Tundu Lissu umetusaliti Waafrika wenzio

Dec 13, 2018
30
150
TUNDU LISSU MTUMWA WA WAZUNGU.

Tundu Lissu kwa kuwafanya wazungu kuwa Baba zako na Mama zako, umeusaliti Mkutano Mkuu wa kwanza wa watu Weusi duniani (Pan Africanism Conference) ulioitishwa na Kwame Nkrumah mjini Manchester, mwaka 1945 kuzungumzia Mshikamano wa mtu mweusi.

Tundu Lissu umeusaliti mkutano wa Mataifa yote ya Afrika (All African People's Conference) mjini Accra, wa December 1958,ulioitishwa na Kwame Nkrumah kuzungumzia agenda ya harakati za Uhuru, namna ya kulinda Uhuru unaopatikana kutoka kwa Wazungu na kuupinga ukoloni mamboleo.

Kwame Nkrumah ndiye Afrika na Afrika ndiyo Kwame Nkrumah; Kwa Wakoloni na Mabeberu jina la Kwame Nkrumah ni laana kwao; kwa Masetla na Walowezi jina lake ni onyo kwamba siku zao zinahesabika Afrika na duniani,kwa Waafrika wanaokandamizwa kwa ukoloni na ubeberu wa kimataifa, jina la Kwame Nkrumah na Julius Nyerere ni pumzi ya matumaini kwa Waafrika dhidi ya Wazungu, nyenzo ya uhuru, ushindi, undugu na usawa kwa Waafrika,Jina la Kwame Nkrumah na Julius Nyerere kwa wazungu ni ishara ya kukombolewa kwa mtu mweusi.

Tundu Lissu kwa kuwafanya Wazungu kuwa Baba zako na Mama zako umewasaliti Mashujaa waliopigania Uhuru wa Mwafrika dhidi ya Mzungu ambao waliwapinga wazungu na kuwaondoa kwenye ardhi ya Afrika,Tundu Lissu umemsaliti Martin Luther King, Malcolm X, Master Fard Mohammed,W.E.B Dubois, Kwame Nkrumah,George Padmore,Nelson Mandela, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika); Dakta Hastings Kamuzu Banda (Nyasaland, baadaye kuitwa Malawi); Joshua Nkomo (Southern Rhodesia/Zimbabwe), Dakta Keneth Kaunda (Northern Rhodesia/Zambia) na Patrice Emery Lumumba (Congo Leopoldville/Zaire/DRC).Amilcar Cabral (Portuguese Guinea/Guinea Bissau); Holden Robert (Angola) Edward Mondlane na Samora Machel,Jommo Kenyatta,na Tom Mboya (Kenya) mwakilishi wa Vyama vya Wafanyakazi barani Afrika miaka ya 1958.

Tundu Lissu umewasaliti wanamichezo walioteseka na ubaguzi wa rangi toka kwa wazungu mfano wa Abeid Pele, Mohamed Ali na Brother George Foreman ambao walipata kuwa World heavy weight Champions na wazungu kuwaita Mabingwa wa watu weusi licha ya kuwabonda wazungu kila uchwao na mechi baina yao iliamriwa isichezwe Amerika wala Ulaya ila Zaire na kweli mechi ya Mkanda wa Dunia wa heavy weight kati Mohammed Ali na George Foreman ilichezwa Kinshasa,Zaire(Kongo).

Tundu Lissu umemsaliti Kinjekitile Ngwale aliyekuwa Jemedari wa Vita vya Majimaji,vita hivyo vililenga kumkomboa Mtanzania kutoka mikononi mwa Wajerumani na kuwa si sahihi kuwa vita hiyo ilikuwa na uwezo wa kugeuza risasi kuwa maji bali ililenga kuwapa nguvu wapiganaji ili waweze kujitolea hata ikibidi kupoteza maisha yao ili mradi tu waweze kujikomboa kutoka kwa Mzungu Mjerumani, Watu walikufa kwa faida ya kuikomboa Afrika na tuliokombolewa ni Mimi Msemakweli Chakubanga na Wewe Tundu Lissu, Leo unamsaliti Mkombozi wetu Kinjekitile Ngwale, ni nini kimekukumba ewe Mwanampotevu Tundu Lissu.?

Tundu Lissu kwa kuwafanya wazungu kuwa Baba zako na Mama zako, umemsaliti Chief Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (1855–19 July 1898),Chief Mkwawa ambaye aliwapiga Wazungu na kujinyonga ili wasimuue wao kwa kumdhalilisha, leo hii wewe Tundu Lissu umewachagua Wazungu kuwa Baba zako na Mama zako!?

Kwa kuwafukuzia Wajerumani baada ya vita vya Lugalo, Mkwawa alipompoteza makamu kiongozi wa Kalenga, Ngosi Ngosi Mwamugumba.

Tundu Lissu umewasaliti Chief Rumanyika, Mtemi Isike wa Wanyamwezi, Chifu wa Waluguru, Chifu Songea wa Wangoni, na Mbunga wa Wandebele,Chief wa Waluguru na Chief wa Wamanyema,Kwa machungu makubwa Tundu Lissu umemsaliti Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga Mkwawa kwani ndiye mtu pekee aliyeanzisha umoja ambao leo hii tunajivunia na kama machifu wenzake wangetambua azma hiyo, pengine Wajerumani wangeweza kuondolewa kwa nguvu hata kabla ya jaribio la Vita vya Maji Maji vya mwaka 1905 hadi 1907. Kama mpango wa Chief Mkwawa ungefanikiwa, Wajerumani wangepigwa kuanzia Tabora hadi Songea,na kuweka historia kubwa ya mzungu kupigwa Afrika.

Tundu Lissu kwa kuwafanya wazungu kuwa Baba zako na Mama zako umemsaliti Kwame Nkrumah ambaye alikuwa na sifa zote za usomi hata kuweza kumuoa mwanamke wa kizungu lakini alimwambia Abdul Nasser aliyekuwa Rais wa Misri amtafutie binti wa kiafrika ili aweze kumuoa na Basset akamletea binti kimisri na kumuoa binti huyo wa kiafrika mwenye asili ya kiarabu,ilikuwa ni kujaribu kuimarisha mshikamano wa Kiafrika (Pan-Africanism) kwa kujenga tafsiri mpya kwamba “Mwafrika” maana yake si “Mtu mweusi” pekee, bali ni “mzalendo yeyote mkazi wa Afrika mwenye mapenzi mema kwa Afrika.

Ni ukweli usiopingika, wala si uzushi, kwamba kupinduliwa kwa Kwame Nkrumah pale Ghana ulikuwa ushindi kwa Wazungu hasa ubeberu wa Kimataifa na ukoloni mamboleo Kuanza kutawala katika Afrika. Kuanzia hapo, msukumo wa Afrika kuungana umetoweka, udikteta na uporaji wa rasimali za Afrika umetia fora; Afrika inazidi kudhoofika katika nyanja zote kuliko mwanzo; haina jeshi la pamoja la kujilinda wala kutetea uhuru wake ila kwa “msaada” kutoka nje. Na ndio watu kama Tundu Lissu wanakuwa vibaraka wa wazungu na kufanywa kila kitu na wazungu ili hali wazungu hao wawasaidie kupata madaraka na wapatapo madaraka kuunda Serikali ya nusu mkate na wazungu.

Kwame Nkrumah aliangushwa kwa kuthubutu kuchokoza ubeberu wa Kimataifa na kwa kutaka kuunganisha Afrika na nchi za dunia ya tatu kupambana na ubeberu wa Wazungu.

Ndoto ya Nkrumah ya kuunda Shirikisho la Mataifa ya Afrika (United States of Africa) – “USA” mithili ya USA ya Marekani; kuunda ngome ya Kijeshi Afrika, mithili ya Umoja wa Kujihami Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) na kwa kujaribu kuinasua Afrika kutoka kwenye ushawishi wa Mataifa makubwa (Non-alignment) iliwaumiza sana wazungu ambao leo Tundu Lissu amejitoa kwa wazungu wamtumie kuua ndoto zozote zile za Waafrika kujikomboa na ukoloni mamboleo.

Kwame Nkrumah akichukiwa Sana na Wazungu baada ya kuchapisha kitabu alichokipa jina “Neo-Colonialism: The Highest stage of Imperialism” (Ukoloni Mamboleo: Hatua ya Juu kabisa ya Ubeberu) Oktoba 1965 kushambulia Ubeberu, kitabu iko kiliwatia kichaa wazungu na kiliitia kichaa Marekani hata kufuta msaada wa dola milioni 35 kwa Ghana. Miezi minne baadaye Kwame Nkrumah akapinduliwa kwa msaada wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA).Je Lissu uko tayari kuwekwa kwenye kumbukumbu sawa na Kanali wa Jeshi la Ghana aliyetumiwa na Wazungu kumpindua Kwame Nkrumah, Je Tundu Lissu uko tayari dunia ikuweke kwenye historia sawa na Mongosuthu Buthelezi akiyeipinga ANC na kuungana na Makaburu!?

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kitu ambacho angependa kufanya ni kutumia muda wake wote hata ikiwezekana kujiuzuru urais kuiona Afrika ikiwa huru dhidi ya Wazungu na yenye Umoja. Kwa Mwalimu Nyerere kwake suala la mke, watoto na mambo ya kifamilia kwa ujumla hayakuwa masuala ya Kiserikali bali ya kibinafsi; akisema “ni hatari sana, na kwa kweli ni ubatili mtupu, kwa mke na familia kujiona kuwa sehemu ya utawala na Serikali.Je Tundu Lissu unayo hekima hii au unataka wazungu wakusaidie halafu uifanye Serikali ya nusu mkate, yaani wewe,familia yako na Wazungu waliokusaidia, kamwe hatutakurusu na kamwe husipime maji maana utazama,Nakusihi zingatia malezi ya Mwalimu Julius Nyerere na pengine zingatia malezi ya Edward Sokoine.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
 

bababikko

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,391
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom