kyene kyaka
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 318
- 315
Nimekaa nimefikiria kwa muda mrefu huyu wakili mkongwe anasumbua sana kama hamna mawakili wengine wenye kushindana naye, maana huwa naamin kuwa serikal inaajiri wanasheria au mawakili wenye IQ kubwa sana lakini wakikutana na huyu jamaa wote weupe tu.
Mpaka nimekuja kuandika hii thread hapa ni kutokana kusoma kesi ya jana ya Tundu Lissu pale mahakama ya hakimu mkazi na kupata mawazo ambayo yalinifikirisha yule jamaa anaogopwa.
Mfano 1; Pale Hakimu mkazi mkuu wa Kisutu bwana Thomas Simba kumwambia wakili wa serikali bwana Patrick Mwita kuwa unamuogopa Lissu, hiyo kauli ilitoka baada ya hakimu Thomas Simba kumuhoji sababu za kushindwa kutekeleza amri ya kumkamata Lissu wakati hati ya kumkamata ilitolewa Novemba 3, 2016 na wakili huyo kuisaini.
Kauli ya hakimu mkazi akimuambia wakili Mwita "kwanini hamkumkamata " si mlikuwa na wajibu wa kumkamata? Mnamuogopa?"
Mfano 2; Pale ambapo naye Hakimu mkazi akatoa povu kwa Lissu na kuonekana anajihami kwa wakili mkongwe huyo pindi Lissu alipohojiwa kwanini hakutoa taarifa wakati amesafiri na kwenda kwenye kesi Bunda na kushindwa kuudhuria kesi mara mbili mahakaman na Lisu kutoa kauli kuwa alituma barua ya udhuru kuwa hatokuwepo kupitia kwa wasaidizi wake.
Kujihami kwa hakimu mkazi baada ya kauli ya Lissu "Hakuna barua iliyotufikia. Usituingize katika migogoro kutokana na nafasi yako katika jamii ya mwanasheria. Hatukuogopi labda upande wa mashtaka ndio wamekuogopa.Tunataka kufuata mfumo hatutakuonea, Hapa naona upande wa mashtaka wanapiga blaa blaa, tuelewane tunaichukua hati yako yako ya kusafiria ili ukitaka kusafiri tujue"
.......Kupitia mifano miwili hapo juu nimebaki najiuliza wanachomuogopea Tundu Lissu haswa ni nini?
Kyenekyaka mkighanile une