Tundu Lissu: Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri


Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,162
Likes
20,178
Points
280
Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,162 20,178 280
YA JOSHUA NASSARI NA UBUNGE WAKE

Wandugu wapendwa salaam,

Nimesoma yanayomhusu Mh. Josh Nassari humu. Kuna mwelekeo mkubwa wa kukubaliana na hukumu ya Spika Ndugai kwamba Mh. Nassari hajahudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge, kwa hiyo amepata anachostahili.

Baadhi wameenda mbali zaidi na kudai Mh. Nassari 'amevuta mpunga' na kuuza jimbo. Wengine wamesema ni maandalizi ya 'kuunga mkono juhudi', n.k.

Katika yote haya, sijasikia yeyote akidai kujua upande wa Mh. Nassari mwenyewe una msimamo gani. Inaelekea tumekimbilia kwenye hukumu kutokana na maneno ya Spika na tafsiri zetu wenyewe.

Hii sio sawa sawa. Mimi nimewasiliana na Josh Nassari jana usiku. Amenitafuta mwenyewe kunitaka ushauri. Kwa maneno yake mwenyewe, hii habari ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge sio ya kweli.

Ameniambia alihudhuria vikao vya Bunge la November mwaka jana, na alisaini na kulipwa posho zake kama kawaida. 'Vikao vya Mkutano' ni pamoja na vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, kwa mujibu wa tafsiri ya neno 'kikao' katika Kanuni za Kudumu za Bunge.

Kama anayoyasema Mh. Nassari ni ya kweli, basi kuna ziada kubwa ya maneno tusiyoijua katika jambo hili. Sio sahihi kurukia kwenye hitimisho bila kusikiliza upande wake.

Pili ni kuhusu barua yake ya tarehe 29 January. Mh. Nassari ameniambia alikuwa anamuuguza mke wake ambaye alipata matatizo makubwa ya uzazi wakati anajifungua tarehe 27 January.

Siku iliyofuata, tarehe 28 (siku ya kuanza vikao vya Bunge) aliwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai. Akashauriwa na msaidizi huyo kumwandikia Spika Ndugai juu ya suala lake, na akafanya hivyo kesho tarehe 29 January.

Majibu ya barua ya Mh. Nassari kwa Spika Ndugai ni taarifa yake ya jana ya kumfuta Ubunge.

Sasa hapa kuna suala la tafsiri ya sheria. Je, kama ni kweli Spika Ndugai aliandikiwa barua ya kuombwa ruhusa katika mazingira hayo ya dharura na hakuijibu, hicho kimya chake kina maana gani kisheria??? Is it not the case of 'silence means consent' here???

Jambo la tatu ni la utaratibu wa uamuzi wenyewe. Spika Ndugai hajamuandikia au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na Mh. Nassari ili kumjulisha juu ya hatua anazotaka kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Ni kweli kwamba ibara ya 71 ya Katiba haijaweka utaratibu wa Spika kumwandikia au kumjulisha Mbunge juu ya hatua anazopanga kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano ya Bunge.

Je, ukimya huo wa Katiba una maana Spika Ndugai hawajibiki na hakuwajibika kumjulisha Mh. Nassari kabla ya kumfuta Ubunge???

Hili ni suala lingine la tafsiri ya sheria. 'Natural justice', misingi ya haki ya asili, inamtaka mtoa maamuzi yeyote yanayoweza kuathiri haki ya mtu mwingine, kumpa mtu huyo fursa ya kujitetea kabla ya uamuzi utakaomwathiri kutolewa.

Masharti haya ya haki ya asili ni ya lazima hata pale ambapo sheria haijaweka utaratibu huo. 'Audi alteram partem', 'sikiliza upande mwingine.' Huo ndio msimamo wa kisheria wa Tanzania hii.

La mwisho ni huu utaratibu wa Spika Ndugai kuwasiliana na mitandao ya kijamii au hadharani badala ya kuwasiliana kwanza na Mbunge anayehusika kwanza.

Mh. Nassari ameniambia amesikia taarifa za kufutwa Ubunge wake mitandaoni kama wewe na mimi. Na mimi nilisikia habari ya kufutiwa mshahara na posho za kibunge mitandaoni.

Je, huu ni utaratibu sahihi wa Spika wa Bunge kuwasiliana na Wabunge kuhusu masuala yao ya kibunge???

Yote haya ni masuala muhimu kuyaangalia kabla ya kukimbilia kwenye hukumu kwamba Mh. Nassari 'ameuza Jimbo', au amekosea, n.k.

Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri. Tuvute subira.

Tundu Lissu, MB
Tienen, Ubelgiji
'
 
M

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
570
Likes
737
Points
180
M

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2017
570 737 180
Kupiga kura ya ndiyo au hapana ni mojawapo ya kazi za mbunge bungeni si kuongea tu
Seriously uende kupiga kura ya ndio au hapana kisha uchukue sitting allowance ya 200,000, na bado uone ni sahihi mtu kulipwa hela ya hivyo!? Hiyo hata mtoto mdogo si anaweza kwenda kuweka ndio au hapana.
 
MKANDAHARI

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2011
Messages
2,603
Likes
2,406
Points
280
MKANDAHARI

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2011
2,603 2,406 280
Chadema kazi kuhubiri utawala wa sheria huku hamuwezi kabisa kufuata hata tone la utawala wa sheria wala democrasia.

Hauendi bungeni miezi mitatu unajirusha na mademu Ulaya unategemea nini?.

Sheria ni msumeno

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM ndio mnafuata utawala wa sheria? unasemaje kuhusu chattle international airport iliyojengwa bila gharama kuidhinishwa na bunge?
 
MKANDAHARI

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2011
Messages
2,603
Likes
2,406
Points
280
MKANDAHARI

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2011
2,603 2,406 280
Pamoja na mapungufu yake lakini Tundu Antipas Lisu ana uwezo mkubwa wa kiakili.

Bunge kama sehemu ya kutunga sheria linapaswa kuwa makini kwa kila jambo, binafsi namkubali sana mzee Chenge na yule Zungu wale Nassari wangemchukulia poa tu.

Yaani tukarudie uchaguzi kwa gharama kubwa kisa Joshua alikuwa anamuuguza mkewe so hakufika bungeni?!!
sema YOSHUA alikuwa anakuuguza wewe. napata wasiwasi ni kwa nini leo unamuunga mkono mwana CHADEMA wakati sio kawaida yako? mbona ulikuwa unafurahia Lissu kupigwa risasi pamoja na kunyimwa stahiki zake ikiwamo matibabu na mshahara wake? leo imekuwaje? pole sana bibie
 
K

konyola

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Messages
1,036
Likes
1,315
Points
280
K

konyola

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2016
1,036 1,315 280
LEO NIMEMCHANGIA NDUGU YANGU KAKA YANGU TUNDU AM LISSU MOYO WANGU UMETULIA NA MAPIGO YA MOYO YANAKWENDA MORORO KABYSA NA KILA MWEZI NITAFANYA HIVYO KWANI HUYU NDIYE MWOKOZI WA NCHI HII AFU NAMPENDA LISSU ILE MBAYA MAANA NIKIMSIKIA MTU ANAMSEMA VIBAYA HUWA NATAMANI NIMLE AIRTEL NA VODA KAMA SIYO KUMFUMUA MFEREJI WA SUEZI HUU MWAKA KUNA JITU LITAJINYONGA KIUKWELI NIKIAMBIWA NIMPENDE BASHITE KAMA NINAVYOMPENDA LISSU NI BORA NIKAFUNGWE MIAKA 100 NA KAZI NGUMU KILA SIKU HUKO JELA
 
Meking

Meking

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Messages
223
Likes
30
Points
45
Meking

Meking

JF-Expert Member
Joined May 24, 2011
223 30 45
Jambo la tatu ni la utaratibu wa uamuzi wenyewe. Spika Ndugai hajamuandikia au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na Mh. Nassari ili kumjulisha juu ya hatua anazotaka kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.
Ni kweli kwamba ibara ya 71 ya Katiba haijaweka utaratibu wa Spika kumwandikia au kumjulisha Mbunge juu ya hatua anazopanga kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano ya Bunge.
Yaani mwanasheria msomi anataka spika ndiyo amuandikie mtoro kuhusu utoro wa mtoro mwenyewe?
Kwamba mtoro mwenyewe hata hajielewi siyo?
Hivi mnauchukuliaje ubunge nyie watu? Yaani wananchi wanakosa uwakilishi kwa kujisikia na sababu za kizembe tu...
 
M

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
570
Likes
737
Points
180
M

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2017
570 737 180
Msimshangae huyo mgonjwa hana kazi huko Belgium kwahiyo kazi yake ni hiyo,kushinda na laptop kuandika upuuzi.
Mange Kimambi na huyu hawapishani,
Tofauti ni yule aliandika udaku huyu anaandika sheria ambayo hata yy haijui anaotea.
Ni kawaida kwa majobless wote Ulaya.
Unaweza ukakuta ww uliyeandika huu usenge umeajiriwa na mwanaume mwenzio na hapa umepost huu utoto kwa kutumia computer ya huyo mwanaume aliyekuajiri. Unaoongea kwa nyodo maana umevimba makalio kisa kila mwisho wa mwezi unapokea mshahara. Lissu sio jobless kwa taarifa yako maana hajakimbia nchi kwani yuko Ulaya kwa matibabu baada ya kushambuliwa na hao unaowaopa tundu la mbolea hapo nyuma. Kama umechoka kuchangia kwa nidhamu jiandae kukutana na lugha ambazo hutokaa uamini ww ****.
 
Isanga family

Isanga family

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Messages
6,384
Likes
6,444
Points
280
Isanga family

Isanga family

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2015
6,384 6,444 280
Ubunge unafutwa kirahisi hivyo basi kuna shida ya Elimu yetu ya juu sio bure...
 
Kima wa Maputo

Kima wa Maputo

New Member
Joined
Mar 12, 2019
Messages
4
Likes
5
Points
5
Kima wa Maputo

Kima wa Maputo

New Member
Joined Mar 12, 2019
4 5 5
Nimesoma kwa makini sna hoja za lissu, nachoweza kusema ni kuwa wajibu wa Chama tawala ni kujali pia sauti za wanaowaongoza. Kama Nasari alichaguliwa kwa haki. Wanaumiaa nini kungoja kamwaka kamoja tu amalize muhula wake. Kwa nini wanadharau gharama za uchaguzi Katika nchi masikini kama hii. Makusanyo yao wnaficha sasa ilihali inajulikana wako 50 percent
 
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
4,344
Likes
2,785
Points
280
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
4,344 2,785 280
TL sheria kama kazaliwa nayo aisee
Anajua mpaka anapitiliza yaani Mungu huyu, yeye ndio angesimama kama wakili, tungeomba kesi iamishiwe uwanja wa taifa. Kuna sehemu alinichanganya, ibara ya 71 kuwa kimya kuhusu spika kumtaarifu mbunge kabla hajamuhukumu. Nilishtuka nikajua basi Ndugai ndio aliegemea hapo basi katumaliza. Nikijapa moyo konde nikaendelea kumsoma mbobezi wa sheria. Akasema kukaa kimya hakumpi mamlaka ya kuhukumu kabla ya kumsikiliza, hiyo ni haki ya Asili ya kila mtu. Ndugai kaingia chaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
4,344
Likes
2,785
Points
280
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
4,344 2,785 280
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Wewe shabikia ujinga tutakutana mahakama kuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
4,344
Likes
2,785
Points
280
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
4,344 2,785 280
Chadema kazi kuhubiri utawala wa sheria huku hamuwezi kabisa kufuata hata tone la utawala wa sheria wala democrasia.

Hauendi bungeni miezi mitatu unajirusha na mademu Ulaya unategemea nini?.

Sheria ni msumeno

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeliona hilo la kujilusha na mademu, pole maana moyo unakuuma sana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,272,376
Members 489,924
Posts 30,449,310