Tundu Lisu amtaka Spika Ndugai aache Unafiki kwa lengo la kutaka kuonekana mwema machoni mwa jamii

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amemshukia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kumtaka kuacha unafiki kuhusu futari yake aliyoandaa na kususiwa na wabunge wa upinzani.

Lissu amesema kuwa hawezi kushiriki kwenye futari ya Spika Ndugai au kiongozi yeyote wa CCM kwa sababu wameamua kuwabagua na kuwadhalilisha.

Maneno hayo ya Lissu yamekuja ikiwa ni siku chache tangu Spika Ndugai alipoeleza kuhusu madai ya upinzani kupanga kususia futari yake aliyoandaa Jumanne wiki hii na kusema kuwa jambo hilo si zuri kwani kuna umuhimu wa jamii kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao.

Ndugai alielezea pia wabunge wa upinzani walisusia futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisema kuwa inapofika hatua ya kutoshirikiana katika masuala ya kijamii inakuwa sio vizuri sana.

Lissu alisema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwadhalilisha na kutoa adhabu za vifungo vya nje ya bunge huku akiwazuia kutoa mawazo mbadala ndani ya bunge.

"Kiongozi anayewabagua namna hii bungeni, unawezaje kwenda kwenye futari au shughuli yake? Aache unafiki kwa lengo la kutaka kuonekana mwema machoni mwa jamii".

Aidha, Lissu alienda mbali na kusema kuwa Ndugai amebinafsisha shughuli za bunge kwa serikali na kwamba kwa sasa anafanyakazi kwa kushirikiana na serikali badala ya bunge kubaki lifanye shughuli za kibunge.

Chanzo: Swahilitimes
 
Hii ni ngumu sana kuungwa mkono muda wa kuwa hayuko pamoja nao kule mjengoni. Ajitathimini upya
 
Lissu umeongea kweli kabisa,kwa Haya yanaondelea dhidi ya upinzani kama kung'oa bango,kuzuiwa vikao vya kitaifa mfano meya wa Moshi,kesi za kizushi hakuna maana yoyote kujumuika na ccm
 
Huyo mzee Ndugai ameishiwa Sera kabisa.
Yaani anajifanya hayaoni ayafanyayo,alafu awabembeleze watu kwa ftari. Hizo ni dharau kabisa.
Hiyo Pesa yake ya ftari kosa aipeleke hata kwenye vituo vya kulelea watoto.
Tanzania Yangu bhaana.
 
Hivi Lisu ana xheo gani CDM? Ni mwenyekiti, katibu au msemaji wa chama? Maana mi mgeni hapa mjini
 
Back
Top Bottom