Tundu Lissu, wewe unakula posho Ulaya unataka Tanzania wasipewe misaada kutoka Ulaya

Watanzania watawaliwa kila tukipata chama shindani na CCM ni wajibu wetu kukiimarisha kwa faida yetu. Watawala wanafurahi na wanatelax kama hakua chama imara cha upinzani.
NCCR MAGEUZI ilipoanza kuibuka watanzania tukarubuniwa tukaiacha ikapotea. CUF vile vile.

Sasa hivi CHADEMAkimeanza kuwa chama makini shindani sasa hivi tunaruhusu kinapotezwa mbele ya macho yetu. Watawala wanafurahia hawatadumbuliwa.

Nchi na wananchi watafaidi kama tututakuwa na vyama mbadala imara haijalishi majina ya vyama.

Bunge letu sasa hivi ni kamalachama kimoja. Hoja za watawala zinateleza tu hakuna wa kuhoji.

Tozo zinapitishwa bungeni sasa huku mitaani baadhi ya wabunge nao wanashangaa.

Bunge lachama kimoja nimaumivu kwanchi na watawaliwa na ni furaha watawala!!Watanzania tuamke kwa umoja wetu tutengeneza vyama wakau giwili vyenye nguvu na uwezo wa kuongoza nchi.

Haijalishi chama gani kiwe madarakani iwe CCM, CHADEMA, ATC au chenginecho, uimara wa chama mbadala ni muhimu sana.

Ushabiki wa kisiasa unaofanana na wa Simba na Yanga utatuchelewesha sana!!
 
TULIPIGANIA uhuru ili tuweze kujitawala na kufanya maamuzi yetu binafsi kama taifa bila kuingiliwa.
Kama ni matatizo ya kisiasa tunapaswa kuyamaliza sisi wenyewe sio mambo ya kaka nipigie.
Marekani hakuna udhalimu, dhulma, uvunjifu wa Haki? Nani anawawekea vikwazo vya kiuchumi?
Mkuu sisi ni matajiri hata wakituwekea vikwazo hatutishiki!
 
Tunasikitika sana; Chama na kiongozi anayetegemea siku moja watanzania wampigie kura awe Rais wa nchi hii kuomba tuwekewe vikwazo vya kiuchumi, yaani wananchi tuumie kisa wanasiasa?
Tunaona hali halisi ya Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi vilimuumiza Mugabe au kikundi chake?

Hivyo vikwazo vilikula mpaka kwa Mugabe. Rejea nini kilimtoa madarakani, jitahidi kutafuta mifano itakayobeba hii propaganda yako mfu.
 
Mpumbavu ni nani?

Ni Mtanzania anayeshangilia Tundu Lissu aliyepo nje ya nchi anakula posho wazngu Ulaya halafu huyo anataka Tanzania wasipewe misaada kutoka Ulaya. Anaomba jumuiya ya kimataifa na nchi wafadhili waiwekee Tanzania vikwazo vya kiuchumi na kuzuia misaada.

Lissu angekuwa wa maana angekuja Kuishi Tanzania kisha toa haya matamko yako upo Ulaya na familia yako unataka Watanzamia tupate vikwazo.

Msamehe bure. Labda amehamisha kijiji chao kizima Ulaya. Ndio wasomi na wapinzani hao.
 
Hii awamu naona team Mohamed Said imejipanga kumshambulia Mbowe kila siku. Wee mzima mzima hovyo, ni lini utaacha udini? Unafanya mambo ya kitoto kabisa kwa kutumia ID bandia ili tu uishambulie Chadema.Unafiri tumesahau siku ile ulivyojichanganya na kupost majibizano ya Mohamed Said kwa kutumia hii ID ya Ritz?
Yaani kupingana na Lissu Tanzania kuwekewa vikazwo ni udini?
 
