Tundu Lissu: Waliofaulu kidato cha nne 2011 ni asilimia 9.98

Wazazi wengine hatusomi alama za nyakati. Mtoto hafanyi vizuri tangu akiwa form 1 unajipa matumaini kwamba ataimprove, form two mambo yaleyale, bado unasubiria improvement (bila kufanya chochote) - form 3 hivyohivyo. Je kuna chochote kitarajiwe form 4?

Serikali nayo ni hovyo pia. Watoto wanahitimu std 7 bila kujua kusoma na kuandika, lakini tunaambiwa wamefaulu.Wanamaliza form 1 bila walimu, vitabu, madawati wala maabara, hatushtuki. Ingawa mtihani wa form 2 hauzuii kwenda form 3, lakini upo. Hivyo hali mbaya kielimu inaonekana. Sasa tutarajie nini form 4 kama taifa? Nadhani ni mass failure kama ilivyo sasa.

Nilimshauri mzazi mmoja ambaye mtoto wake yuko form 2 shule ya kata amhamishie private school, akasema kwa vile mtoto hasikii 'ana kibri' anasubiri amalize form 4 afeli ili 'apate fundisho'. Anasahau kuwa fundisho la kufeli ni kwa mzazi pia.

Kagera kuna msemo kuwa 'enyampisa ekiniga ______'
 
Kama ni vijana hawasomi, basi sisi wazazi na walezi ndio wenye shida! Ili kuwaje sisi tujione kuwa tulikuwa tunasoma (kwa mujibu wa andishi lako) lakini wanetu hawasomi? Mimi naamini tofauti na unavyoamini. Kuna tatizo tena kubwa tu. Miaka ya 1990 kurudi nyuma, shule walizosoma watoto wa viongozi ndiko waliikosoma watoto wa walalahoi, leo je? Ni Tanzania hii hii.

Kulikuwa na vyuo vingi na shule nyingi za kati, leo vingi vimegeuzwa vyuo vikuu sio? Tabaka la kati la watenda kazi watafundishwa wapi? Sio ajabu miaka 5 ijayo mainjinia wakawa ndio hao hao "fore men" na "washika mwiko vile. Tafakari!

Tanzania uifaidi, uwe mwanasiasa mtawala!


Mkuu kama umesoma hiyo post vizuri nimesema pamoja na matatizo mengine. Wazazi tuna nafasi kubwa sana ya kwanza kuwafanya hawa vijana kujua kuwa hatma ya maisha yao ipo mikononi mwao. Kuna katabia kameibuka hawa vijana muda mwingi ni wa kucheza na simu, mitandao, na mengine mengi ambayo sio ya kishule. Mkuu usije ukafikiri kuwa wanaofaulu kwenye maseminari ni watoto tofauti au walimu wao ni tofauti sana. La hasha, ni nidhamu tu. Bila mtoto kujua kuwa kazi yake kuu ni kusoma hakuna kitu hapo. Nakubaliana na wewe kuwa kuna shida ya kimfumo japo naamini kuwa uzembe wa wanafunzi ni mkubwa zaidi
 
jifunze vizuri kuesabu hizo point hyo ni div 3 point 25.
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.
 
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.

we na kumbe kilaza sasa c-3 na d- 6 ni four hiyo ndo ninyi tunaowazungumzia kilazestttttttttt...siyo kila kitu uchangie tu hata kama hauna point za kuchangia shame on you
 
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.

Mr. Mzumbe, nadhani unatambua kuwa ili uweze kufanya mtihani wa kidato cha sita ni lazima uwe na credit 3 angalau. Hivyo analysis yako ungetueleza kuwa wale watu wenye Div 4 ya C3 wanaweza fanya mtihani wa kidato cha sita, ila inategemea pia ufaulu wa masomo. Kama ni Science, halafu akawa na F ya Hisabati hawezi chaguliwa huyo. Na hata uchukue masomo 12, yatakayo hesabiwa pointi za daraja lako ni masomo 7 tu. Ila kiukweli, ufaulu hauridhishi . Hii analysis yako ni sawa na tunalinganisha mgonjwa wa kawaida na yule ambaye yupo mahututi, halafu tukubaliane yule mgonjwa wa kawaida eti ana afya njema.
 
naona tumejipatia wabunge wa kutosha mwaka huu,ukichukulia kwamba mbunge anaweza kuwa drs la saba
 
"Maana halisi ya mtu aliyefaulu ni yule aliyepata daraja la kwanza mpaka la tatu, chini ya hapo amefeli. Kwa maana hii basi waliofaulu katika mtihani
wa kidato cha nne mwaka 2011 ni asilimia 9.98 pekee.

Wanafunzi 10 kati ya 100! Hao ndio waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza mpaka la tatu. Vijana wetu hawajifunzi tena. Hawa asilimia 90 wanaelekea wapi?"

Nawasilisha

kwa hiyo ufaulu umezidi kushuka kulinganisha na mwaka jana kwasababu 2010 wanafunzi waliofaulu division 1 mpaka 3 ilikua asilimia 11.
 
We unafikiri wanafunzi wote wanasoma kombi mchanganyiko(art+sayansi) kwa pamoja?

Wengi wanasoma masomo 7 kwa mtiani wa form 4.
Sasa sijajua unataka kuzungumza nini.

Labda alitaka kusema C3 na zingine zote F, ambayo inakuwa ni four ya 29 lakini je hali hii inaweza kujitokeza? Awe amechagua combination tangu akiwa form one?
 
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.

Wewe ndio mwanaasha? naona unajitengenezea mazingira...................
 
Labda alitaka kusema C3 na zingine zote F, ambayo inakuwa ni four ya 29 lakini je hali hii inaweza kujitokeza? Awe amechagua combination tangu akiwa form one?

Form two ndo wanachagua kombi,soon after intering form3.

But hasara ya masomo7 zani ukipata f somo1 inakuwa ni tatizo
 
Hili swala la kufeli inabidi Serikali yetu ilichukulie kwa uzito mkubwa na si kutuletea propaganda kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia mbili (2) siku hizi watu wengi sana wanaweza waka access matokeo na kujionea wenyewe na kwangu ninaweza kusome kwa miaka miwili mfululizo tumeshuhudia wanafunzi wa kifeli kwa kiwango kikubwa sana na hatuna haja ya kufunika funika hilo kwa takwimu. Sababu zipo nyingi sana na baadhi ni hivi;

(i) Shule nyingi sana na hasa hizi za kata hakuna vitabu, na vitabu vichache vinavyopatikana ni hivyo vya Nyangiwe aabavyo ubora wake ni wakutiliwa shaka. Wanafunzi muda mwengi wamekuwa wakipoteza kujadili mitihani iliyopita, kwa kuomba na kusali ili baadhi ya maswali yarudiwe iwe pona yao...Hili tatizo la past papers hata Mwl. Nyerere aliliona na katika paper yake ya Education For Self Reliance aliliongelea na kulipinga kwa nguvu zote, kwa sabubu hazimjengei uwezo mwanafunzi...
(ii) Walimu, walimu wengi hasa wa shule za Sekondari wamepoteza hamasa za kufundisha sababu kubwa ni kama zifuatazo;
  • wamekuwa wakipewa maslai duni na baadhi hata yaho duni hawayapati (kuna baadhi wanadiriki kusema wanafundisha kutokana na wanacholipwa...why should they bother)
  • mazingira ya kufanyia kazi ni duni mno, mfano ukosefu wa nyumba za walimu, zana za kufundisha na kujifunzia
  • Kila Serikali inapo badilisha mitaala walimu wanakuwa hawapelekwi semina ili kuendana na mabadiliko na kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakifundisha kwa kutumia uzoefu tu na si uhalisia wa mtaala unavyo mtaka.

(iii) wanafunzi; ukiwaweka katika mizani wanafunzi wazama hizi na wale wa zamani, hawa wa sasa wanavitu vingi sana vya kuwafanya washindwe au wafauli vizuri sana and therefore kwa wanafunzi wetu wa sasa wanatakiwa wawe na nidhamu kubwa sana karibu ya kila kitu wanachokifanya..Mfano, wakati sasa si jambo la ajabu kumkuta mwanafunzi ana laptop, ipad, galaxytab,au hata smart phone ambavyo vitu hivyo vinaweza kumpeleka na kumsogeza karibu sana na dunia ya maarifa, ila bila nidhamu, vitu hivyo hivyo vitamvuta kuelekea kwenye dunia ya anasa na ngono, na badala ajikite kutafuta maarifa kupitia google na site nyingine za kimaarifa atajikita kutafuta ma-boyfriends na ma-girl friends kupitia, hi5, twitter, facebook na mitandao mengine ya hivyo. Wakati sasa maarifa yameshushwa mikononi mwao ila imeambatana na distractors nyingi kiasi cha kumfanya awe makini sana kuchagua afanye nini na wakati gani..
(iv) wazazi; wazazi wamekua too soft now days na kuwaachia watoto wao uhuru mkubwa sana, mfano ni aghalabu kumwona mzazi sasa akimwambia au akimzuia mtoto kuacha kuangalia tv ili akafanye homework, wazazi wengi siku hizi hawafuatilii maendeleo ya kielimu na kinidhamu ya watoto wao....
 
Ni kweli!
Halafu ndio unakuta wanahangaika kutafuta vyuo vya ualimu ili wakafundishe watoto wetu!...kipofu anamuongoza kiwete!...huh!

No wonder watu wanaquestion mfumo wetu wa elimu..

elimu ya o' level inapasa kumuandaa mwanafunzi,tayari kwa kujiendeleza kwa masomo ya A' level,lakini pia,hata kwa stadi mbalimbali za kazi,hivyo hiyo 90% haitakuwa tatizo la kulijadili tena...
 
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.

Cheti hakitolewi kwa aliyepata div iv ndiyo taratibu na sheria. Wewe wa wapi? Hwapati vyeti hawajasoma waliopata div iv. Wakienda chuo bado walifeli tu, lakini pia unaibua mkanganyiko wa kweli ya mifumo ya elimu isiyo tafsirika.
 
Tatizo wanasoma maswali na majibu ya Nyambale Nyangwine wa CCM badala ya kusoma vitabu wapate uelewa wa kupambana na changamoto za kidunia. Mtu aliyesomea mtihani kwa miaka mi4 akifeli ujue kwishnei, either aolewe au ataishia kuwa kibaka tu. Kawambwa anaangalia tu... Au kwa kuwa Mwanaasha naye ana 4 then tubadili standards na 4 iwe ufaulu kumfuata FIRST STUDENT
Tuna tatizo kubwa kwenye elimu yetu, siasa ni maisha lakini 'kusiasisha elimu' ni kosa kubwa sana ambalo linatugahrimu na litatugahrimu bilivyo muda si mrefu. Haieleweki asilimia 90 iliyofail itaenda wapi (natambua kuwepo kwa asilimia 43 yenye daraja la nne).
Kwenye wino ulokoleza, huyu Mtanzania kwa vijana wasiopenda kusaka maarifa wanamuona kama 'muokozi' wao, kazi zake anazoziandaa na kuziita vitabu havimsaidii mwanafunzi kusoma na kupata maarifa, kifupi ninaweza kusema Nyangwine anawatia uvivu wa kujisomea vijana wa Kitanzania kwa kuandaa vitabu vinavyotapeli elimu na mustakabli wa maisha ya vijana.

Maarifa kama ufaulu ulivyo, umo katika vitabu, kujitambua na kujifunza kupitia mazingira yanayokuzunguka, vitabu vya maswali na majibu vinakaririsha na hili si lengo la elimu kwa ngazi yoyote.

Takwimu za mwaka1999 zinaonesha kuwa takriban vijana laki 9+ wanamaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo huku soko likichukua chini ya laki moja (kumbuka hawa EK hawaisomi tena).

Huku ni kufanya mahaba na hatari, mageti makubwa na fences tunazojenga sasa hazitasaidia
 
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.

Wewe ndiyo mbumbu kabisa. Nani kakuambia c3 na d6 ni division 4. Fanya utafiti kabla hujaanza kudomokaya, digit zako hapo juu zinaonyesha division 3 ya points 24. Nendaga school acha ushoga!
 
"Maana halisi ya mtu aliyefaulu ni yule aliyepata daraja la kwanza mpaka la tatu, chini ya hapo amefeli. Kwa maana hii basi waliofaulu katika mtihani
wa kidato cha nne mwaka 2011 ni asilimia 9.98 pekee.


Wanafunzi 10 kati ya 100! Hao ndio waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza mpaka la tatu. Vijana wetu hawajifunzi tena. Hawa asilimia 90 wanaelekea wapi?"

Nawasilisha
vijana watasoma saa ngapi wakati muda mwingi wanafikiria maandamano tu
 
Back
Top Bottom