Tundu Lissu: Uchaguzi huu siyo kusema tu "People's power" wala "tumekupa kura zote tayari"; huko ni kutiana ujinga. Uchaguzi ni kusoma makaratasi

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Haya yamejiri jana usiku wa tarehe 6/10/2020 Mlandizi katika semina ya ndani ya viongozi na wagombea ubunge, udiwani na wanachama wa CHADEMA wa majimbo mawili ya uchaguzi Kibaha mjini na vijijini.

Kwa ufupi TUNDU LISSU alitoa tahadhari na kufundisha yafuatayo kuhusu namna ya kuushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020, Oktoba 28;

1. Alisema, ushindi wa uchaguzi wa mwaka huu haupo kwenye kutiana ujinga wa kauli kama "people's power" au "mheshimiwa Rais umeshinda ukipiga kura, wewe nenda kalale". Aliwaonya kuwa wasitiane ujinga kwa kauli hizi bali, hizi kauli zitolewe tarehe 29/10/2020 baada ya ushindi kwelikweli.

2. Alisema, kuishinda CCM na kuitoa madarakani siyo kazi lelemama maana wana pesa nyingi, CHADEMA haina; mfumo wote wa uchaguzi unawabeba wao; polisi, TISS na NEC iko upande wao. Ndiyo maana ya tukio la kunizuia leo kuja hapa Mlandizi na kunizuia kuendelea na kampeni.

3. Kisha, akasema, kuwa kuishinda CCM ni vita ya mapambano very serious. Inahitaji kujitoa na kujiachilia kwelikweli....

Kwamba, Ili kuiondoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura, kwanza ni lazima uruke vihunzi/vikwazo vyote vya NEC, polisi na wasimamizi wa uchaguzi (DEDs) ambao wote ni makada wa CCM na wapo pale kupigania na kulinda maslahi ya chama chao - CCM.

4. Akasema kuwa, wakati wa kushangilia ushindi bado. Msije mkaingia kwenye mazoea ya kijinga hayo.....

Akawapa mfano wa aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mwaka 2015 wa CHADEMA Bw. Shelembi...

Akasema, ushahidi wote ulionesha kuwa ameshinda na kwa kutozingatia umakini akaanza kushangilia kabla ya kutangazwa.....

Ndani ya ukumbi wa majumuisho ya matokeo wakamdanganya kuwa tupate mapumziko kidogo, naye bila kutafakari akawakubalia....

Na alipotoka kidogo tu kuwapa kisogo, akachachuliwa na mpinzani wake Steven Masele aliyekwisha kumshinda tayari, haraka haraka akatangazwa mshindi. Mwisho wa siku kwa mshtuko wa presha, akaishia kufa....!!

Amewaambia, kilichopo mbele kwa sasa ndiyo FINAL BATTLE KUUENDEA USHINDI. Kwamba, kushindwa kutenda wajibu wetu kwa KUPAMBANA katika hatua hizi ni KUIPA USHINDI CCM asubuhi tu. Vita iliyoko mbele na ambayo lazima tushinde ni;

å Kuteuliwa na kuapishwa kwa mawakala wetu wote Tanzania nzima.

å Kuhakikisha kuwa mawakala wetu wote wanaingia katika vituo vyote vya kupigia kura.

å Kuhakikisha kuwa mawakala wetu wote wanapewa nakala za fomu za matokeo ya kura za kila kituo kwa ajili ya udiwani, ubunge na urais kwa kila kituo.

5. Akasema, hili likifanyika nchi nzima kwa ufanisi na ufasaha, hatua ya KUTANGAZA MSHINDI HALALI ni rahisi maana kila mtu atakuwa anajua nani kashinda kwa ushahidi wa fomu za matokeo kutoka kila kituo cha kupigia kura.

Akasisitiza kuwa, HIKI NDICHO AMBACHO CCM na NEC wanataka Kuhakikisha hakitokei na hii ndiyo VITA NA MAPAMBANO tunayosema na NI LAZIMA TUSHINDE YOTE HAYA kwa Kuhakikisha kuwa tunatumia nguvu ya umma na mikakati yetu. Hatuna fedha lakini watu (umma) unatuunga mkono. Tuitumie vizuri nguvu ya umma hii.

6. Alisema, USHINDI katika UCHAGUZI hauko kwenye kujaza NYOMI kwenye mikutano yetu ya kampeni wala ku - shout tu "people's power", bali uko kwenye kusoma makaratasi ya tume ya uchaguzi yanayoelekeza kila hatua ya mchakato wa uchaguzi.

7. Alisikitika kwa kusema kuwa, bahati mbaya wengi wa watu wetu wakiwemo viongozi wakipewa makaratasi ya tume badala ya kuyasoma na kuyaelewa, wao huyatupa kule na kubaki na kauli tu midomoni za kujipa matumaini hewa ya "tumeshinda, tutashinda ama People's power" na kujifurahisha na nyomi ya watu kwenye mikutano ya kampeni na kudhani kuwa huo tayari ni ushindi.

Akasema, huo ni ujinga na kutoelewa. Na hapo ndipo tunapopigiwa na kuibiwa kura zetu na CCM.

8. Alisisitiza kuwa, wizi mwingine upo kwenye mbinu ya kutengeneza VITUO HEWA VYA KUPIGIA KURA.

Akawasisitizia viongozi na wagombea kuwa wahakikishe kuwa wanayo orodha yote ya vituo HALALI vya kupigia kura katika kila KATA na JIMBO la uchaguzi lolote na wavihakiki kuwa ndivyo na vipo kweli.

Na siku ya Kujumuisha matokeo katani ama jimboni kwa msimamizi wa uchaguzi (DED), basi wawe na orodha hiyo iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi huyo huyo ili akitaja kituo ambacho hakipo kwenye orodha rasmi, akamatwe hapo hapo
na kuadhibiwa sawia.

7. Alimaliza kwa kusema, ikifika SAA 2 hadi 6 usiku siku ya tarehe 28/10/2020 mshindi atakuwa ameshajulikana kulingana na fomu za matokeo ya kila kituo ambazo mtakuwa nazo mikononi mwenu kama ushahidi....

Hiyo ndiyo shughuli iliyoko mbele yenu na mbele yetu....

Akasema, hii ikifanyika kwa ukamilifu, hapo unaweza kuanza kushangilia (kama umeshinda) na ruksa kutangaza matokeo yako ya Udiwani ama Ubunge ama Urais na wala hilo siyo kosa la jinai so long as unao ushahidi wa kura katika fomu za matokeo ya kila kituo cha kupigia kura...

Akasema, tukifanya haya USHINDI UKO WAZI na CCM kamwe hawawezi na hawajawahi kushinda popote kihalali katika SANDUKU LA KURA maana tayari hawana kibali cha UMMA (watu) na kwa MUNGU pia....

Na hii ndiyo maana tunasema, NCHI HII HAITATAWALIKA na HAPATATOSHA IWAPO mshindi halali hatatangazwa na badala yake atangazwe ambaye hajashinda.

Na ndiyo maana ya kusema, ikitokea hili hapo tutaingiza watu barabarani kudai haki yetu, haki yao ya USHINDI.

Alimaliza Tundu Lissu na kisha akaenda kulala.

Leo ziara Makamu mwenyeki - CHADEMA ndugu Tundu Lissu mkoa wa Pwani majimbo ya Kibaha mjini na vijijini inaendelea.
 
Nani asiyemjua Lissu hadi uhangaike kuchapisha makaratasi ? ni wapi uliona picha ya Mtume Muhammad , lakini mbona kila siku waislam wanamtaja ?
Nani asiyeijua Coca Cola au Pepsi, kwanini kila ujao wanachapicha mabango na matangazo ya TV, radio kila kona....Uliza watu wa marketing kuwa kwanini kuna kujitangaza hata kama unafahamika kama CCM?
 
Kweli ccm ilitukamata pabaya
Kutegemea polisi kumeifanya ccm ianguke sana , walionywa wakapuuza

FB_IMG_1574277425198.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom