Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Kama kuna kosa la kisiasa ambalo Lissu amelifanya ni kugombea urais mwaka huu,japokuwa ni haki yake ya kikatiba kugombea hiyo nafasi lakini ni kweli kuwa hiyo nafasi tayari inaonyesha amepwaya.
Hoja unazozitoa majukwaani,tayari zinaonyesha kuwa ulikurupuka kuchukua uamuzi wa kugombea urais,au mwenyekiti wa Chadema alikubwagia mzigo mzito uubebe ili hali akijua kuwa huwezi kuubeba.
Umezunguka sehemu mbalimbali na kila unapokuwa majukwaani watu wanakufuatilia,na wanashangazwa kwa nafasi nyeti kama hii ya urais na hoja ambazo umekuwa ukizitoa. Mfano ulikuwa mtwara,ukasema utaruhusu wakulima kuuza korosho nchi yoyote wanayotaka. Yaani wakivusha wakapeleka msumbiji sawa,Comoro sawa, je hujui hapa taifa linapoteza mapato yanayopatikana na Cashewnut export levy? Sasa wewe ni rais gani utayeruhusu serikali yako ikose mapato?
Hii la kuigawa nchi kwenye majimbo je ulipima uzito wake? Na ugumu wake? Mbon unaliropoka kiasi cha kuwakatisha tamaa watanzania! Mbali na hayo umekuwa ukituhumu kuwa miradi mingi inayotekelezwa na CCM imejaa ufisadi,je hili sisi kama watanzania ambao hatuna uwezo wa kupata ukweli juu ya hizi tuhuma unaweza kuthibitisha vipi? Mfano unasema mradi wa JNHPP unajengwa kwa dola bil 11, tena kwa mkopo wa mabenki ya Misri, unaweza kuthibitisha haya? Hii ni dhahiri uligombea nafasi nzito ambayo haipatikani kwa hoja za kizushi au zisizo na mashiko.
Lakini kama ungerudi kwenye jimbo ambalo ulishinda hapo awali,jimbo la Singida Mashariki, Lissu ulikuwa na uhakika wa kushinda kwa 100%. Na hapa zile kura za huruma toka kwa ndugu,jirani na wazee wa Ikungi ungezipata kwa urahisi mno. Lakini najua chama chako kina kiongozi mnafiki na huyu ndie amekuingiza mkenge ugombee urais huku akijua huwezi kushinda.
Hii kwako ilikuwa nafasi kurudi bungeni na kuendeleza harakati zako za kutetea wananchi. Na nina uhakika safari hii ungerudi bungeni pangewaka moto.