Tundu Lissu: Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri


Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,162
Likes
20,178
Points
280
Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,162 20,178 280
YA JOSHUA NASSARI NA UBUNGE WAKE

Wandugu wapendwa salaam,

Nimesoma yanayomhusu Mh. Josh Nassari humu. Kuna mwelekeo mkubwa wa kukubaliana na hukumu ya Spika Ndugai kwamba Mh. Nassari hajahudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge, kwa hiyo amepata anachostahili.

Baadhi wameenda mbali zaidi na kudai Mh. Nassari 'amevuta mpunga' na kuuza jimbo. Wengine wamesema ni maandalizi ya 'kuunga mkono juhudi', n.k.

Katika yote haya, sijasikia yeyote akidai kujua upande wa Mh. Nassari mwenyewe una msimamo gani. Inaelekea tumekimbilia kwenye hukumu kutokana na maneno ya Spika na tafsiri zetu wenyewe.

Hii sio sawa sawa. Mimi nimewasiliana na Josh Nassari jana usiku. Amenitafuta mwenyewe kunitaka ushauri. Kwa maneno yake mwenyewe, hii habari ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge sio ya kweli.

Ameniambia alihudhuria vikao vya Bunge la November mwaka jana, na alisaini na kulipwa posho zake kama kawaida. 'Vikao vya Mkutano' ni pamoja na vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, kwa mujibu wa tafsiri ya neno 'kikao' katika Kanuni za Kudumu za Bunge.

Kama anayoyasema Mh. Nassari ni ya kweli, basi kuna ziada kubwa ya maneno tusiyoijua katika jambo hili. Sio sahihi kurukia kwenye hitimisho bila kusikiliza upande wake.

Pili ni kuhusu barua yake ya tarehe 29 January. Mh. Nassari ameniambia alikuwa anamuuguza mke wake ambaye alipata matatizo makubwa ya uzazi wakati anajifungua tarehe 27 January.

Siku iliyofuata, tarehe 28 (siku ya kuanza vikao vya Bunge) aliwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai. Akashauriwa na msaidizi huyo kumwandikia Spika Ndugai juu ya suala lake, na akafanya hivyo kesho tarehe 29 January.

Majibu ya barua ya Mh. Nassari kwa Spika Ndugai ni taarifa yake ya jana ya kumfuta Ubunge.

Sasa hapa kuna suala la tafsiri ya sheria. Je, kama ni kweli Spika Ndugai aliandikiwa barua ya kuombwa ruhusa katika mazingira hayo ya dharura na hakuijibu, hicho kimya chake kina maana gani kisheria??? Is it not the case of 'silence means consent' here???

Jambo la tatu ni la utaratibu wa uamuzi wenyewe. Spika Ndugai hajamuandikia au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na Mh. Nassari ili kumjulisha juu ya hatua anazotaka kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Ni kweli kwamba ibara ya 71 ya Katiba haijaweka utaratibu wa Spika kumwandikia au kumjulisha Mbunge juu ya hatua anazopanga kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano ya Bunge.

Je, ukimya huo wa Katiba una maana Spika Ndugai hawajibiki na hakuwajibika kumjulisha Mh. Nassari kabla ya kumfuta Ubunge???

Hili ni suala lingine la tafsiri ya sheria. 'Natural justice', misingi ya haki ya asili, inamtaka mtoa maamuzi yeyote yanayoweza kuathiri haki ya mtu mwingine, kumpa mtu huyo fursa ya kujitetea kabla ya uamuzi utakaomwathiri kutolewa.

Masharti haya ya haki ya asili ni ya lazima hata pale ambapo sheria haijaweka utaratibu huo. 'Audi alteram partem', 'sikiliza upande mwingine.' Huo ndio msimamo wa kisheria wa Tanzania hii.

La mwisho ni huu utaratibu wa Spika Ndugai kuwasiliana na mitandao ya kijamii au hadharani badala ya kuwasiliana kwanza na Mbunge anayehusika kwanza.

Mh. Nassari ameniambia amesikia taarifa za kufutwa Ubunge wake mitandaoni kama wewe na mimi. Na mimi nilisikia habari ya kufutiwa mshahara na posho za kibunge mitandaoni.

Je, huu ni utaratibu sahihi wa Spika wa Bunge kuwasiliana na Wabunge kuhusu masuala yao ya kibunge???

Yote haya ni masuala muhimu kuyaangalia kabla ya kukimbilia kwenye hukumu kwamba Mh. Nassari 'ameuza Jimbo', au amekosea, n.k.

Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri. Tuvute subira.

Tundu Lissu, MB
Tienen, Ubelgiji
'
 
mbarika

mbarika

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2015
Messages
1,719
Likes
1,066
Points
280
mbarika

mbarika

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2015
1,719 1,066 280
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Kenge ww weka vifungu vya sheria vinavyo kinzana na alivo vitaja Hapo Juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hanang1

Hanang1

Member
Joined
Mar 11, 2019
Messages
59
Likes
47
Points
25
Hanang1

Hanang1

Member
Joined Mar 11, 2019
59 47 25
Pamoja na mapungufu yake lakini Tundu Antipas Lisu ana uwezo mkubwa wa kiakili.

Bunge kama sehemu ya kutunga sheria linapaswa kuwa makini kwa kila jambo, binafsi namkubali sana mzee Chenge na yule Zungu wale Nassari wangemchukulia poa tu.

Yaani tukarudie uchaguzi kwa gharama kubwa kisa Joshua alikuwa anamuuguza mkewe so hakufika bungeni?!!
Leo akili imekurudia
 
PumziNdefu

PumziNdefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
469
Likes
942
Points
180
PumziNdefu

PumziNdefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
469 942 180
Ujana na dharau nyingi sana. Sioni sababu ya msingi inayo shawishi kwanini alikuwa haendi bungeni. Pia kwanini wabunge wenzie walikuwa hawampi ushauri juu ya jambo hilo ambalo lipo wazi kikatiba na kanuni za bunge. Mambo mengine mta mulaumu sana spika au rais wa JMT kwa kuwaonea tu.
Si amesema alitoa taarifa za kumuuguza mke wake?? Au hiyo sio sababu ya msingi kwa mtazamo wako?? Au ni roho mbaya tu uliyonayo??
 
K

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Messages
1,514
Likes
990
Points
280
K

Kuntakint

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2011
1,514 990 280
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Anaeumwa na mke wake siyo Ansari hivyo watakapotaka prove ndio ataweza cheti au vyetu vya hospital
 
babukijana

babukijana

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2009
Messages
5,625
Likes
2,165
Points
280
babukijana

babukijana

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2009
5,625 2,165 280
Unaweza ukakuta ww uliyeandika huu usenge umeajiriwa na mwanaume mwenzio na hapa umepost huu utoto kwa kutumia computer ya huyo mwanaume aliyekuajiri. Unaoongea kwa nyodo maana umevimba makalio kisa kila mwisho wa mwezi unapokea mshahara. Lissu sio jobless kwa taarifa yako maana hajakimbia nchi kwani yuko Ulaya kwa matibabu baada ya kushambuliwa na hao unaowaopa tundu la mbolea hapo nyuma. Kama umechoka kuchangia kwa nidhamu jiandae kukutana na lugha ambazo hutokaa uamini ww ****.
Kaf.rwe we kima kule alipo ni jobless mama we,sijaona jitu ngumbaru km ww badala kutafuta ugali wa wanao unahangaishana na siasa za kifala,haya we mjasiriamali unatukana waajiriwa biashara yenyewe usikute unafuga nguruwe🤣. Hapo ulipo unanuka mafi matupu
 
V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Messages
4,310
Likes
2,801
Points
280
V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2014
4,310 2,801 280
Iwe kweli basi kuwa Nasari 'hajaunga mkono juhudi '. Siamini kama Nasari hajui kilichotokea, siamini kuwa 'mpango' wa kumpoka Nasari Ubunge uwe siri kiasi cha kutovuja kabla.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
570
Likes
737
Points
180
M

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2017
570 737 180
Kaf.rwe we kima kule alipo ni jobless mama we,sijaona jitu ngumbaru km ww badala kutafuta ugali wa wanao unahangaishana na siasa za kifala,haya we mjasiriamali unatukana waajiriwa biashara yenyewe usikute unafuga nguruwe🤣. Hapo ulipo unanuka mafi matupu
Hakuna basha anayehitaji shoga asiye na shanga. Kapelekee mabasha wa kichaga huko wanaokula hilo shimo na condom.
 

Forum statistics

Threads 1,272,373
Members 489,924
Posts 30,449,207