Lissu anajua vema kuwa licha ya yeye kuzunguka Ulaya na Marekani kuomba wahisani wamuwekee vikwazo JPM hakuna kilichotokea. Kama balozi za wahisani wetu wakubwa usembassytz, UKinTanzania, EUinTZ na CanadaTanzania hawajatamka lolote kuhusu Mbowe, hivyo vikwazo vitatoka wapi.
 
Zidisha kuishambulia Chadema. Pengine serikali itasikia kilio chako iandike upya historia ya TANU na Uhuru wa Tanganyika kama unavyotaka wewe. Maana kila siku huishi kulalama kuwa uhuru uliletwa na wazee wa kiislam lakini sasa wakiristo ndiyo wanakula nchi kwenye mfumo Kristo!
Mkuu umekunywa viroba? Mbona sikuelewi unaandika nini.
 
..tunaweza kuwekewa vikwazo kutokana na UDHALIMU unaofanywa na CCM.

..kwa hiyo wanaotuweka ktk risk ya kuwekewa vikwazo ni CCM na hila zao za kukandamiza wananchi.
Hii strategy imepitwa na wakati, nchi ikiwekewa vikwazo rais haumii wala kiongozi yeyote hawi maskini bali atakayeumia ni mwananchi wa kawaida sasa Lissu yupo tayari sisi tuumie ilihali wanasema nia yao ni kututea.
 
..tuishinikize serikali isifanye udhalimu ambao utapelekea Tanzania iwekewe vikwazo.

..vikwazo hutokana na matendo ya kidhalimu ya watawala, na sio makelele ya vyama vya upinzani.
 
..tuishinikize serikali isifanye udhalimu ambao utapelekea Tanzania iwekewe vikwazo.

..vikwazo hutokana na matendo ya kidhalimu ya watawala, na sio makelele ya vyama vya upinzani.
Watanzania wameshindwa kuandama kwenye tozo waje kuandama kumtetea Lissu?
 
Watanzania wameshindwa kuandama kwenye tozo waje kuandama kumtetea Lissu?

..wapinzani hawana uwezo wa kujitetea, lakini hiyo isiwe sababu ya CCM kuwadhulumu kila kukicha.

..CCM wamekuwa kama watu wanaofurahia kutesa ndugu zao, badala ya kutawala kwa haki na kuleta furaha kwa wananchi wote.
 
Lissu anajua vema kuwa licha ya yeye kuzunguka Ulaya na Marekani kuomba wahisani wamuwekee vikwazo JPM hakuna kilichotokea. Kama balozi za wahisani wetu wakubwa usembassytz, UKinTanzania, EUinTZ na CanadaTanzania hawajatamka lolote kuhusu Mbowe, hivyo vikwazo vitatoka wapi.
Kama hamna kilichotokea mbona unalialia?!
 
Bwana mdogo hujui ishu ya Mugabe na wazungu hususan waingereza, ni suala la Ardhi aliyoitwaa kwa mujibu wa mkataba wa Lancaster
Hivyo vikwazo vilikula mpaka kwa Mugabe. Rejea nini kilimtoa madarakani, jitahidi kutafuta mifano itakayobeba hii propaganda yako mfu.
 
Huwezi kutaka nchi yako iwekewe vikwazo wakati una ndugu , wazazi na wale ambao unategemea wakupe kura uwaongoze leo unataka wapate shida wewe hufai hata kukuishi maana damu ya watu itakulilia sana , wewe unashiba na kusaza unataka watanzania wateseke na ulaaniwe.
 
Mpumbavu ni nani?

Ni Mtanzania anayeshangilia Tundu Lissu aliyepo nje ya nchi anakula posho wazngu Ulaya halafu huyo anataka Tanzania wasipewe misaada kutoka Ulaya. Anaomba jumuiya ya kimataifa na nchi wafadhili waiwekee Tanzania vikwazo vya kiuchumi na kuzuia misaada.

Lissu angekuwa wa maana angekuja Kuishi Tanzania kisha toa haya matamko yako upo Ulaya na familia yako unataka Watanzamia tupate vikwazo.

Kwanini na wewe usiende kula hizo posho?
 
Back
Top Bottom