Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,739
Lissu alaani agizo la Magufuli kwa wakuu wa mikoa ya kukamata watu ovyo.
Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu, ametoa maoni yake kuhusu kauli ya Rais Magufuli ya kuwaagiza wakuu wa mikoa kawakamata vijana wanaocheza pool muda wa kazi.
Mwanasiasa huyo maarufu, alisema ni wazi kuwa agizo la Rais Magufuli linataka kuchochea matumizi mabaya ya madaraka kwa wakuu wa mikoa na wilaya nchini.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambayo ndio inasimamia agizo hilo, inawapa mamlaka ya kipolisi wakuu wa mikoa na wilaya kukamata watu wanaovunja sheria pale ambako hakuna polisi.
Alisema sheria hiyo pia inaeleza kuwa mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 na aliyemkamata anapaswa kuandika maelezo ya sababu za kumkamata.
“Sifahamu kama maelekezo hayo wamepatiwa au wameelekezwa tu wakamate wanaovunja sheria? Lakini pia wafahamu sheria hii inaruhusu kiongozi huyu kumkamata mtu kama hakuna polisi na kama wapo, sheria hii haimruhusu kufanya hivyo.
"Siku hizi kila tukio mkuu wa wilaya anaongozana na OCD (mkuu wa polisi wa wilaya), je ni wakati gani atakamata watu kama si kutaka kuvunja sheria?” alihoji.
Lissu alieleza agizo hilo ni wazi litasababisha wakuu hao wa mikoa na wilaya kukamata hata wasio na hatia.
“Wameelezwa tu kuwa wakamate watu wawaweke polisi, lakini hawajapewa maelezo ya sheria hii inayowasimamia, hivyo ni hatari kwa jamii, matokeo yake ni muendelezo wa matukio kama kukamatwa kwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,” alisema.
Source:Nipashe
***
Binafsi nashangaa na ulevi huu wa Madaraka magufuli anajua vijana hatuna kazi na wanaotegemea kilimo ni cha msimu kutegemea na mvua sasa tunaitwa wazururaji...angeanza kufungua viwanda, kilimo kitunufaishe wakulima, aache kuwapa vikongwe uRC wakati vijana na magamba yetu yanachakaa tu...