Tundu Lissu: UKUTA umedhihirisha CCM sio chama cha siasa

Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,480
2,000
Ukisoma maelezo ya Tundu Lissu na ukisoma maelezo ya Prof.Kitila kwenye gazeti la leo la Mwananchi utagundua a big gap of critical argumentation kati ya hawa wawili. Prof anatakiwa ajifunze historia na kutumia ubunifu kufikia malengo chanya.
Yule ni hajui sana mambo ya siasa..alipopata huo uprofesa ndo kajifanya anajua mambo ya siasa ..nakala zake huwa na malengo maalumu..ni aina ya ma prof kama lipumba
 

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,157
2,000
Ukisoma maelezo ya Tundu Lissu na ukisoma maelezo ya Prof.Kitila kwenye gazeti la leo la Mwananchi utagundua a big gap of critical argumentation kati ya hawa wawili. Prof anatakiwa ajifunze historia na kutumia ubunifu kufikia malengo chanya.
Weee Kitila Mkumbo hasogei hata nusu kwa Tundu Lisu.. When comes to integrating history with current situation and give the meaning, Tundu Lisu ni mashine ingine. sijaona wa kufananishwa naye..
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,420
2,000
Tundu Lissu the Geneous. Huyu mtu alisoma shule za Tanzania Kweli? Mungu amlinde Tundu Lissu ili Taifa liendelee kupata maarifa yake. Huyu ni tofauti na akina Prof. Kitila Mkumbo ambaye ana mawazo ya kusadikika. Eti huu ni wakati wa upinzani kutumia akili na siyo nguvu. Je, kuna akili zaidi ya hii ya akina Lissu? Huyo Mkumbo haelezi ni akili ya aina gani mtu ataitumia ili CCM na Serikali waelewe. Mkumbo tuambie hiyo aina ya akili ambayo unafikiri ikitumiwa na wapinzani itaeleweka au itafanikiwa kwa utawala huu wa hofu na mashaka. Mtu ni kama vile hajiamini kama ana madaraka aliyonayo. Au ni kweli kwamba anajua hakushinda? Kwanini wale vijana wa Chadema walivamiwa wakati wa utangazaji wa matokeo ya urais? Kuna mashaka hapo. Ukiona mwalimu anaingia darasani na kuanza kujihami kwa mikwara ujue hana kitu kichwani huyo.
 

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,874
2,000
Mbona Chadema wanataka kuiingiza CCM kwenye mgogoro wao na Serikali. Lissu anataka kutuambia chadema wakiunda Serikali chama kitakuwa kinalumbana na vyama vinavyoingia mgogoro na serikali?
 

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,874
2,000
Na sisi tukishinda Vita hii dhidi ya Mafisadi basi watoto wetu watakuwa na nchi nzuri yenye haki na yenye maendeleo lkn mpaka siku hiyo ifike ni lazima kuondoa kansa ya Kifisadi inayoiangamiza nchi hii Kansa hiyo ni fisadi lowasa, tundu lisu, Mbowe &Co.!

Pamoja na Pombe Magufuli (PhD) tutayashinda mafisadi na kuyaangamiza kabisa, sisi tuna Dola na Mungu wao mafisadi akina lowasa, tundu wana shetani na dhuluma!
Chadema wanatapatapa, ni UKUTA vs Serikali, wasiingize CCM kwenye mgogoro huo.
 

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,874
2,000
Tundu Lissu the Geneous. Huyu mtu alisoma shule za Tanzania Kweli? Mungu amlinde Tundu Lissu ili Taifa liendelee kupata maarifa yake. Huyu ni tofauti na akina Prof. Kitila Mkumbo ambaye ana mawazo ya kusadikika. Eti huu ni wakati wa upinzani kutumia akili na siyo nguvu. Je, kuna akili zaidi ya hii ya akina Lissu? Huyo Mkumbo haelezi ni akili ya aina gani mtu ataitumia ili CCM na Serikali waelewe. Mkumbo tuambie hiyo aina ya akili ambayo unafikiri ikitumiwa na wapinzani itaeleweka au itafanikiwa kwa utawala huu wa hofu na mashaka. Mtu ni kama vile hajiamini kama ana madaraka aliyonayo. Au ni kweli kwamba anajua hakushinda? Kwanini wale vijana wa Chadema walivamiwa wakati wa utangazaji wa matokeo ya urais? Kuna mashaka hapo. Ukiona mwalimu anaingia darasani na kuanza kujihami kwa mikwara ujue hana kitu kichwani huyo.
Wewe hata hii kauli tu ya lissu unaona kuna hata chembe ya akili?
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,522
2,000
Na bado Askari wetu watawachapa mpka muombe poo!
ukiitwa dikteta utakimbilia mahakamani!jaribu kujenga hoja basi hata kidogo!!!!unaongea kama yusuf mskamba bana!!!!huu mchezo hauhitaji hasira...ukishapiga ukaua unajua kinachotokea?binadamu akishaona maiti zinazagaa huogopa mara ya kwanza,ila akishazoea ni hatari sana...it's like a cat pushef to the corner and behind a closed door,it bound to react...preach peace brethren/sisthren
 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,706
2,000
UKUTA UMEFUNUA SIRI YA TANZANIA - Tundu Lissu

Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba nchi yetu inatawaliwa na chama cha siasa, yaani CCM. Hata hivyo, wapo wachache ambao walishaanza kuhoji kama CCM ni chama cha siasa hata kabla mfumo wa vyama vingi vya siasa kuruhusiwa miaka 25 iliyopita. Ukisoma 'The State and the Working People in Tanzania', kilichohaririwa na Prof. Issa G. Shivji na kuchapishwa mwaka '87, utagundua kwamba tayari kuna wasomi ambao walishaanza kuhoji kama kweli CCM ni chama cha siasa. Chama cha siasa huongoza kwa hoja za kisiasa, sio kwa bunduki, mizinga na mabomu.

Chama cha siasa hushinda mijadala ya kisiasa kwa kutumia ushawishi wa hoja za kisiasa na kiitikadi, sio kwa vitisho vya kuua au kuvunja miguu ya mahasimu wake wa kisiasa. Chama cha siasa huenda kwa wananchi kuwashawishi wakiunge mkono, hakijifichi nyuma ya vyombo vya ukandamizaji vya dola na kuwatisha wananchi. Miaka miwili iliyopita Jakaya Kikwete aliwaambia wanaCCM wenzake waende kwa wananchi wakafanye kazi ya siasa, waache kutegemea kubebwa na Jeshi la Polisi.


Hili limewashinda, bila majeshi na bunduki na mabomu, CCM haiwezi kufanya kazi ya siasa. Bila ma-DC na ma-OCD, CCM haiwezi chochote. Zamani walikuwa wanatuita sisi wapinzani vyama vya msimu vinavyosubiri uchaguzi ndio tufanye kazi ya siasa. Sasa wanatukataza kufanya kazi ya siasa mpaka tusubiri msimu wa uchaguzi. Sasa sisi ndio chama cha siasa, maCCM yamegeuka kuwa chama cha msimu. Wanajifanya walishinda uchaguzi lakini hawadiriki kuturuhusu sisi tulioshindwa kwenda kuongea na wananchi.


Wenye hatia huwa na hofu - the guilty are afraid. Wanatukataza siasa kwa sababu wanajua hawakushinda uchaguzi na wanajua wananchi wengi wanajua hivyo. Na wanajua hawana majibu ya hoja nyingi za kisiasa za utawala huu wa kidikteta. Kwenye 'The State and the Working People in Tanzania' kuna makala inayoitwa 'The State and the Party' ambayo inazungumzia uhusiano kati ya CCM na vyombo vya dola, hasa majeshi. Tangu mwaka '64 lilipoundwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana kati ya chama na vyombo vya ukandamizaji vya dola. Mfano mzuri wa uhusiano huu ni makada wa chama kuingizwa jeshini na kufanywa maafisa wa jeshi, na maafisa wa jeshi kufanywa makada wa chama na kupewa kazi za kisiasa na/au za kiraia. Wafikirie akina Kikwete, Kinana, Makamba, Nsa Kaisi, Kiwelu, Nnauye, Kafanabo, n.k. Orodha ni ndefu sana.

Wakati wa mfumo wa chama kimoja, majeshi yaligeuzwa kuwa Mkoa wa Chama, sawa na mikoa ya kijiografia kama Dar au Singida. Lengo lilikuwa ni ku-integrate zaidi majeshi katika mfumo wa kisiasa na kiraia ili kuulinda mfumo unaotawala. Katika era ya vyama vingi, majeshi yameondolewa katika siasa kikatiba na kinadharia tu. Katika hali halisi, mambo hayajabadilika kwa kiasi chochote cha maana.

Angalia wanajeshi walioko katika nyadhifa za kisiasa za kiraia kama ma-DC, ma-RC na sasa hata maKatibu Wakuu wa wizara. Wote hawa ni maCCM kwa Katiba ya sasa ya CCM. Angalia wanajeshi walioko katika uongozi wa CCM ambao jana tu walikuwa wanakatazwa na Katiba ya nchi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Kwa hiyo, kinachoonekana sasa kwa majeshi kujitokeza hadharani ili kuzuia UKUTA, ni ushahidi wa wazi kwamba CCM haiwezi tena kujenga hoja ya kisiasa kwa wananchi na ikakubaliwa.


Sasa ni wakati wa mabavu ya kijeshi tu. Na wala sio utii wa sheria bila shuruti tena. Kwa vile sheria ya mikutano ya kisiasa na maandamano iko upande wetu, sasa ni wakati wa shuruti ya kijeshi bila sheria. Tukishinda vita hii ya sasa, watesi wetu hawatakuwa ni silaha nyingine yoyote itakayobaki. Tutashinda. Wakati ni UKUTA. Aluta continua!!!!!!
 

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,874
2,000
ukiitwa dikteta utakimbilia mahakamani!jaribu kujenga hoja basi hata kidogo!!!!unaongea kama yusuf mskamba bana!!!!huu mchezo hauhitaji hasira...ukishapiga ukaua unajua kinachotokea?binadamu akishaona maiti zinazagaa huogopa mara ya kwanza,ila akishazoea ni hatari sana...it's like a cat pushef to the corner and behind a closed door,it bound to react...preach peace brethren/sisthren
Nyie lazima mtandikwe tu, hakuna namna
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,622
2,000
Ukisoma maelezo ya Tundu Lissu na ukisoma maelezo ya Prof.Kitila kwenye gazeti la leo la Mwananchi utagundua a big gap of critical argumentation kati ya hawa wawili. Prof anatakiwa ajifunze historia na kutumia ubunifu kufikia malengo chanya.
Kitila namheshimu sana ila kwakweli yuko miongoni mwa Wachumia tumbo waandamizi
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Lowassa is a formidable opponent and skilled in mobilising support unlike the previous predictable opponents which CCM is used to; UKUTA imekuwa well communicated, planned, motivated watu wajitokeze.

Tofauti na serikari wao trick yao ni moja tu vitisho pekee (not bad) lakini hakuna counter arguments kwenye hoja za wapinzani ambazo azisimami zenyewe wao awana muda kuelimisha jamii kuhusu sheria za nchi hakuna kiongozi wa upinzani aliewahi kwenda mahakamani kuthibitisha Tanzania inaongozwa na mtu mmoja aliehozi vyombo vya mahakama na bunge. Ni hadithi tu ambazo watu wamejitungia kwa wananchi ambao ni gullible uthibitisho wake ni matendo mawili matatu ya kupishana mtazamo, media interpretation na kauli za upinzani. Ukijumlisha na hali ya pesa mtaani, tozo za kupata huduma, ubora wake inaweza kuwa rahisi sana agenda ya UKUTA kupata support.

Hizi siasa tuwaachie wazungu tu wanaojua cabinet gani inafaa muda gani; uwezi kuwa na cabinet ya kujaza nafasi tu wakati maamuzi yako yanataka watu wenye werevu wa juu sana kuyatekeleza na kutoa somo kwa raia; as much na support kichapo kijacho lakini raisi inabidi afanye reshuffle ya uongozi wake kajaza watu wengi sana wanaoongeza hasira kwa wanachi na wasio na uwezo wa kuzimudu wizara for god-sake watu awajuhi wanaanzia wapi in trouble shooting logistic za wizara zao.
 

huskryderz

Member
Dec 23, 2011
24
45
Sasa tumeondoa maneno!
 

Attachments

  • UKUTA.jpg
    File size
    34 KB
    Views
    32

SAMTII

Member
Aug 5, 2016
43
95
Kuna udikteta mzuri na wenye tija kama wa Magufuli.
Kuna udikteta mbaya wa kujenga hoja kuharibu udikteta mzuri ili kumchelewesha kiongozi asitimize matakwa ya wananchi ili wapate cha kuzungumza!.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
103,722
2,000
Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba nchi yetu inatawaliwa na chama cha siasa, yaani CCM. Hata hivyo, wapo wachache ambao walishaanza kuhoji kama CCM ni chama cha siasa hata kabla mfumo wa vyama vingi vya siasa kuruhusiwa miaka 25 iliyopita.

Ukisoma 'The State and the Working People in Tanzania', kilichohaririwa na Prof. Issa G. Shivji na kuchapishwa mwaka '87, utagundua kwamba tayari kuna wasomi ambao walishaanza kuhoji kama kweli CCM ni chama cha siasa.

Chama cha siasa huongoza kwa hoja za kisiasa, sio kwa bunduki, mizinga na mabomu. Chama cha siasa hushinda mijadala ya kisiasa kwa kutumia ushawishi wa hoja za kisiasa na kiitikadi, sio kwa vitisho vya kuua au kuvunja miguu ya mahasimu wake wa kisiasa. Chama cha siasa huenda kwa wananchi kuwashawishi wakiunge mkono, hakijifichi nyuma ya vyombo vya ukandamizaji vya dola na kuwatisha wananchi.

Miaka miwili iliyopita Jakaya Kikwete aliwaambia wanaCCM wenzake waende kwa wananchi wakafanye kazi ya siasa, waache kutegemea kubebwa na Jeshi la Polisi. Hili limewashinda, bila majeshi na bunduki na mabomu, CCM haiwezi kufanya kazi ya siasa. Bila ma-DC na ma-OCD, CCM haiwezi chochote. Zamani walikuwa wanatuita sisi wapinzani vyama vya msimu vinavyosubiri uchaguzi ndio tufanye kazi ya siasa. Sasa wanatukataza kufanya kazi ya siasa mpaka tusubiri msimu wa uchaguzi. Sasa sisi ndio chama cha siasa, maCCM yamegeuka kuwa chama cha msimu.

Wanajifanya walishinda uchaguzi lakini hawadiriki kuturuhusu sisi tulioshindwa kwenda kuongea na wananchi. Wenye hatia huwa na hofu - the guilty are afraid. Wanatukataza siasa kwa sababu wanajua hawakushinda uchaguzi na wanajua wananchi wengi wanajua hivyo. Na wanajua hawana majibu ya hoja nyingi za kisiasa za utawala huu wa kidikteta.

Kwenye 'The State and the Working People in Tanzania' kuna makala inayoitwa 'The State and the Party' ambayo inazungumzia uhusiano kati ya CCM na vyombo vya dola, hasa majeshi. Tangu mwaka '64 lilipoundwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana kati ya chama na vyombo vya ukandamizaji vya dola. Mfano mzuri wa uhusiano huu ni makada wa chama kuingizwa jeshini na kufanywa maafisa wa jeshi, na maafisa wa jeshi kufanywa makada wa chama na kupewa kazi za kisiasa na/au za kiraia. Wafikirie akina Kikwete, Kinana, Makamba, Nsa Kaisi, Kiwelu, Nnauye, Kafanabo, n.k. Orodha ni ndefu sana.

Wakati wa mfumo wa chama kimoja, majeshi yaligeuzwa kuwa Mkoa wa Chama, sawa na mikoa ya kijiografia kama Dar au Singida. Lengo lilikuwa ni ku-integrate zaidi majeshi katika mfumo wa kisiasa na kiraia ili kuulinda mfumo unaotawala. Katika era ya vyama vingi, majeshi yameondolewa katika siasa kikatiba na kinadharia tu. Katika hali halisi, mambo hayajabadilika kwa kiasi chochote cha maana. Angalia wanajeshi walioko katika nyadhifa za kisiasa za kiraia kama ma-DC, ma-RC na sasa hata maKatibu Wakuu wa wizara. Wote hawa ni maCCM kwa Katiba ya sasa ya CCM. Angalia wanajeshi walioko katika uongozi wa CCM ambao jana tu walikuwa wanakatazwa na Katiba ya nchi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Kwa hiyo, kinachoonekana sasa kwa majeshi kujitokeza hadharani ili kuzuia UKUTA, ni ushahidi wa wazi kwamba CCM haiwezi tena kujenga hoja ya kisiasa kwa wananchi na ikakubaliwa.

Sasa ni wakati wa mabavu ya kijeshi tu. Na wala sio utii wa sheria bila shuruti tena. Kwa vile sheria ya mikutano ya kisiasa na maandamano iko upande wetu, sasa ni wakati wa shuruti ya kijeshi bila sheria. Tukishinda vita hii ya sasa, watesi wetu hawatakuwa ni silaha nyingine yoyote itakayobaki.

Tutashinda. Wakati ni UKUTA. Aluta continua!!!!!!
Mungu akubariki sana mh kingozi wetu mpendwa Lissu
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,670
2,000
kambarage.jpg

Udikteta ni Serikali ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache na wao ndiyo huwa sheria. Anayepinga watakayo, basi huonyeshwa cha mtema kuni. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Julai 19,1967


defence nimeliboresha tu Bandiko lako. Tunashukuru sana kwa kuleta bandiko kama hili wakati kama huu. MUNGU AKUBARIKI!!
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
103,722
2,000
Na sisi tukishinda Vita hii dhidi ya Mafisadi basi watoto wetu watakuwa na nchi nzuri yenye haki na yenye maendeleo lkn mpaka siku hiyo ifike ni lazima kuondoa kansa ya Kifisadi inayoiangamiza nchi hii Kansa hiyo ni fisadi lowasa, tundu lisu, Mbowe &Co.!

Pamoja na Pombe Magufuli (PhD) tutayashinda mafisadi na kuyaangamiza kabisa, sisi tuna Dola na Mungu wao mafisadi akina lowasa, tundu wana shetani na dhuluma!
Mkaanze na kina anaconda yupo bariadi anavizia vizia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom