Tundu Lissu: Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri

Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Sio kila binaadamu anauwezo wa kufikiri na kuelewa kama watu wengine. Wako watu wanasifa zote za binadamu lakini uwezo wao wa kufikiri kama samaki. Pahala pa kazi kama supervisor ataona kuwa barua yako haina viambatanisho au maelezo ya kutosha anaweza akakutaka utoe maelezo ya kutosha au uambatanishe vielezo, au akakukatalia kwa kuwaviambatanisho havijitoehelezi au akakubalia ila utakaporudi hakikisha unasubmit viambatanisho.
 
Utoro kazini ina adhabu mbaya sana ya kuachishwa kazi ndo kilichomkuta saivi nassari.

Kama ana nyaraka na ushahidi za kuomba ruhusa na akakubaliwa, apo kesi dogo sana ubunge hawezi vuliwa. Ila ikiwa aliondoka ndo baadae anaomba ruhusa dah kazi anayo, bora tuuu asihangaike kwenda ata mahakamani

ghost rider
 
Tunahitaji katiba mpya

Sasa hawa vyenge badala ya kushughulika kitu muhimu kama hiki cha katiba kubadili hii nchi,wanaishia kuangalia madaftari ya rollcalls!

Na majina yanayoangaliwa ni ya opposition only...wakati Mkono is outta bunge for decades now untouched!
 
YA JOSHUA NASSARI NA UBUNGE WAKE

Wandugu wapendwa salaam,

Nimesoma yanayomhusu Mh. Josh Nassari humu. Kuna mwelekeo mkubwa wa kukubaliana na hukumu ya Spika Ndugai kwamba Mh. Nassari hajahudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge, kwa hiyo amepata anachostahili.

Baadhi wameenda mbali zaidi na kudai Mh. Nassari 'amevuta mpunga' na kuuza jimbo. Wengine wamesema ni maandalizi ya 'kuunga mkono juhudi', n.k.

Katika yote haya, sijasikia yeyote akidai kujua upande wa Mh. Nassari mwenyewe una msimamo gani. Inaelekea tumekimbilia kwenye hukumu kutokana na maneno ya Spika na tafsiri zetu wenyewe.

Hii sio sawa sawa. Mimi nimewasiliana na Josh Nassari jana usiku. Amenitafuta mwenyewe kunitaka ushauri. Kwa maneno yake mwenyewe, hii habari ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge sio ya kweli.

Ameniambia alihudhuria vikao vya Bunge la November mwaka jana, na alisaini na kulipwa posho zake kama kawaida. 'Vikao vya Mkutano' ni pamoja na vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, kwa mujibu wa tafsiri ya neno 'kikao' katika Kanuni za Kudumu za Bunge.

Kama anayoyasema Mh. Nassari ni ya kweli, basi kuna ziada kubwa ya maneno tusiyoijua katika jambo hili. Sio sahihi kurukia kwenye hitimisho bila kusikiliza upande wake.

Pili ni kuhusu barua yake ya tarehe 29 January. Mh. Nassari ameniambia alikuwa anamuuguza mke wake ambaye alipata matatizo makubwa ya uzazi wakati anajifungua tarehe 27 January.

Siku iliyofuata, tarehe 28 (siku ya kuanza vikao vya Bunge) aliwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai. Akashauriwa na msaidizi huyo kumwandikia Spika Ndugai juu ya suala lake, na akafanya hivyo kesho tarehe 29 January.

Majibu ya barua ya Mh. Nassari kwa Spika Ndugai ni taarifa yake ya jana ya kumfuta Ubunge.

Sasa hapa kuna suala la tafsiri ya sheria. Je, kama ni kweli Spika Ndugai aliandikiwa barua ya kuombwa ruhusa katika mazingira hayo ya dharura na hakuijibu, hicho kimya chake kina maana gani kisheria??? Is it not the case of 'silence means consent' here???

Jambo la tatu ni la utaratibu wa uamuzi wenyewe. Spika Ndugai hajamuandikia au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na Mh. Nassari ili kumjulisha juu ya hatua anazotaka kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Ni kweli kwamba ibara ya 71 ya Katiba haijaweka utaratibu wa Spika kumwandikia au kumjulisha Mbunge juu ya hatua anazopanga kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano ya Bunge.

Je, ukimya huo wa Katiba una maana Spika Ndugai hawajibiki na hakuwajibika kumjulisha Mh. Nassari kabla ya kumfuta Ubunge???

Hili ni suala lingine la tafsiri ya sheria. 'Natural justice', misingi ya haki ya asili, inamtaka mtoa maamuzi yeyote yanayoweza kuathiri haki ya mtu mwingine, kumpa mtu huyo fursa ya kujitetea kabla ya uamuzi utakaomwathiri kutolewa.

Masharti haya ya haki ya asili ni ya lazima hata pale ambapo sheria haijaweka utaratibu huo. 'Audi alteram partem', 'sikiliza upande mwingine.' Huo ndio msimamo wa kisheria wa Tanzania hii.

La mwisho ni huu utaratibu wa Spika Ndugai kuwasiliana na mitandao ya kijamii au hadharani badala ya kuwasiliana kwanza na Mbunge anayehusika kwanza.

Mh. Nassari ameniambia amesikia taarifa za kufutwa Ubunge wake mitandaoni kama wewe na mimi. Na mimi nilisikia habari ya kufutiwa mshahara na posho za kibunge mitandaoni.

Je, huu ni utaratibu sahihi wa Spika wa Bunge kuwasiliana na Wabunge kuhusu masuala yao ya kibunge???

Yote haya ni masuala muhimu kuyaangalia kabla ya kukimbilia kwenye hukumu kwamba Mh. Nassari 'ameuza Jimbo', au amekosea, n.k.

Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri. Tuvute subira.

Tundu Lissu, MB
Tienen, Ubelgiji
'
Haki huinua taifa!
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
wewe kwa akili yako lisu yupo wapi sasa? akifanya nini
 
Ukiona umesoma bandiko la lissu ukatoka kapa we kufa tu!
huna faida kabisa!

huyu Jamaa sheria sijui alianza kusoma kabla hajazaliwa?
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Kama barua haikuonyesha kwanini spika hakumtafuta kujua yaliyomsibu achilia mbali kujua yupo hospitali gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Haya majibu yamfikie Lissu ikiwa yeye mwenyewe Lissu taarifa zake za tiba serikali na bunge inazipata kwa kupitia mitandao...
Zamani kulikuwa na kitu inaitwa "kata funua".... watajiliza sana
 
YA JOSHUA NASSARI NA UBUNGE WAKE

Wandugu wapendwa salaam,

Nimesoma yanayomhusu Mh. Josh Nassari humu. Kuna mwelekeo mkubwa wa kukubaliana na hukumu ya Spika Ndugai kwamba Mh. Nassari hajahudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge, kwa hiyo amepata anachostahili.

Baadhi wameenda mbali zaidi na kudai Mh. Nassari 'amevuta mpunga' na kuuza jimbo. Wengine wamesema ni maandalizi ya 'kuunga mkono juhudi', n.k.

Katika yote haya, sijasikia yeyote akidai kujua upande wa Mh. Nassari mwenyewe una msimamo gani. Inaelekea tumekimbilia kwenye hukumu kutokana na maneno ya Spika na tafsiri zetu wenyewe.

Hii sio sawa sawa. Mimi nimewasiliana na Josh Nassari jana usiku. Amenitafuta mwenyewe kunitaka ushauri. Kwa maneno yake mwenyewe, hii habari ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge sio ya kweli.

Ameniambia alihudhuria vikao vya Bunge la November mwaka jana, na alisaini na kulipwa posho zake kama kawaida. 'Vikao vya Mkutano' ni pamoja na vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, kwa mujibu wa tafsiri ya neno 'kikao' katika Kanuni za Kudumu za Bunge.

Kama anayoyasema Mh. Nassari ni ya kweli, basi kuna ziada kubwa ya maneno tusiyoijua katika jambo hili. Sio sahihi kurukia kwenye hitimisho bila kusikiliza upande wake.

Pili ni kuhusu barua yake ya tarehe 29 January. Mh. Nassari ameniambia alikuwa anamuuguza mke wake ambaye alipata matatizo makubwa ya uzazi wakati anajifungua tarehe 27 January.

Siku iliyofuata, tarehe 28 (siku ya kuanza vikao vya Bunge) aliwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai. Akashauriwa na msaidizi huyo kumwandikia Spika Ndugai juu ya suala lake, na akafanya hivyo kesho tarehe 29 January.

Majibu ya barua ya Mh. Nassari kwa Spika Ndugai ni taarifa yake ya jana ya kumfuta Ubunge.

Sasa hapa kuna suala la tafsiri ya sheria. Je, kama ni kweli Spika Ndugai aliandikiwa barua ya kuombwa ruhusa katika mazingira hayo ya dharura na hakuijibu, hicho kimya chake kina maana gani kisheria??? Is it not the case of 'silence means consent' here???

Jambo la tatu ni la utaratibu wa uamuzi wenyewe. Spika Ndugai hajamuandikia au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na Mh. Nassari ili kumjulisha juu ya hatua anazotaka kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Ni kweli kwamba ibara ya 71 ya Katiba haijaweka utaratibu wa Spika kumwandikia au kumjulisha Mbunge juu ya hatua anazopanga kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano ya Bunge.

Je, ukimya huo wa Katiba una maana Spika Ndugai hawajibiki na hakuwajibika kumjulisha Mh. Nassari kabla ya kumfuta Ubunge???

Hili ni suala lingine la tafsiri ya sheria. 'Natural justice', misingi ya haki ya asili, inamtaka mtoa maamuzi yeyote yanayoweza kuathiri haki ya mtu mwingine, kumpa mtu huyo fursa ya kujitetea kabla ya uamuzi utakaomwathiri kutolewa.

Masharti haya ya haki ya asili ni ya lazima hata pale ambapo sheria haijaweka utaratibu huo. 'Audi alteram partem', 'sikiliza upande mwingine.' Huo ndio msimamo wa kisheria wa Tanzania hii.

La mwisho ni huu utaratibu wa Spika Ndugai kuwasiliana na mitandao ya kijamii au hadharani badala ya kuwasiliana kwanza na Mbunge anayehusika kwanza.

Mh. Nassari ameniambia amesikia taarifa za kufutwa Ubunge wake mitandaoni kama wewe na mimi. Na mimi nilisikia habari ya kufutiwa mshahara na posho za kibunge mitandaoni.

Je, huu ni utaratibu sahihi wa Spika wa Bunge kuwasiliana na Wabunge kuhusu masuala yao ya kibunge???

Yote haya ni masuala muhimu kuyaangalia kabla ya kukimbilia kwenye hukumu kwamba Mh. Nassari 'ameuza Jimbo', au amekosea, n.k.

Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri. Tuvute subira.

Tundu Lissu, MB
Tienen, Ubelgiji
'
Hivi lissu na kambi nzima ya upinzani walikuwa wapi kumshauri dogo kablanya yote haya?
 
Pamoja na mapungufu yake lakini Tundu Antipas Lisu ana uwezo mkubwa wa kiakili.

Bunge kama sehemu ya kutunga sheria linapaswa kuwa makini kwa kila jambo, binafsi namkubali sana mzee Chenge na yule Zungu wale Nassari wangemchukulia poa tu.

Yaani tukarudie uchaguzi kwa gharama kubwa kisa Joshua alikuwa anamuuguza mkewe so hakufika bungeni?!!
"chukulia powa tu"... kila mtu na kila idara anachukulia powa tu.... wezi wa serikalini tuwachukulie powa tu.. Noway
 
Lissu kwenye Sheria wewe ni numberi one...hata Ndugai kajifunza kitu kwamba huwezi kukurupuka na kumfukuza hata mfanyakazi wako wa ndani bila kumwambia personally before uanze kutangaza kwa majirani

Tena hao majirani wakiwa na busara watakuona wewe hamnazo.
hayo maneno mawili ya kilatini yamemfanya awe nambari one?
Kuabudu pia ni ugonjwa
 
Apeleke ushahidi safari hii sio taarifa mahakamani kama kipindi kile la sivyo asipoteze muda wake.
 
Back
Top Bottom