Tundu Lissu: Wanaomsingizia Mbowe kwa ufujaji wa pesa za chama wapuuzwe kabisa - Ripoti za CAG miaka yote ni uthibitisho tosha

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Haya yamesemwa na Mh Tundu Lissu akionyesha kukerwa na baadhi ya watu (wengi wao wakiwa ni wale waliobebwa na kulelewa na Chadema hadi wakajulikana na kuinuliwa) kumsingizia mwenyekiti Mbowe ufujaji wa fedha za ruzuku zinatolewa na serekali kwa Chadema kwa mujibu wa sheria. Na wote hao wamekuwa wakitoa accusations hizi kila wanapokuwa wanaondoka chamani.

Mh Lissu anazidi kushangazwa na hao watu ni kwa nini iwe Mh Mbowe tu na si watendaji wakuu wa chama?

Pia anaendelea kuchagiza kuwa kwa vile ruzuku toka serekalini ni fedha za umma, CAG hufanya ukaguzi wake mara kwa mara kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa.

Sasa miaka yote hii CAG amekuwa akifanya ukaguzi na kutoa ripoti zake, mbona hakuna hata moja inayomu incriminate Mh Mbowe personally? Anazidi kuuliza Mh Lissu.

Hata mimi hapa mwalimu M-Mbabe nabaki kushangaa... kwa jinsi awamu ya 5 ilivyokuwa obsessed na kukandamiza watu wanaoipinga, nina uhakika kwa 100% Mh Mbowe angekuwa yupo lupango Segerea tangu November 2015 hata kama angekuwa amekwapua jero tu!

Taarifa nzima ya Mh Lissu hii hapa....

==================================
Hili la CHADEMA na tuhuma dhidi ya Mwenyekiti Mbowe jibu lake hili hapa:

Haya malalamiko sio ya jana na sio ya juzi; na sio ya mwaka jana wala mwaka juzi. Tangu nimeingia CHADEMA mwaka 2004, kila kiongozi ambaye ameondoka CHADEMA na kujiunga na CCM amehalalisha kuondoka kwake kwa kutoa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za chama.

Sio Lijualikali na Silinde na Mwambe wa leo tu. Kila kiongozi - kuanzia marehemu Amani Walid Kabourou na Chacha Wangwe na kuendelea - amelalamikia matumizi mabaya ya fedha za chama pale anapoondoka kwenye Chama. Na mgomvi wao wa miaka yote ni Mwenyekiti Mbowe, sio Dr Slaa au Dr Mashinji waliokuwa Makatibu Wakuu wa Chama wa hivi karibuni.

Cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuthibitisha madai yao haya. Ajabu nyingine ni kwamba wanatoa tuhuma wakati wa kuondoka kwenye Chama tu. Wakati wakiwa ndani hakuna shida.

Fedha za chama cha siasa ni fedha za umma; ndio maana hukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kila mwaka. Ndio maana hukaguliwa pia na wahasibu huru na mahesabu hayo hupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ukaguzi zaidi.

Ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha hizo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Mwenye kutenda makosa hayo alipaswa na anapaswa kuchukuliwa hatua za kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Sasa kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu na Msajili wa Vyama vya Siasa na wahasibu wa kujitegemea hawajawahi kuona huo ubadhirifu au matumizi mabaya fedha, hawa wanaolalamikia jambo hili, hasa wanapoelezea sababu za kuondoka kwenye Chama na kujiunga na CCM wanawezaje kuwa taken seriously???

Kwa nini hamuwaulizi hata uthibitisho wa tuhuma hizo, kama sio kujaribu kuficha sababu halisi za kukimbia kwao kwenye Chama???

Kwa jinsi ambavyo mamlaka za Serikali ya Magufuli na ya Kikwete kabla yake ambavyo zimekuwa zinatuchukia, kama kweli kungekuwa na ubadhirifu tunaotukanwa nao miaka yote hii, tungeshafungwa wote zamani. Huyu Mbowe si angeshaozea gerezani???

Badala yake, tumekuwa Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yetu licha ya matusi yote haya na licha ya uonevu mkubwa ambao tumeendelea kufanyiwa. Tunasonga mbele.

Kuhusu Wabunge kuchangishwa michango mbali mbali. Tofauti na CCM ambayo huchotewa pesa za serikali na za wafanya biashara wanaohitaji tender au leseni mbali mbali, CHADEMA imejengwa kwa michango ya wanachama, hasa Wabunge.

