Tundu Lissu: Ufukuaji wa Machifu unavunja Katiba na Sheria. Samia akemewe

Swali limeulizwa na mjumbe akiwataja yeye TAL,Mnyika,Mbowe,JK nk. Anasema hivyo ni vilemba vya heshima tu na kuna tofauti. Kikwete anakwenda kwenye mkutano na kuvikwa kilemba na wananchi,ni kilemba cha ukoka tu na haina mamlaka yeyote na inaishia hapo kwenye mkutano.
Lakini hii ya Samia ni Chiefdoms/Mamlaka ambapo mchakato umeshaanza kwa kupatikana machief zaidi ya 90.
 
View attachment 2116953
Kupitia mtandao wa ClubHouse Mzalendo wa Kweli Tundu Lissu anahutubia na anaeleza kwa kina historia ya machif. Ameeleza chimbuko la machif wakati wa ukoloni na kufutwa kwake 1965. Anasema katika utawala wa Mwalimu Nyerere bunge la Tz chini ya Katibu Pius Msekwa lilitunga sheria kupiga marufuku machif na shughuli zao na kuondoa kabisa masalia ya machif.

Jamaa anaongea mambo mazito hatua kwa hatua ngazi kwa ngazi. Anaeleza historia kama vile katunga yeye.

Anaendelea. Anasema Katiba ya sasa imepiga marufuku vyeo vya kurithi au jadi ikiwemo uchifu. (Nawaza: Mama Samia hajui Katiba?).

Anasema kurejesha machif ni kitendo cha kijinai. Anamuuliza Rais Samia au Chief Hangaya kama ameamua kupuuza sheria na matakwa ya nchi?

Anasema kama malengo ni mazuri kwa nini Samia hajaanzisha michakato ya kufufua mfumo wa Usultani huko Zanzibar 🤣🤣🤣🤣🤣

"Rais Samia amekuwa na mwenendo wa kudhalilisha na kuipuuza katiba ya JMT. Dawa ya makosa ya kupuuza katiba ni kwa bunge kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani" anasema ☹☹☹

Nasema pamoja na misingi ya Jamhuri na maono ya Mwalimu na mwenyekiti wa CCM kuvunjwa,lakini CCM imekuwa kimya na haijasema chochote. Anashangaa wazee wa nchi ikiwemo Pius Msekwa, NGO na taasisi za kisheria wamekuwa kimya huku vyama vingine vikipigana vikumbo kumpongeza Rais.

Anaeleza kuna malengo ya kisiasa ndani yake na kuvuruga kabisa mfumo huru wa Serikali za Mitaa.

Rais Samia anasema machief watakuwa wanatatua migogoro ya kijamii. Anahoji wenyeviti wa mitaa na mahakama zitakuwa na kazi gani? Samia anasema serikali imetenga fedha za kuanzia. Lissu anaahoji vyanzo ya mapato ya kugharamia shughuli za machief.

Tundu Lissu anahoji mfumo huu utaendeshwa kwa sheria ipi?

Anahitikisha kuwa Katiba Mpya ni muhimu sana kwa sababu nchi inaendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja au kikundi cha watu bila kuhofia chochote
Naendelea kumsikiliza kwa makini. Naomba na Rais Samia apewe link amsikilize

Hua sikubalianagi na huyu mwamba mambo mengi ila kwa hili nakubaliana naye 100%.
Wengi tumekua tunasema samia amekua rais wa nchi yetu kufuatana na katiba. Ukweli hana capacity. Hajui mambo mengi na kiitikadi sio mjamaa.
Ni mbinafsi ndio maana ameruhusu vigogo upigaji wa hela ya umma kwa kadri ya urefu wa kamba ya mbuzi ya kila kigogo.
Mungu akijalia 2025 nchi itaweza kupata magufuli mpya. Rip Jpm.
 
Yaani ni Kama mtu una matatizo lukuki unaamua kwenda kutafuta mengine kuongezea...,

In this day and age haya mambo ya Uchifu ni only symbolically na kila mtu kuyafanya kivyake..., sio kuyabeba kama taifa
 
Sifa za Lissu:
1. Smart
2.Knolewgeable
3.Outspoken
4. Bold and courageous.
5.Patriotic
6. Mtu mwenye foresight.

Ukiwa na sifa kama hizo na ukawa ni mwanasiasa tena wa upinzani, basi Africa kwako sio Sehemu sahihi na salama kwa wewe kuishi.
Aje huku tumumiminie lisasi zingine afe kabisa. Kwanini anaogogopa Kama yeye mwanaume?
 
Hua sikubalianagi na huyu mwamba mambo mengi ila kwa hili nakubaliana naye 100%.
Wengi tumekua tunasema samia amekua rais wa nchi yetu kufuatana na katiba. Ukweli hana capacity. Hajui mambo mengi na kiitikadi sio mjamaa.
Ni mbinafsi ndio maana ameruhusu vigogo upigaji wa hela ya umma kwa kadri ya urefu wa kamba ya mbuzi ya kila kigogo.
Mungu akijalia 2025 nchi itaweza kupata magufuli mpya. Rip Jpm.
Leo ndio umemkubali?
Aje huku tumumiminie lisasi zingine afe kabisa. Kwanini anaogogopa Kama yeye mwanaume?
Uhuru wa maoni ni pamoja na ujinga na upumbavu.
 
Sifa za Lissu:
1. Smart
2.Knolewgeable
3.Outspoken
4. Bold and courageous.
5.Patriotic
6. Mtu mwenye foresight.

Ukiwa na sifa kama hizo na ukawa ni mwanasiasa tena wa upinzani, basi Africa kwako sio Sehemu sahihi na salama kwa wewe kuishi.
Lissu ni kati ya wanasiasa wanaoaminika mno. Hadi leo Lissu hajawahi kunidanganya jambo ama kuyumba katika misimamo yake.
 
Lissu asimnukuu Mwalimu vibaya. Kwanza atafute a history book ya kwa nini Mwalimu Nyerere aliunda Wizara Maalumu ya Utamaduni mwaka 1963 na Waziri wa kwanza kuwa Chief Erasto Mbwana Mang'enya.

Yes, Mwalimu ali dissolve chiefdom lakini hakufuta maendeleo ya utamaduni. Katika dhana za maendeleo; yapo ya uchumi (Economic development), Social development, Political development na cultural development.

Mwalimu alikuwa ni mwanazuoni na Mwanamajumui mzuri wa Afrika. Asingeweza hata siku moja kupuuza maendeleo ya utamaduni ya nchi yake. Ndiyo maana katika hotuba yake ya mwaka 1963 alipounda Wizara ya Utamauni alisema; ameunda Wizara hiyo Maalumu ili mtafute mambo yote ya fahari ya makabila yetu yawe ni fahari ya Taifa la Tanganyika.

Utamaduni ni utambulisho wa Taifa, uchumi na hata chanzo cha ajira. Kwa mfano, muziki wa Jazz unafahamika kama Afro-American folk music. Ila umesambaa duniani kama biashara. Leo hii Kwaito ni utambulisho wa Afrika kusini. Vazi la Igbo ni fahari Nigeria. Mapiramidi ya Misri ni maendeleo ya sanaa za mikono. Sasa katika mzunguuko wa maendeleo ya utamaduni huwezi kuwaacha machifu.

Point: Mwalimu Nyerere alifuta mamlaka za kidola za Machifu lakini hakufuta maendeleo ya utamaduni. Rais Samia anachofanya ni kukuza maendeleo ya utamaduni ili utamaduni wetu uwe ajira, uchumi na biashara. Hakurudisha wala harudishi Tawala za kidola za Machifu. Kwa akili ndogo tu ya darasa la pili; Lissu alitakiwa kujua hilo haliwezekani.

Kwa hiyo sioni point yoyote ya kumsifia Lissu zaidi ya kumuona ni mtu asiyejua dhana mbili tofauti alizosimamia Mwalimu; ambazo ni kupiga vita ukabila na dhana ya maendeleo ya utamaduni.🙏🙏🙏
 
  • Thanks
Reactions: Tui

Mkuu naamini hoja ya Lissu na wengine unaielewa vizuri. Maneno yako ni kama unajaribu kuokoteza mambo kubariki jambo la hovyo
 
Mkuu naamini hoja ya Lissu na wengine unaielewa vizuri. Maneno yako ni kama unajaribu kuokoteza mambo kubariki jambo la hovyo:

Ni mjadala wa hoja ndugu. Kuna tofauti ya kurudisha dola za Machifu na kuwatumia Machifu kama kiungo cha maendeleo ya utamaduni. Mwalimu alipiga marufuku tawala za kidola za Machifu hakupinga maendeleo ya utamaduni. Rais Samia harudishi tawala za kidola za Machifu bali maendeleo ya utamaduni. Kuhusu Machifu kusaidia kujenga maadili na kusuluhisha migogoro ni utamaduni wa heshima tu kama tunavyokwenda kwa mjumbe, ila mwisho wa siku hawana nguvu zozote za kisheria. 🙏🙏
 
Hizo sherehe ni za kawaida na hata Rais alivyofanyiwa mwanza haikuwa na shida,tatizo ni kuziendekeza na kutaka kuzirudisha kwa kuzipa mamlaka yake ya awali. Haingii akilini kiongozi mkuu anasafiri kwa ajili ya kupewa uchifu!! Ikitokea imemkuta kwenye ziara rasmi ya majukumu ya kiserikali haina shida. Ni vizuri kujiamini kwa kuongoza kwa kufuata sheria na katiba. Hoja za Lisu zina mashiko hata kama na wao walishiriki nyakati za kampeni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom