Tundu Lissu: Wanaosema turudi kwenye mfumo wa chama kimoja hawajui walisemalo, Mungu awasamehe bure

Wewe ndio huna habari wewe, hizo kazi alizifanya akiwa mbunge, haya tuambia values za kuongoza watu jimboni kwako ni zipi? Wewe ukiwa mbunge wa kinond
Neno langu la leo, watu wengi sana wana hofu kuhusu mwisho, wanachukua muda mrefu sana, wanapata mawazo wakifikiria mwisho wa siku itakuwaje? mwisho wangu ukoje? nitapona kweli huu ugonjwa, nitamaliza kweli hii shule, nitakaa kweli kwenye hichi cheo, nitajenga kweli hii nyumba, nitaolewa kweli na huyu bwana, nitalipa kweli haya madeni, nitafika salama kweli? ni kawaida kuwa na hofu, lakini kuna vitu vilivyo ndani ya uwezo wako na vingine viko nje ya uwezo wako, fanya kilicho ndani ya uwezo wako vilivyo nje ya uwezo wako mwachie Mungu, huwezi kujua mwisho wako, badala ya kuishi mbeleni, ishi na ulichonacho sasa, ufurahie maisha yako
Nakutakia asubuhi njema
oni taa za barabarani ukaweke Tandahimba?
Unasoma unachokiandika unaweka taa za barabarani sehemu ambazo hakuna msongamano wa magari?
 
Lakini mbona kama kuna mismatch hapa? Watanzania hawajali hayo yote uliyoyasema na ndiyo maana kwenye uchaguzi mdogo CCM imepata Kata 19 kati ya 20 tena Kata moja CCM imechukua KLM ambako ni ngome ya chadema!

Hivyo kwa mtu mwenye akili alipaswa leo hii awekeze muda kujiuliza kwa nini na kulifanyia kazi kwani hizi Siasa zenu Watanzania wamezikataa ndo maana yake lkn kwa kuwa Tundu Lisu ni zero brain anaendeleza Siasa zile zile za siku zote kwa matokeo yale yale kama siyo mabaya zaidi!
Kama Watanzania wangejali huo mnaouita udikteta wangemkataa Mwenyekiti wa CCM pmj na Chama anachokiongoza, lkn matokeo yake Watanzania wameikataa chadema na Viongozi wake less intelligent kama Tundu Lisu!
Ulicho jibu ni tofauti na mada iliyopo mezani kweli wewe umedumaa kiakili sababu ya ukada,.
 
Hii style ya kumtongoza mwanamke kwa kumkandia mume wake huwa haina ushawishi.

CHADEMA badilikeni mfanye siasa safi. Waambieni wananchi wakiwachagua mtawafanyia nini.

Nyie kila siku Rais kafanya hivi mara kafanya vile. Propaganda na siasa za chuki hazitawasaidia. Wananchi wa siku hizi wana akili.
Toeni Uhuru wa vyama vya Upinzani kadiri ya Haki yao iliyoelekezwa kwenye Katiba.Na Pili kukosolewa mtakosolewa tu hakuna njia nyingine.
 
wapinzani wabadilike siasa za chuki zimepitwa na wakati, mm sioni kama raisi kujenga uwanja chato ni kosa kwasababu huko nako ni tanzania nako wanahaki ya kuw na miundo mbinu mizuri ukizingatia geita ni mkoa mpya.
Kwa nchi yetu value for money ni muhimu.Huwezi kuweka asset mahali.ambapo hakuna uwezo wa kupata faida au mapato kulingana na uwekezaji.

Kuna maeneo mengi International airport ingeweza kujenga kama Dodoma au kumaliza ya Mwanza na Mbeya.

Chuki.na Ubaguzi anao Mwenyekiti wa CCM
 
Kwa hoja kama hizi bado naona upinzani wanajidharilisha. Hivi hizo taa za barabarani kama zingefungwa ngalenaro angelalamika au kisa ni kwa sababu kule ni kwao. Kwaiyo Rais akifanya kitu mkoa aliotoka ni hatia?kwani watu wa chato Rais wao ni nani? Na mbona hakutoa takwimu za mikoa mingine kimejengwa nini au ndo anataka kutuaminisha kuwa Mkuu kajenga chato tu?
Tunataka wapinzani mfanye mambo ya maana yatakayotuliea hamasa ya kubadilisha utawala na sio kuleta hoja zisizo na mashiko. Kwa namna hii mnazidi kuwachanganya hata na wale walioakuwa tayari kuwaunga mkono.
Kuna haja gani ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato? Wakati Songwe airport haina taa za kuongozea ndege ili ziwe zinatua all the time? Hilo la mpwa wake kumpa ukatibu Mkuu wizara ya fedha ni hatari sana.
 
Kwa hoja kama hizi bado naona upinzani wanajidharilisha. Hivi hizo taa za barabarani kama zingefungwa ngalenaro angelalamika au kisa ni kwa sababu kule ni kwao. Kwaiyo Rais akifanya kitu mkoa aliotoka ni hatia?kwani watu wa chato Rais wao ni nani? Na mbona hakutoa takwimu za mikoa mingine kimejengwa nini au ndo anataka kutuaminisha kuwa Mkuu kajenga chato tu?
Tunataka wapinzani mfanye mambo ya maana yatakayotuliea hamasa ya kubadilisha utawala na sio kuleta hoja zisizo na mashiko. Kwa namna hii mnazidi kuwachanganya hata na wale walioakuwa tayari kuwaunga mkono.
Unaongea ujinga, kama watakata tamaa kwa ajili ya kuongelea hujuma, waende zao tu.
 
Siamini kama haya maneno yanaweza kusemwa na Tundu lissu, mkuu ww ni mtu una ufahamu mkubwa wa masuala mengi sana kuna mambo mengine kama hayo uliyoyataja hapo hayana msaada wa moja kwa moja kwa wananchi wa chini kabisa, kuna mambo mengine huwa yapo tu mfano hata Trump juzi kamteua mkwe wake kuwa senior advisor wa white house, marafiki zake na hata wafanyabiashara wenzake kibao amewaingiza kwenye serikali yake kwa maslahi ya serikali atakayoiongoza, sasa kwa mtu kama ww siku zote ulitakiwa kifikisha ujumbe kwa wapiga kula wa chini na kueleza mikakati yako na chama chako ili wawape nafasi ya kuongoza lkn habari ya kumsema Rais wananchi hawaelewi kabisa wanachukulia kama ni chuki mliyo nayo kwa Rais na mnachokitaka ni madaraka tu, kwa sababu watu wanaona Rais anafanya ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na wapinzani ikiwemo ww kwa miaka mingi sana. Kwa maoni yangu ebu jikite ktk kujenga hoja ss wananchi tutaelewa tu lkn siyo kumsema mtu tunaona kama ni chuki tu
Akili yako ndogo sana, kuteuliwa kuwa senior ikulu ni cheo cha usimamizi tu, usifananishe na kuwa Katibu wa hazina acha upunguani.
 
Hii style ya kumtongoza mwanamke kwa kumkandia mume wake huwa haina ushawishi.

CHADEMA badilikeni mfanye siasa safi. Waambieni wananchi wakiwachagua mtawafanyia nini.

Nyie kila siku Rais kafanya hivi mara kafanya vile. Propaganda na siasa za chuki hazitawasaidia. Wananchi wa siku hizi wana akili.
Sumu kazi yake ni kuua. Povu tupu, ukiweka promises bila kumkosoa mtawala aliyepo kwa miaka hii mi 5 turudi tu nyuma! Shame on you!
Kwanini usionyeshe mfano wewe na familia yako?
 
Hatuwezi kuwa na akiri mfu kama hizi!!! Na watanzania tusipokuwa makini kelele za wanaharakati zitatuchelewesha tu!!!
-Ulitaka chato lini wapate mafanikio hayo ya kuwa na taa barabarani???,ulitaka hadhi ya chato kuwa na uwanja wa ndege iwe lini???
Mbona tunafikiri kama wafu?? Nchi hii n yetu sote na maendeleo ya kuinua uchumi wetu yanahitajika kila mahala bhana!!! Sehemu zote zinahitaji taa za barabarani na viwanja vya ndege n.k.

Mwajiri huajili watumishi wenye sifa anazozitaka!!! Hao ndg zake unataka wapate uongozi Kenya??? Kama wana elimu inayokidhi nyadhifa hizo kwann wasipewe nafasi hizo??? Jiulize maswali mengi kabla ya kuhoji ndg!!! Nchi hii ina Makatibu wangapi mpaka uhoji huyo mmoja tu???
-Nchi hii ina ma Das wangapi mpaka uhoji huyo ndg mmoja??
-Jiulize nafasi hizi za uongozi ziko ngapi kitaifa ndio uhoji uozo unaotaka watu waunge mkono.

Kampuni lenye sifa na vigezo ndilo litapata fursa popote pale!!! Acha siasa za udaku bro panapo hoja ya msingi tuseme si kutuletea vioja humu.
Umetumwa wewe, kama hujaona hoja hapo pole sana, lakini baadae utakuja kukiri.
 
Kuna haja gani ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato? Wakati Songwe airport haina taa za kuongozea ndege ili ziwe zinatua all the time? Hilo la mpwa wake kumpa ukatibu Mkuu wizara ya fedha ni hatari sana.
Kwaiyo wewe ungekuwa Rais kama kuna mtu ambaye ni ndugu yako na ni mtendaji mzuri wa kazi huta mteua kisa ni ndugu yako, je tangu huyo mtu ateuliwe kuna kashfa yoyote inayomkabili?, Tatizo ni kutafuta mtu mwaminifu au tatizo ni ndugu? Je huyu mtu wasifu wake ukoje je hana elimu na uwezo juu ya kazi aliyo teuliwa kwaiyo? Hebu nijibu kwanza nikuelewe ila Tafadhali jibu hoja.
 
upo sahihi saana mkuu,,, kinachoniuma zaidi ni pale ambapo tunapoaminishwa kua tuna taasisi ya usalama wa taifa yenye jicho la tatu, nashindwa kuelewa wakati wanafanya mchakato wa jumteua mgombea urais je walizingatia maadili pamoja na weledi na busara za wahusika? je walifuatilia historia binafsi za wahusika kuanzia unasaba pamoja na upeo wa akili wa waty husika?

je jopo la wana ccm nguli hasa wale wazee wa chama walifanya maamuzi ya kuwapitisha watu wale na kuwapeleka katika mkutano mkuu kupigiwa kura kwa kuzingatia vigezo gani?

ninachokiona hapo kulikua na mchezo mchafu na ubabe uliotumika ili waweze kukinusuru chama chao na hali hili hiyo ilipelekea kufunika kombe.............apite.

wakuu kuna kila haja ya kuambiana ukweli na kuelimishana kuhusiana na mambo haya ambayo ni muhimu kuyajua kwa mustakabali mzima wa nchi yetu pamoja na vizazi vyetu.

Tanzania niinayo sasa ni ya ajabu saana, naiona nchi iliovurugwa na kuvurugika na ya watu waliokata tamaa, naiona nchi ya watu wasiokua na uzalendo wala mapenzi ya dhati ya kua tayari hata kufa kwajili ya nchi yao, naiona nchi ya watu waliogawanyika na wanaochukiana kutokana na itikadi za vyama na maelekezo kutoka kwa wanasiasa.

nilitaraji kuona taasisi ya urais yenye kuhubiri uzalendo, demokrasia na umoja wa kitaifa kwa maneno na vitendo, nilitaraji kumpata Rais ambae atakua mstari wa mbele kuboresha maisha ya wananchi na kuja na ubunifu wa kuwainua wajasiriamali na wafanya biashara ili kuweza kuza sekta binafsi na kuwafanya watu kua na furaha na kujivunia kua watanzania.

nahisi kwa hali ilivyo sasa ni rahisi sana kwa baadhi ya tanzania kutoa siri nyeti na kuuza utu na maslahi ya taifa letu kwa maadui zetu.

ikumbukwe kua tuna maadui wengi wametuzunguka hasa majirani zetu kutokana na wivu walionao dhidi ya rasilimali zetu pamoja na amani iliotukuka kwa miaka mingi...

natumia nafasi hii kuwaonya watawala na vyombo vyao vya dola kua hii nchi sio yao peke yao ni yetu sote na tumeirithi toka kwa mababu zetu na pia sisi na vizazi vyetu tuna haki ya kuishi kwa raha mustarehe huku tukifanya shughuli zetu, wao sio wakwanza kutawala na kamwe hawatokua wa mwisho watakufa na sote tutakufa lakini Tanzania mama yetu itaendelea kuwepo.

asanteni sana nawasilisha.
Samahani mkuu, kwani wakati Ukawa wanampitisha Lowassa je walitumia busara katika uamuzi ule? Je walifuatilia CV zake kwa umakini? Ama ni maamuzi tu ya wachache na nguvu kubwa ilitumika kumpitisha Lowassa? Hebu nambie kuhusu hili nalo
 
Nimempa mfano wa trump, jamaa kateua hadi mtu aliyeoa mtoto wake(mkwe) kuwa senior advisor wa ikulu, pia marafiki zake na wafanyabiashara wenzake kawapa nafasi ktkt serikali aliyoiunda na wala hakuna kelele yoyote ni kwa sababu watu wanachoangalia ni uwezo wa mtu. Labda niulize hivi kumbe mtu ukiwa Rais unafukuza ndugu zako wote uliowakuta kwenye utumishi wa umma ?

..mpaka mTz umeyajua hayo ni kwasababu wako watu wamepiga kelele kupinga ukiukwaji wa maadili ktk teuzi hizo.
 
Samahani mkuu, kwani wakati Ukawa wanampitisha Lowassa je walitumia busara katika uamuzi ule? Je walifuatilia CV zake kwa umakini? Ama ni maamuzi tu ya wachache na nguvu kubwa ilitumika kumpitisha Lowassa? Hebu nambie kuhusu hili nalo

Mkuu nadhani sote tunatambua kua ccm ni chama dola na chama tawala, ccm ndio chama kinachoongoza serikali well fine labda tukubaliane kwa uamuzi wao wa kumpiga china lowasa na membe je huyu waliotupatia walimuandaa? kwa kutumia vyombo vyao walifanya utafiti wa kina na kujua Nchi itabaki katika mikono salama au walifanya hivyo ili kuzuia mafuriko?
sijawaongelea ukawa kwakua hata kakma wali au wangeshinda kwa jinsi ccm ilivyojipenyeza kwenye vyombo vyote vya dola wasinge na hawajapewa dola. swali linabaki pale pale vyombo vya ulinzi na usalama vilitekeleza wajibu wao katika kuwachunguza wote waliokua wanagombea nafasi ya juu kabisa ya kuongoza nchi?
 
Hivi uwepo wa ofisi za TRA mahala unamaana gani? Unajengaje ofisi za TRA mahali ambapo hakuna mapato ili iweje? Hivi hata mtu ambae hajasoma anaweza kutambua kua hoja kama hii ni propaganda tu. Mi kulekijijini kwetu wasingependa ofisi ya TRA ijengwe kwani wanaona kua TRA ni wasumbufu katika kudai kodi.
 
..mpaka mTz umeyajua hayo ni kwasababu wako watu wamepiga kelele kupinga ukiukwaji wa maadili ktk teuzi hizo.
Je CDM hakuna ukikwaji wa maadili katika teuzi mbalimbali? Mi naona katika suala la uteuzi vyama vyote nchi vinatatizo hilo. Hata vitapo shika dola vitafanya hayohayo. Hebu leteni hoja za kimaendeleo acheni siasa majitaka.
 
Back
Top Bottom