Wabunge wa CHADEMA miaka yote wamechangia fedha, magari na muda wao kwa ajili ya shughuli za Chama. Ndio maana tumeweza kupata Wabunge, madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa wengi. Hawa akina Lijualikali na wenzake wanaolalamika sasa hivi, walipatikana kutokana na michango ya Wabunge waliokuwapo kabla yao.

Nimemsikia akidai kwamba alichangiwa na wananchi wake tu. Ni mwongo. Mimi mwenyewe nimemchangia kwa fedha, mali na muda wangu. Nimekwenda kumfanyia kampeni za uchaguzi wa Diwani wa Kata ya Ifakara mwaka '13 kwa gharama zangu mwenyewe.

Nimemsaidia kesi ya Ubunge wakati hawa maswahiba zake wa sasa walipojaribu kumvua Ubunge wake kihuni. Nimemsikia akilia Bungeni kwamba alifungwa jela miezi sita kwa uonevu kwa ajili ya CHADEMA.

Hakusema ukweli wote. Hakusema nani aliyemhangaikia Mahakama Kuu kwenye rufaa mpaka akatoka gerezani. Mimi sio tu nilimtetea mahakamani; nilienda kumwona gerezani Ukonga na kumfariji. Baba yake mzazi ni shahidi yangu.

Hakusema kama alisaidiwa na chama au na sisi wanachama wenzake. Hawezi kusema amewahi kutulipa au kuwalipa hao waliomsaidia kiasi gani cha pesa. Hakusema na hatasema kwa sababu anajua jinsi ambavyo Chama chake na wanachama wenzake walivyombeba.

Sasa amepanda bei anaomba CCM wampe kazi. Wale wale waliomfunga na kumnyanyasa na kumdhalilisha mara nyingi, sasa ndio maswahiba zake. Sisi tuliomsaidia kwenye shida yake hatuna maana tena. Hamna shida. Tunasonga mbele.

Nilichokisema kuhusu Lijualikali linawahusu Wills Lwakatare na Cecil Mwambe na David Silinde. Wamebebwa na chama na viongozi na wanachama. Sasa Chama hakiwababaishi tena.

Siwezi kuwaambia wakumbuke walikotoka, maana hawatakumbuka. Nawasihi wajiulize walikoishia waunga juhudi za Rais wengine wote wa miaka ya nyuma.
 
Hata huyo Lissu anayo mengi tu ila kwa kuwa sasa hivi anatumikia cheo cha fadhila cha kupomoroshewa risasi anajifanya ni mtetezi wa fisadi wakati wake ukifika nae pia ataongea kama hawa!
 
Muda Ni Rafiki mzuri siku zote

Tuombe uzima tu tutashuhudia mengi sana.

M .

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Magigazi,

Chama cha siasa ili kiweze kuimarika kinahitaji watu, tena watu walio imara. Na watu hawa utengenezwa kutokana na matunda ya chama chenyewe. Kazi, juhudi na maarifa ndio mwongozo wa uimarishaji wa chama cha siasa. Ni wazi sasa baada ya kufanya utafiti wa zaidi ya miaka mingi wa katiba ipi inafaa kuwa katiba bora ya wananchi na ni ipi inaweza kuwa Itikadi yenye kuishi ndani ya watu, na sasa chama kimepata mwarobaini wake. Katiba ya CCM ndio inayobeba Itikadi ya UTU ambayo misingi yake ni ya kujenga usawa kwa watu wote, udugu, maadili, haki, Imani, mabadiliko, wajibu, asili pamoja na kazi kwa wananchi wote.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Kiongozi yoyote wa chama cha siasa ni lazima awe tayari kukubali kukosolewa pale anapokuwa na mapungufu na awe tayari kujirekebisha, kitu ambacho CHADEMA hakipo na ni makosa makubwa kumkosoa kiongozi, utaitwa msaliti au unatumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
 
CHADEMA iliyokuwa inapinga kauli mbiu ya zidumu fikra za Mwenyekiti sasa imetengeneza miungu watu wake, na kwamba yeyote anayehoji mienendo ya Mwenyekiti hushambuliwa na kutengwa kama alivyofanya Lisu kwa Lijualikali.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Mwanasheria msomi hajui kazi za CAG wala maauditor! CAG anakagua samples tu kwenye lundo la mafile.
CHADEMA mnatakiwa mfanye special audit kwa ajili ya kuaudit tuhuma hizo tu ndio tutajua ukweli. Sio kazi ya CAG kukamata wezi labda iwe negligence sana.
 
Kapewa Umakamu mwenyekiti bila jasho atasema nini kwa mtu anayemgusa aliyempa hiko cheo, atampigia hata deki kama wafanyavyo wafuasi wao.
 
Back
Top Bottom