Tundu Lissu: Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri

tatizo sheria au katiba haijaweka wazi kama kunautaratibu wa kukusikiliza yenyewe inasema ukifulluliza kutega mara tatu basi umekosa sifa labda wafanyie marekebisho hapo lakini tayari nasari ameshakosa sifa si mbunge hata aende mahakamani
Tuache sheria ichukue mkondo wake. Nasari aende mahakamani nasi tujifunze jinsi wanavyo tafsiri sheria. Sheria ni zaidi ya kiingereza au kiswahili ina mengi yaliyojificha.
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Huwezi elewa hata ukieleweshwa, kwa sababu akili hiyo huna
 
Huyu TL hana mbadala linapokuja suala la kutafsiri vipengele vya sheria. Ndiyo maana Bunge hadi leo halimfuta TL ubunge wake wakaona wamkimbilie Nassari kumbe nako watakutana na mashuti ya TL kupitia mahakamani, kinadharia atahudhuria TL hivyo tusubiri TAFSIRI nyingine juu ya maamuzi ya kukurupuka yanayotokea nchini
 
Yaani mtu anauguza mke wake na taarifa katoa halafu wanamfutia ubunge? Kama sio ukatili ni nini??
Tuna viongozi wa ajabu kuwahi kutokea.

Ujana na dharau nyingi sana. Sioni sababu ya msingi inayo shawishi kwanini alikuwa haendi bungeni. Pia kwanini wabunge wenzie walikuwa hawampi ushauri juu ya jambo hilo ambalo lipo wazi kikatiba na kanuni za bunge. Mambo mengine mta mulaumu sana spika au rais wa JMT kwa kuwaonea tu.
 
Siku iliyofuata, tarehe 28 (siku ya kuanza vikao vya Bunge) aliwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai. Akashauriwa na msaidizi huyo kumwandikia Spika Ndugai juu ya suala lake, na akafanya hivyo kesho tarehe 29 January
Kutojibu barua was a deliberate move apate mahali pa kum -pin! Lakini amebugi maana kuna hivi vitu!

There are two main rules of natural justice:
1. The "hearing rule" is that people who will "e affected "by a projected decision must "be given an opportunity to express their views to the judgment maker.

2. The "bias rule" is that the judgment maker must "be impartial and must have no personal stake in the matter to be decided. This guide deals with deliberations that commonly rise when the rules of natural justice are applied to administrative decision making

Natural Justice is an expression of English common law. In one of the English decisions Viscount Haldane observed: …….those whose duty it is to decide must act judicially. They must deal with the question referred to them without "bias” and they must give to each of the parties the opportunity of adequately presenting the case made. The decision must come to the spirit and with the sense of responsibility of a tribunal whose duty it is to meet out justice

Aristotle "before the era of Christ spoke of such principles calling it as universal law. Justinian in the fifth and sixth Centuries called it jura naturalia i.e Natural Law
 
katika watu wenye umeme mdg baada ya jiwe anafata sabufa yaani jamaa wana uwezo mdg hadi unajiuliza walitoboaje izo nafasi kubwa
upooo
IMG-20190313-WA0058.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Demokrasia yetu ikiruhusu mwakilishi wa wananchi akiuguliwa akae nyumbani kumuuguza patina wake kwa Munda wowote ule itageuka kuwa domokrasia; afu utakuta mtu anamzuia mwenzake asitumie Mitandao uku yeye akitumia kwa asilimia Mia. Kweli yajayo yanafurahisha.
 
YA JOSHUA NASSARI NA UBUNGE WAKE

Wandugu wapendwa salaam,

Nimesoma yanayomhusu Mh. Josh Nassari humu. Kuna mwelekeo mkubwa wa kukubaliana na hukumu ya Spika Ndugai kwamba Mh. Nassari hajahudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge, kwa hiyo amepata anachostahili.

Baadhi wameenda mbali zaidi na kudai Mh. Nassari 'amevuta mpunga' na kuuza jimbo. Wengine wamesema ni maandalizi ya 'kuunga mkono juhudi', n.k.

