Tundu Lissu: Waliofaulu kidato cha nne 2011 ni asilimia 9.98 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu: Waliofaulu kidato cha nne 2011 ni asilimia 9.98

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanakili90, Feb 14, 2012.

 1. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,570
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  "Maana halisi ya mtu aliyefaulu ni yule aliyepata daraja la kwanza mpaka la tatu, chini ya hapo amefeli. Kwa maana hii basi waliofaulu katika mtihani
  wa kidato cha nne mwaka 2011 ni asilimia 9.98 pekee.

  Wanafunzi 10 kati ya 100! Hao ndio waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza mpaka la tatu. Vijana wetu hawajifunzi tena. Hawa asilimia 90 wanaelekea wapi?"

  Nawasilisha
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,233
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ni kweli!
  Halafu ndio unakuta wanahangaika kutafuta vyuo vya ualimu ili wakafundishe watoto wetu!...kipofu anamuongoza kiwete!...huh!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 34,330
  Likes Received: 11,065
  Trophy Points: 280
  90% ni mtego ukija kuteguka hakutakalika hapa nchini
   
 4. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 840
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Jamani pamoja na kwamba kuna matatizo ya kisekta watoto wetu hawasomi. Wameaminishwa/ kujiaminisha kuwa maisha ni rahisi sana. Vijana wanatumia muda wa kusoma vibaya sana. Cha kusikitisha wanapenda sana anasa za muda mfupi. Wamekuwa hedonists (Piga starehe kesho itajipa yenyewe). Hawatafaulu kwa staili hii na wanapaswa walaumiwe. Kwanza wafundishwe kuwa maisha ni magumu then wakitambua hilo watasoma.
   
 5. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,570
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye kiwete kidogo niseme umeandika kikwe...
   
 6. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni bomu hilo likija kulipuka sasa
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,203
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Tatizo wanasoma maswali na majibu ya Nyambale Nyangwine wa CCM badala ya kusoma vitabu wapate uelewa wa kupambana na changamoto za kidunia. Mtu aliyesomea mtihani kwa miaka mi4 akifeli ujue kwishnei, either aolewe au ataishia kuwa kibaka tu. Kawambwa anaangalia tu... Au kwa kuwa Mwanaasha naye ana 4 then tubadili standards na 4 iwe ufaulu kumfuata FIRST STUDENT
   
 8. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 756
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
  Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.
   
 9. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona lissu anaongeza speed ya 2015 kama lowassa vile
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  hili ndio tatizo la wabongo.....mtu anaongea ukweli nyie mnaingiza siasa zenu....phuuum
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kama ni vijana hawasomi, basi sisi wazazi na walezi ndio wenye shida! Ili kuwaje sisi tujione kuwa tulikuwa tunasoma (kwa mujibu wa andishi lako) lakini wanetu hawasomi? Mimi naamini tofauti na unavyoamini. Kuna tatizo tena kubwa tu. Miaka ya 1990 kurudi nyuma, shule walizosoma watoto wa viongozi ndiko waliikosoma watoto wa walalahoi, leo je? Ni Tanzania hii hii.

  Kulikuwa na vyuo vingi na shule nyingi za kati, leo vingi vimegeuzwa vyuo vikuu sio? Tabaka la kati la watenda kazi watafundishwa wapi? Sio ajabu miaka 5 ijayo mainjinia wakawa ndio hao hao "fore men" na "washika mwiko vile. Tafakari!

  Tanzania uifaidi, uwe mwanasiasa mtawala!
   
 12. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,570
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  We unafikiri wanafunzi wote wanasoma kombi mchanganyiko(art+sayansi) kwa pamoja?

  Wengi wanasoma masomo 7 kwa mtiani wa form 4.
  Sasa sijajua unataka kuzungumza nini.
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 19,468
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 180
  hivi wewe unajua unachoongea wewe..C-3 na D-6 ni division 4?? watu wengine bana....
   
 14. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 736
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  jana nilikuwa na waalimu mahali.nikaleta hoja ya matokeo,mmoja akasema hiyo ni trela bado picha,tunataka matokeo yajao pasiwe na one ata moja.tuone sisi na madaktari nani? Nani zaidi.mgomo huu baridi unaua taifa
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,336
  Likes Received: 269
  Trophy Points: 180

  Kwa kweli huu mtindo wa kisasa wa kusoma maswali mimi siuelewi na siuungi mkono. Siamini kama mtu anaweza kupata ulewewa wa kina wa mambo mbalimbali kwa kusoma maswali na majibu ya mitihani. Kwa bahati mbaya siku hizi watoto wa shule wamezoezwa kusoma hivi vijitabu na wanadhani wanaelewa.
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,254
  Likes Received: 4,242
  Trophy Points: 280
  ni kweli div 4 sio ufaulu,
   
 17. m

  msambaru JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 231
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Pa1 na ugamba na ukakasi alionao EL aliwahi kusema vijana wanaomaliza shule na kufeli namna hio ni bomu litalolipuka siku ikifika, mimi nasema litalipuka 2015 na litaangamiza kila aliekuwa kikwazo cha elimu yao kuwa duni na katika mazingira magumu kama yalivyo sasa.
   
 18. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,500
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo walimu(hasa wa cheti), ambao wengi wamepata foo kati ya 26-28 inamaanisha ni felia na kwa hiyo hawapaswi kufundisha?
   
 19. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,570
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Najua unaweza kufikiria zaidi ya hapa.
  Keep on thinking.
   
 20. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,500
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Nina uhakika ni shule hiyo tu ndo haitakuwa na one. Kinachofanya matokeo yawe mabovu ni ****** wa kuondoa mchujo wa mtihani wa fomu twu, mivilaza mingi imekuwa inafika fomu foo wakati zamani ilikuwa inachujwa toka fomu twu. Na hii ndio sababu zero na foo zimeongezeka.
   
Loading...