidi
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo kwenye red ni Kilangi, na huenda alikuwa analinda kibarua chake, kwani serikali ilishatoa circular katika vyuo Binafsi na vya UMMA ikikataza masuala ya siasa vyuoni.
  Mimi nashindwa kuelewa kwa mtu makini kama TL kukatazwa kufanya mkutano kwenye viwanja vya chuo, kunakuwa vipi ni kikwazo wakati kuna maeneo ya wazi hapo jirani!.
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  CCM imefika mahali inakimbia kivuli, kutokana na maovu na kashfa waliyo nayo, na namna siri zinavovuja kwa kasi toka ikulu na kwenye taasisi nyingi za serikali na chama tawala, basi kila wakisikia mtu machachari na makini kama lissu anataka kuhutubia hofu ni kuwa analipua bomu lipi??kumbe walitakiwa wamwache atoe aliyo nayo kama yana majibu ajibiwe, ila hofu nyingine mengi hayana majibu!! kazi ipo, hadi tufike 2015!!! "mtu mwoga akisikia unyasi unatikisika anahisi nyoka"
   
 8. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CCM wanachofanya ni kuichelewesha tu haki kwani ni lazima itapatikana tu...Mkumbusheni pia Lissu afanye mkutano mwingine maeneo ya Kirumba.
   
 9. D

  DOMA JF-Expert Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ndio maana wanasemaga wanasheria wa agu ni vilaza muondoeni huyo jamaa
   
 10. ikuo

  ikuo Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Huyo mkuu wa chuo tena ni mnyaturu mwenzie hapo ndo utakapo choka.
   
 11. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sasa unyaturu wa Mkuu wa chuo na hilo zuio vinahusiana nini, acha mambo ya ukabila hapa watu wanajadili haki iliyozuiwa bila kujali dini, rangi, kabila ya aliyezuia na aliyezuia! Ungeleta maana kama ungesema " tena huyo mkuu wa chuo ni chadema mwenzio"! Afterall si mkuu wa chuo alimruhusu!
   
Loading...