Tundu Lissu: Wadhamini hawawezi kunirudisha Tanzania, nitarudi nikihakikishiwa usalama wangu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1579686728052.png

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA - Bara, Tundu Lissu amesema anawaonea huruma waliomdhamini katika kesi ya uchochezi inayomkabili, kuiomba mahakama itende haki kwa kuwa hawawezi kumrejesha Tanzania.

Lissu ambaye kwa sasa yupo nchini Ubelgiji anakabiliwa na kesi ya uchochezi katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, juzi Januari 20, 2020 wadhamini wake walitakiwa na mahakama hiyo kuhakikisha anarejea nchini ili kuendelea na kesi yake.

Mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki amesema wadhamini hao, Robert Katula na Ibrahimu Ahmed hawawezi kumrejesha Tanzania kwa kuwa hawakumpekea.

“Mimi nitarejea nitakapohakikishiwa usalama wangu, uhai ni mkubwa kuliko kesi hiyo,” amesema mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki.

Lissu ameeleza hayo jana Jumanne Januari 21, 2020 ikiwa ni siku moja tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa siku 31 kwa wadhamini wake kuhakikisha wanamfikisha mahakamani hapo.

Juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisikilizwa kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alielezwa na wadhamini wa Lissu kuwa wamemuandikia barua mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtaka amrejeshe mshtakiwa huyo nchini.

Lissu yupo Ubelgiji tangu Januari 6, 2018 alikokwenda kwa matibabu akitokea Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako nako alifikishwa usiku wa Septemba 7, 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa katika makazi yake eneo la Area D, Dodoma.

Hakimu Simba alitaka wadhamini hao kuhakikisha Februari 20 wanampeleka mshitakiwa hiyo na si vinginevyo. Kabla ya maagizo hayo Katula alisema juhudi walizofanya kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani ni pamoja na kumwandikia barua Mbowe.

Katika maelezo yake kuhusu wadhamini wake, Lissu amesema, “ninawahurumia sana wadhamini wangu kwa sababu wamewekwa katika mazingira ambayo ni magumu na mabaya bila sababu ya msingi.”

“Mtu anapokuwa mdhamini katika kesi za jinai, anachukua reasonable steps kuhakikisha mtu aliyemdhamini anafika mahakamani wakati anapohitajika kufika mahakamani.”

Ameongeza, “mdhamini sio askari magereza wa kumsimamia mtuhumiwa muda wote na huo siyo udhamini. Kazi ya mdhamini siyo kuhakikisha kwamba huyo aliyedhaminiwa anakuwa naye muda wote bali wajibu wake ni kuhakikisha anafika mahakamani kwa kuchukua reasonable steps.”

“Kwa mfano mtuhumiwa amekimbia au ametoroka, anachotakiwa kufanya mdhamini ni kwenda mahakamani na kusema niliyemdhamini ametoroka na nimemfuatilia na kushindwa kumpata na siwezi kumpata na akifanya hivyo mahakama inamfutia huo udhamini na hiyo ndiyo sheria ya Tanzania.”

Huku akizungumza kwa umakini Lissu amesema, “katika kesi yangu, hakimu anajua na waendesha mashtaka wanajua kuwa niliondoka Tanzania katika mazingira gani, wote wanajua na dunia inajua, katika mazingira hayo hata bila kuambiwa au kuombwa alipaswa awaondoe kwa sababu hawana namna yoyote ya kunirudisha.”

“Sasa mahakama huyu Hakimu Simba anasema wanipeleke mahakamani, hawawezi kunileta na hawawezi tena na wamesema hivyo na Hakimu Simba anachokifanya anacheza ngoma ambayo haipo kisheria.”

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati Januari 12 na 14, 2016 jijini Dar es Salaam ambapo Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’ Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi kweli yule Hakimu Simba akili zake zina akili?

Risasi zaidi ya 30 aliyetoa order zipigwe anajulikana halafu unatoa maagizo ya kiboya hivyo kwamba LISSU ARUDI KUENDELEA NA KESI YAKE afadhari hata angesema Lissu arudi tummalizie maana huko aliko mgambo wetu hawawezi kumdhuru maana hawajui hata lugha
 
Sasa akifutiwa udhamini akirudi si atakaa jela au Hana mpango wakurudi bongo?
Halafu huo ulinzi ahakikishiwe na Nani na atakuaje Kama amehakikishiwa?
NB.zamani bi.mkubwa akitaka kukuchapa halafu ukakimbia utasikia njoo mwanangu mpendwa hata sikuchapi,ukirogwa kwenda tu unachezea kichapo!!
 
Natoa pole za dhati kwa wadhamini kwa sababu mliyemdhamini hadhaminiki.

Lissu àkipitia mitandaoni kusoma "comments" za vijana wa ufipa anaweza kudhani anaweza kushinda urais kama alivyoshinda umakamu akiwa mafichoni
Kama Kuna tume huru ya uchaguzi na akiwa mgombea wa uchaguzi kwa tiketi ya chama tofauti na Chadema. Akiwa Chadema siwezi mpa kura yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadhamini wa Tundu Lissu;

"Tumemwandikia barua, Freeman Mbowe ili amlete mshitakiwa mahakamani",

1. Hivi ktk situation hii, kisheria Freeman Mbowe ana mamlaka na wajibu gani juu ya mshtakiwa huyu ambaye yeye hata hakumdhamini?

2. Taratibu za sheria ya udhamini zinasema nini kwa mshtakiwa wa kosa la jinai ambaye ametoweka ama haonekani wala kufika mahakamani ktk kesi yake?

3. Siyo kwamba, wadhamini wanatoa taarifa mahakamani na wao kuondolewa kwenye udhamini na mshtakiwa automatically kufutiwa dhamana yake na hivyo jukumu la kumkamata tena mshtakiwa linarudi mikononi mwa polisi???

4. Hapa ndipo tusiojua sheria tunajiuliza;

å Kitu gani kinashindikana sheria kufuatwa?

å Kwa nini mahakama inawasumbua wadhamini kwa swala lililo wazi na kueleweka kisheria?

å Mbowe afanye ni nini kisheria dhidi ya Mshtakiwa Tundu Lissu?

å Au Mbowe ni polisi siku hizi?

å Je, tuamini kuwa hawa wadhamini ktk mazingira haya hawajui utaratibu wa kisheria wa kufuata ili kujiondoa kwenye kiapo cha udhamini wa mtuhumiwa Tundu Lissu ambaye kwa namna yoyote ile hawawezi kumpata wala kumleta nchini/mahakamani toka huko aliko?

å Kweli hawana wanasheria wa kuwaelekeza utaratibu wa kujiondoa kwenye tanzi hili au nao wamenunuliwa na kuwa sehemu ya uchafuzi wa mfumo wa sheria zetu?

å Tunajiuliza maswali haya magumu kwa sbb, hizi movement wanazozifanya kwa kushirikiana na mahakama/hakimu Simba, kwa vyovyote hazi - make sense kwa mtu yeyote mwelewa na kutia mashaka tupu dhidi ya NIA ya HAKIMU/JAJI ktk kesi ya ndugu huyu...!!


5. Mimi naona kama vile sasa SIASA inaingia mpaka mahakamani jambo ambalo ni baya na la hatari!!
 
Kazi ya Mahakama ni kutafusiri sheria.Hakimu aangalie sheria inasemaje badala yakuwashughurikia wadhamini wa Lissu.Je sheria inasema hivyo.
 
Mahakama ifute dhamana itume polisi wakamkamate Lissu kama sheria inavyotaka na siyo kuwatisha wadhamini. Huyo hakimu anataka tu kujifanya kichaa!
Wadhamini ndio wanatakiwa kulamatwa kwa kumtoroshea kusikojulikana waliyemdhamini
 
Mh. Tundu Lissu umetoa ufafanuzi mzuri kisheria. Hao wadhamini Mahakama iachane nao na isiwasumbue tena.
 
beth,
Kama hawezi kurudi ilikuwaje akagombea umakamu mwenyekiti wa Chadema?

Na huo urais wanaoshabikia akina mmawia atagombea akiwa uhamishoni?

Ufipa ni bure kabisa!
Yohana Mbatizaji ni hivi, aliyemimina zile risasi 30 mchana mchana yupo, sasa mhakikishieni kwamba hatacharaza zingine tena, maana kuna watu wanajinadi kwamba akija tu this time hawatafanya kosa tena - yaani ni moja tu chali.

sasa kauli kama hizi hata ningekuwa mimi - SIRUDI bila kupewa uhakika wa usalama wangu.
 
Mh. Tundu Lissu umetoa ufafanuzi mzuri kisheria. Hao wadhamini Mahakama iachane nao na isiwasumbue tena.
Mkuu bagamoyo kwanza lazima liwekewe wazi suala la usalama wake Tundu Lissu mwenyewe.......

Haiwezekani mchana kweupe, tena kwenye makazi ya viongozi wa serikali, anamiminiwa risasi zaidi ya 30, halafu Jeshi letu la Polisi, linataka kutuaminisha kuwa watu hao HAWAJULIKANI!

Huyo Hakimu kama kweli anasimamia haki, angehoji kwanza watu waliomshambulia Tundu Lissu, wakamatwe kwanza kabla hajashinikiza Tundu Lissu arejee nchini
 
beth,
Kama hawezi kurudi ilikuwaje akagombea umakamu mwenyekiti wa CHADEMA?

Na huo urais wanaoshabikia akina mmawia atagombea akiwa uhamishoni?

Ufipa ni bure kabisa!
Wewe unawashwa nini? Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA, na hatarudi Tanzania hadi jitu shenz lililotaka Kumuua litoweke Tanzania na Taarifa za uhakika tulizonazo ni kwamba hilo jitu halifiki Oct /2020 likiwa hai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom