Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ulipaswa ugombee tena ubunge, kugombea Urais umepwaya sana

Jibu hoja iliyopo mezani,Lissu anafaa kuwa rais? Na hoja mfu anazozitoa kama kuleta serikali ya majimbo na kuruhusu kuuza mazao nje holela? Sio unaleta pumba.
Ndiyo. Bila kumshabikia, anasema kuwa Rais hatakiwi kuwa na madaraka yote ya kuamua kuhusu maendeleo ya wilaya au jimbo. Akiwa mbaguzi ataumiza wengine. Anasema pia kwamba wakuu wa mikoa, wilaya na ma DED, walio na madaraka makubwa ya kila siku kwa wananchi, wapigiwe kura na wananchi ili wawajibike kwao. Ndiyo maana ya majimbo. Na hajakataza tozo kwa mazao yatakayouzwa nje. Wewe usiingie mkumbo wa kugombana humu. Ulileta hoja humu, shiriki namna hii kuzijadili
 
Hiyo mifano tu,acha ujinga kwani kusambaza umeme vijini? Huoni barabara bado zinajengwa?

Hata mkoloni Alifanya yote hayo,

Miaka 55 ya uhuru unajivunia umeme?

Miaka mitano ya jk ilijenga barabara nyingi kuliko ya magufuli

Lete vitu vya msingi
 
Ukweli ni kwamba..

Lissu kushinda ni ngumu (mfumo sio mzuri) but AMEKUBALIKA SANA kadri siku ZIENDAVYO.

HOJA
Lisu kihoja yupo vizuri

Rais wetu (Magufuli)

kushinda atashinda lakini Lissu kamuonyesha what's to be done for the sake of coming up election (2025).
Lisu kaleta hali ya Kujiamini kwa Watanzania wengi just Imagine NYAMAGANA watu bado wameonyesha UPENDO wa hali ya juu kitu ambacho raisi amekiona kitabadilisha baadhi ya utendaji wake

God Bless TANZANIA
Tumeccm wataiba kura lakini watajifunza kuwa watanzania siyo wajinga wanajua ukweli kuwa CCM ni ile ile ukoo wa panya
 
Hata mkoloni Alifanya yote hayo,

Miaka 55 ya uhuru unajivunia umeme?

Miaka mitano ya jk ilijenga barabara nyingi kuliko ya magufuli

Lete vitu vya msingi
Mtukufu mwenyekiti wa CCM ndani ya miaka mitano katumia pesa nyingi kuminya demokrasia unyanyasaji uonevu kuwabambikia kesi wapinzani badala ya maendeleo.
 
Tumeccm wataiba kura lakini watajifunza kuwa watanzania siyo wajinga wanajua ukweli kuwa CCM ni ile ile ukoo wa panya
Kikubwa ni Mabadiliko yale WAHITAJIO WANANCHI.

Rais wetu alipoingia madarakani nae alileta mabadiliko.

Kwasasa pia kuna mabadiliko atakuja nayo
:):):):):):):)
 
Nitajie mmoja tu ambae unao ushahidi amebambikiwa kisiasa.

Acha hawa wananchi wanyonge amabao hata JPM anajua wanaonewa.
Nikimtaja mmoja utasema, ah! Hawa ni wanyonge wanaoonewa. Hao wanyonge, nani anawaonea? Nani anawabambikia kesi? Si ni system hiyohiyo. Angalia hii enguaengua ya waomba udiwani ubunge. Be true to yourself, halafu chambua nani wameonewa na nani hawakuonewa. System hiyo iliyowabambikia makosa na kuwaengua ni hiyohiyo.
 
Serikali za majimbo zipo America , German, China, South Africa, India sehemu nyingi Duniani hata jirani kenya hutumia Serikali za majimbo hazina ubaya wowote tena huharakisha maendeleo kwa kasi zaidi ya mfumo huu wa kikoloni uliopo sasa
Yaani wewe na mgombea wa kiti cha Urais wa Jammii Forums akili zenu ni zero Devide and Rule ulisoma vzr ebu tuacheni na huu mfumo wetu unaoliunganisha Taifa letu
 
Yaani wewe na mgombea wa kiti cha Urais wa Jammii Forums akili zenu ni zero Devide and Rule ulisoma vzr ebu tuacheni na huu mfumo wetu unaoliunganisha Taifa letu
Wewe ndiyo zero tukuache na nani Taifa lenu lipi? Umeliunganisha nini wakati sasa kuna ushetani wa kupita bila kupingwa na bado tarehe 28 kuna uchakachuaji wizi wa kura ni nini kinawaunganisha hapo?
 
Wewe ndiyo zero tukuache na nani Taifa lenu lipi? Umeliunganisha nini wakati sasa kuna ushetani wa kupita bila kupingwa na bado tarehe 28 kuna uchakachuaji wizi wa kura ni nini kinawaunganisha hapo?
Una uhakika au ulafi wa Madaraka Kama alivyo mgombea wenu
 
Kama kuna kosa la kisiasa ambalo Lissu amelifanya ni kugombea urais mwaka huu,japokuwa ni haki yake ya kikatiba kugombea hiyo nafasi lakini ni kweli kuwa hiyo nafasi tayari inaonyesha amepwaya.

Hoja unazozitoa majukwaani,tayari zinaonyesha kuwa ulikurupuka kuchukua uamuzi wa kugombea urais,au mwenyekiti wa Chadema alikubwagia mzigo mzito uubebe ili hali akijua kuwa huwezi kuubeba.

Umezunguka sehemu mbalimbali na kila unapokuwa majukwaani watu wanakufuatilia,na wanashangazwa kwa nafasi nyeti kama hii ya urais na hoja ambazo umekuwa ukizitoa. Mfano ulikuwa mtwara,ukasema utaruhusu wakulima kuuza korosho nchi yoyote wanayotaka. Yaani wakivusha wakapeleka msumbiji sawa,Comoro sawa, je hujui hapa taifa linapoteza mapato yanayopatikana na Cashewnut export levy? Sasa wewe ni rais gani utayeruhusu serikali yako ikose mapato?

Hii la kuigawa nchi kwenye majimbo je ulipima uzito wake? Na ugumu wake? Mbon unaliropoka kiasi cha kuwakatisha tamaa watanzania! Mbali na hayo umekuwa ukituhumu kuwa miradi mingi inayotekelezwa na Ccm imejaa ufisadi,je hili sisi kama watanzania ambao hatuna uwezo wa kupata ukweli juu ya hizi tuhuma unaweza kuthibitisha vipi? Mfano unasema mradi wa JNHPP unajengwa kwa dola bil 11, tena kwa mkopo wa mabenki ya Misri, unaweza kuthibitisha haya? Hii ni dhahiri uligombea nafasi nzito ambayo haipatikani kwa hoja za kizushi au zisizo na mashiko.

Lakini kama ungerudi kwenye jimbo ambalo ulishinda hapo awali,jimbo la Singida Mashariki, Lissu ulikuwa na uhakika wa kushinda kwa 100%. Na hapa zile kura za huruma toka kwa ndugu,jirani na wazee wa Ikungi ungezipata kwa urahisi mno. Lakini najua chama chako kina kiongozi mnafiki na huyu ndie amekuingiza mkenge ugombee urais huku akijua huwezi kushinda.

Hii kwako ilikuwa nafasi kurudi bungeni na kuendeleza harakati zako za kutetea wananchi. Na nina uhakika safari hii ungerudi bungeni pangewaka moto.
Wewe ni mjinga sana, huna uwezo wa kufikiri japo kidogo. Magufuli hata mwenyekiti wa kijiji hafai...Unyapara wa barabara ulikuwa unampa shida sembuse Ubunge.
 
Huyo mgombea hana visibility, haoneshwi kwenye hizo runinga, ila approval rate yake inaongezeka, fanyeni tafiti, kabla ya kuandika mavitu mengi ya kipuuzi ya kuchosha wasomaji
Sehemu aliko pita Lissu yule mzee wa mboga mboga ile ajaze kama mwanzo itabidi aongeze wasanii na malori ya Kusomba watu
 
Back
Top Bottom