Katika yote haya, sijasikia yeyote akidai kujua upande wa Mh. Nassari mwenyewe una msimamo gani. Inaelekea tumekimbilia kwenye hukumu kutokana na maneno ya Spika na tafsiri zetu wenyewe.

Hii sio sawa sawa. Mimi nimewasiliana na Josh Nassari jana usiku. Amenitafuta mwenyewe kunitaka ushauri. Kwa maneno yake mwenyewe, hii habari ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge sio ya kweli.

Ameniambia alihudhuria vikao vya Bunge la November mwaka jana, na alisaini na kulipwa posho zake kama kawaida. 'Vikao vya Mkutano' ni pamoja na vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, kwa mujibu wa tafsiri ya neno 'kikao' katika Kanuni za Kudumu za Bunge.

Kama anayoyasema Mh. Nassari ni ya kweli, basi kuna ziada kubwa ya maneno tusiyoijua katika jambo hili. Sio sahihi kurukia kwenye hitimisho bila kusikiliza upande wake.

Pili ni kuhusu barua yake ya tarehe 29 January. Mh. Nassari ameniambia alikuwa anamuuguza mke wake ambaye alipata matatizo makubwa ya uzazi wakati anajifungua tarehe 27 January.

Siku iliyofuata, tarehe 28 (siku ya kuanza vikao vya Bunge) aliwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai. Akashauriwa na msaidizi huyo kumwandikia Spika Ndugai juu ya suala lake, na akafanya hivyo kesho tarehe 29 January.

Majibu ya barua ya Mh. Nassari kwa Spika Ndugai ni taarifa yake ya jana ya kumfuta Ubunge.

Sasa hapa kuna suala la tafsiri ya sheria. Je, kama ni kweli Spika Ndugai aliandikiwa barua ya kuombwa ruhusa katika mazingira hayo ya dharura na hakuijibu, hicho kimya chake kina maana gani kisheria??? Is it not the case of 'silence means consent' here???

Jambo la tatu ni la utaratibu wa uamuzi wenyewe. Spika Ndugai hajamuandikia au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na Mh. Nassari ili kumjulisha juu ya hatua anazotaka kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Ni kweli kwamba ibara ya 71 ya Katiba haijaweka utaratibu wa Spika kumwandikia au kumjulisha Mbunge juu ya hatua anazopanga kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano ya Bunge.

Je, ukimya huo wa Katiba una maana Spika Ndugai hawajibiki na hakuwajibika kumjulisha Mh. Nassari kabla ya kumfuta Ubunge???

Hili ni suala lingine la tafsiri ya sheria. 'Natural justice', misingi ya haki ya asili, inamtaka mtoa maamuzi yeyote yanayoweza kuathiri haki ya mtu mwingine, kumpa mtu huyo fursa ya kujitetea kabla ya uamuzi utakaomwathiri kutolewa.

Masharti haya ya haki ya asili ni ya lazima hata pale ambapo sheria haijaweka utaratibu huo. 'Audi alteram partem', 'sikiliza upande mwingine.' Huo ndio msimamo wa kisheria wa Tanzania hii.

La mwisho ni huu utaratibu wa Spika Ndugai kuwasiliana na mitandao ya kijamii au hadharani badala ya kuwasiliana kwanza na Mbunge anayehusika kwanza.

Mh. Nassari ameniambia amesikia taarifa za kufutwa Ubunge wake mitandaoni kama wewe na mimi. Na mimi nilisikia habari ya kufutiwa mshahara na posho za kibunge mitandaoni.

Je, huu ni utaratibu sahihi wa Spika wa Bunge kuwasiliana na Wabunge kuhusu masuala yao ya kibunge???

Yote haya ni masuala muhimu kuyaangalia kabla ya kukimbilia kwenye hukumu kwamba Mh. Nassari 'ameuza Jimbo', au amekosea, n.k.

Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri. Tuvute subira.

Tundu Lissu, MB
Tienen, Ubelgiji
'
bado wewe. Yeye amewasiliana na NEC
 
magoiga_sn
•Follow

379 likes

magoiga_sn
Huenda ndiyo maana Nassari alipewa jina la Dogo Janja
_
Na Magoiga SN
_
Kuliandikia bunge barua ya kulitaarifu kuwa hautakuwepo ni jambo jema lakini hiyo siyo ruhusa, ibara ya 71 ya katiba na kanuni ya 147 ya kanuni za kudumu za bunge zinaeleza wazi. Unatakiwa kuwa na ruhusa ya maandishi kutoka kwa spika wa bunge husika kuhusu kutohudhuria kwakoni jambo jingine.
_
Katiba haijasema mbunge atalitaarifu bunge kuwa hatohudhuria vikao vya bunge au mikutano ya bunge, bali katiba na kanuni za kudumu za bunge ukisoma ile kanuni ya 147 imeeleza kuwa Mbunge ambaye hatahudhuria mikutano ya bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa spika moja kwa moja atapoteza ubunge wake.
_
Kama unapata shida kuelewa, pigia mstari neno BILA RUHUSA YA MAANDISHI kutoka kwa spika, kisha ujiulize.kuwa kutoa taarifa ya kutokuwepo kwako ndiyo umepewa ruhusa ya maandishi na ofisi ya spika!?? Utaelewa kuwa aidha Nassari alifanya kosa hilo kimkakati au mazoea ya kufanya mambo kwa tamaduni za 'business as usual' yamemgeuka Nassari.
_
Kwahiyo, Nassari baada ya kuandika barua alipaswa awe na barua kutoka ofisi ya spika inayompa ruhusa sasa ya kutohudhuria vikao hivyo vya mikutano ya bunge.
_
Tuache unafiki na tukubali kuwa Nassari amejichanganya kwa bahati mbaya au kimkakati, na ktk kujichanganya huko katiba na kanuni za kudumu za bunge zimemuengua 'automatically'.
_
Anyway, ukitaka kujua Nassari amecheza kete kwa akili ya juu sana kuliko akina Mtatiro, Mollel, Waitara nk, watazame wafuasi wa Chadema mitandaoni, hawajui wamtetee au wamtukane kama walivyofanya kwa wengine.
_
Magoiga SN |¦|Think Beyond The Obvious

View all 35 comments
 
Lissu kama yako tu (kupata mshahara na marupurupu) yanakushinda, je utaweza kubeba ya wengine? Hata hivyo bado naamini Nassari kaonewa.
 
Kwa hili la Nassari Kuna ukakasi mwingi Sana Nassari anaujua.
This is a play to stall a serious movement !

!
Will need more data to understand!
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Very hopeless judgement. Mtu asiye mtumishi wa umma analazimika kupata kibali kwenda kutibiwa hospitali yoyote ile mahali popote pale alipiamua kutibiwa?

Humu jukwaani tuna watu wana ujinga wa kupindukia.

Tundu Lisu ametoa hoja za msingi sana ambazo mtu yeyote mwenye akili timamu anatakiwa kuzingatia wakati wa kuchangia.

1) Ni kweli Nasari hakuhudhuria vikao 3 vya Bunge mfululizo? Nasari anasema alihudhuria kikao cha Novemba (ni kweli au siyo kweli?)

2) Nasari alipewa haki yake ya kwanza ya kusikilizwa? Nasary anasema siyo tu kwamba hakupewa nafasi ya kusikilizwa lakini hata kutaarifiwa kuwa amevuliwa ubunge, hajaambiwa (ni kweli au siyo kweli?

3) Ni kweli Nasary aliiandikia barua ofisi ya spika kuijulisha kuwa anauguliwa? (Ni kweli au siyo kweli?)

4) Nini tafsiri ya sheria spika anapokuwa ameandikiwa barua halafu akaacha kujibu? Maana yake amekubali, amekataa au amepuuza? Na kama amepuuza, mbunge aliyemwandikia barua atahesabikiwa hajatoa taarifa kwa spika na kupata ruhusa?
 
Kuna wakati tuliwaona akina Chenge, RA na EL hawafai. Tukawaita mafisadi lakini ukiangalia nchi inavyokwenda kwa sasa, TANZANIA BE MUCH MUCH BETTER WITH Chenge as Speaker of the House, RA Finance Manager and EL President/PM than what we have today.

Chini ya Ndugai, Bunge limepoteza hadhi na halina chochote cha kuwaonesha wananchi kama taasisi ambayo uendeshaji wake unatakiwa kuigwa na taasisi nyingine .
 
Yaani wewe ndio Job au Joni kabisa sababu unafikiri the same way wanavyofikiri, mambo ya kazi nyie mna take it personal, ulitaka ajirushe na wewe ulaya we mstue labda vigezo unavyo.

Chadema kazi kuhubiri utawala wa sheria huku hamuwezi kabisa kufuata hata tone la utawala wa sheria wala democrasia.

Hauendi bungeni miezi mitatu unajirusha na mademu Ulaya unategemea nini?.

Sheria ni msumeno

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Huyo mke wa nasari si mbunge wala mtumishi wa umma unataka kuona rufaa ya mhimbili ilikuwa iweje? Kwani anatibiwa kwa hela ya serikali?
 
Pamoja na mapungufu yake lakini Tundu Antipas Lisu ana uwezo mkubwa wa kiakili.

Bunge kama sehemu ya kutunga sheria linapaswa kuwa makini kwa kila jambo, binafsi namkubali sana mzee Chenge na yule Zungu wale Nassari wangemchukulia poa tu.

Yaani tukarudie uchaguzi kwa gharama kubwa kisa Joshua alikuwa anamuuguza mkewe so hakufika bungeni?!!

Cha ajabu huko bungeni kuna wabunge huwa wanajaza viti tu, hawajawahi kuchangia lolote zaidi ya kufukuzia posho.
 
magoiga_sn
•Follow

379 likes

magoiga_sn
Huenda ndiyo maana Nassari alipewa jina la Dogo Janja
_
Na Magoiga SN
_
Kuliandikia bunge barua ya kulitaarifu kuwa hautakuwepo ni jambo jema lakini hiyo siyo ruhusa, ibara ya 71 ya katiba na kanuni ya 147 ya kanuni za kudumu za bunge zinaeleza wazi. Unatakiwa kuwa na ruhusa ya maandishi kutoka kwa spika wa bunge husika kuhusu kutohudhuria kwakoni jambo jingine.
_
Katiba haijasema mbunge atalitaarifu bunge kuwa hatohudhuria vikao vya bunge au mikutano ya bunge, bali katiba na kanuni za kudumu za bunge ukisoma ile kanuni ya 147 imeeleza kuwa Mbunge ambaye hatahudhuria mikutano ya bunge mitatu mfululizo bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa spika moja kwa moja atapoteza ubunge wake.
_
Kama unapata shida kuelewa, pigia mstari neno BILA RUHUSA YA MAANDISHI kutoka kwa spika, kisha ujiulize.kuwa kutoa taarifa ya kutokuwepo kwako ndiyo umepewa ruhusa ya maandishi na ofisi ya spika!?? Utaelewa kuwa aidha Nassari alifanya kosa hilo kimkakati au mazoea ya kufanya mambo kwa tamaduni za 'business as usual' yamemgeuka Nassari.
_
Kwahiyo, Nassari baada ya kuandika barua alipaswa awe na barua kutoka ofisi ya spika inayompa ruhusa sasa ya kutohudhuria vikao hivyo vya mikutano ya bunge.
_
Tuache unafiki na tukubali kuwa Nassari amejichanganya kwa bahati mbaya au kimkakati, na ktk kujichanganya huko katiba na kanuni za kudumu za bunge zimemuengua 'automatically'.
_
Anyway, ukitaka kujua Nassari amecheza kete kwa akili ya juu sana kuliko akina Mtatiro, Mollel, Waitara nk, watazame wafuasi wa Chadema mitandaoni, hawajui wamtetee au wamtukane kama walivyofanya kwa wengine.
_
Magoiga SN |¦|Think Beyond The Obvious

View all 35 comments
Jamaa kawarushia fupa, hawajui waanzie wapi kulitafuna.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom