Tundu Lissu: Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri

Kama mbunge alitoa taarifa za kuuguza mke wake na bado anaadhibiwa kwa kufutiwa ubunge, basi viongozi wa nchi hii sana roho mbaya kama shetani.

Viongozi wa awamu hii wanakosaje utu kuliko wa awamu zingine zote zilizopita?

Katika awamu ambayo imeua watanzania wengi sana moja kwa moja au kwa njia nyingine tofauti ni hii ya 5.
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Eheeee!! Mbona ndio wewe umezidisha chumvi kwenye porojo zako. Kwamba barua haina tarehe ina maana hujui kusoma. Kwamba ulitaka na attachment za hospital na ugonjwa hujui hiyo ni siri?
Unamalizia kwa kusema eti porojo za TL kuwa Ubelgiji si haumwi? Kweli nadhani au wewe ni mchawi au ukoo wenu wamekuambukiza uchawi. Nikuulize hivi ungekuwa ni wewe ndiye umemiminiwa risasi zote alizomiminiwa ungekuwa unapuyanga na mdomo huo? imagine upasuaji mara 24 ameendelea kuishi wakati wengine unapasuliwa mara moja wa kupeleke chumba cha maiti. Chunga mdomo wako Mungu anakuona
 
Una ushahidi gani kuwa kafanyiwa operation 24 weka hapa source ya ushahidi wako
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Mkewe ndio ana complicatiins za uzazi, inawezekana amepewa bedrest na yupo nyumbani sio lazima awe hospitali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema kazi kuhubiri utawala wa sheria huku hamuwezi kabisa kufuata hata tone la utawala wa sheria wala democrasia.

Hauendi bungeni miezi mitatu unajirusha na mademu Ulaya unategemea nini?.

Sheria ni msumeno

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Msimshangae huyo mgonjwa hana kazi huko Belgium kwahiyo kazi yake ni hiyo,kushinda na laptop kuandika upuuzi.
Mange Kimambi na huyu hawapishani,
Tofauti ni yule aliandika udaku huyu anaandika sheria ambayo hata yy haijui anaotea.
Ni kawaida kwa majobless wote Ulaya.
 
YA JOSHUA NASSARI NA UBUNGE WAKE

Wandugu wapendwa salaam,

Nimesoma yanayomhusu Mh. Josh Nassari humu. Kuna mwelekeo mkubwa wa kukubaliana na hukumu ya Spika Ndugai kwamba Mh. Nassari hajahudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge, kwa hiyo amepata anachostahili.

Baadhi wameenda mbali zaidi na kudai Mh. Nassari 'amevuta mpunga' na kuuza jimbo. Wengine wamesema ni maandalizi ya 'kuunga mkono juhudi', n.k.

Katika yote haya, sijasikia yeyote akidai kujua upande wa Mh. Nassari mwenyewe una msimamo gani. Inaelekea tumekimbilia kwenye hukumu kutokana na maneno ya Spika na tafsiri zetu wenyewe.

Hii sio sawa sawa. Mimi nimewasiliana na Josh Nassari jana usiku. Amenitafuta mwenyewe kunitaka ushauri. Kwa maneno yake mwenyewe, hii habari ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge sio ya kweli.

Ameniambia alihudhuria vikao vya Bunge la November mwaka jana, na alisaini na kulipwa posho zake kama kawaida. 'Vikao vya Mkutano' ni pamoja na vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, kwa mujibu wa tafsiri ya neno 'kikao' katika Kanuni za Kudumu za Bunge.

Kama anayoyasema Mh. Nassari ni ya kweli, basi kuna ziada kubwa ya maneno tusiyoijua katika jambo hili. Sio sahihi kurukia kwenye hitimisho bila kusikiliza upande wake.

Pili ni kuhusu barua yake ya tarehe 29 January. Mh. Nassari ameniambia alikuwa anamuuguza mke wake ambaye alipata matatizo makubwa ya uzazi wakati anajifungua tarehe 27 January.

Siku iliyofuata, tarehe 28 (siku ya kuanza vikao vya Bunge) aliwasiliana na msaidizi wa Spika Ndugai. Akashauriwa na msaidizi huyo kumwandikia Spika Ndugai juu ya suala lake, na akafanya hivyo kesho tarehe 29 January.

Majibu ya barua ya Mh. Nassari kwa Spika Ndugai ni taarifa yake ya jana ya kumfuta Ubunge.

Sasa hapa kuna suala la tafsiri ya sheria. Je, kama ni kweli Spika Ndugai aliandikiwa barua ya kuombwa ruhusa katika mazingira hayo ya dharura na hakuijibu, hicho kimya chake kina maana gani kisheria??? Is it not the case of 'silence means consent' here???

Jambo la tatu ni la utaratibu wa uamuzi wenyewe. Spika Ndugai hajamuandikia au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na Mh. Nassari ili kumjulisha juu ya hatua anazotaka kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.

Ni kweli kwamba ibara ya 71 ya Katiba haijaweka utaratibu wa Spika kumwandikia au kumjulisha Mbunge juu ya hatua anazopanga kumchukulia kwa kutohudhuria mikutano ya Bunge.

Je, ukimya huo wa Katiba una maana Spika Ndugai hawajibiki na hakuwajibika kumjulisha Mh. Nassari kabla ya kumfuta Ubunge???

Hili ni suala lingine la tafsiri ya sheria. 'Natural justice', misingi ya haki ya asili, inamtaka mtoa maamuzi yeyote yanayoweza kuathiri haki ya mtu mwingine, kumpa mtu huyo fursa ya kujitetea kabla ya uamuzi utakaomwathiri kutolewa.

Masharti haya ya haki ya asili ni ya lazima hata pale ambapo sheria haijaweka utaratibu huo. 'Audi alteram partem', 'sikiliza upande mwingine.' Huo ndio msimamo wa kisheria wa Tanzania hii.

La mwisho ni huu utaratibu wa Spika Ndugai kuwasiliana na mitandao ya kijamii au hadharani badala ya kuwasiliana kwanza na Mbunge anayehusika kwanza.

Mh. Nassari ameniambia amesikia taarifa za kufutwa Ubunge wake mitandaoni kama wewe na mimi. Na mimi nilisikia habari ya kufutiwa mshahara na posho za kibunge mitandaoni.

Je, huu ni utaratibu sahihi wa Spika wa Bunge kuwasiliana na Wabunge kuhusu masuala yao ya kibunge???

Yote haya ni masuala muhimu kuyaangalia kabla ya kukimbilia kwenye hukumu kwamba Mh. Nassari 'ameuza Jimbo', au amekosea, n.k.

Tutayajua mengi sana endapo Mh. Nassari atafungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kufutiwa Ubunge, kama ambavyo nimemshauri. Tuvute subira.

Tundu Lissu, MB
Tienen, Ubelgiji
'
Duh wewe baba hatari..sasa nimeelewa kwanini kuna aina mbili za mawakili yaani "wakili msomi" na "wakili"..Kwa haya maandishi yako "hakimu yoyote hata awe kilaza kama yule "Mashauri" wa kisutu akimaliza kusoma huu waraka mfupi haitaji kuangalia mara mbili atatoa hukumu hapohapo "in favour of Nassari" na sidhani kama kuna wakili mwenye akili timamu kutoka serikalini anaweza kukubali kwenda mahakamani kumpinga Nassari kama akiyapanga maelezo kama ulivyoyaweka ..labda huyo awe ametoka kwenye kundi lile la mawakili ambao wanapinga dhamana ya Mbowe na matiku hadi leo...kwa ufupi hii paragraph pekee inawatosha kuwamaliza mahakamani.."Hili ni suala lingine la tafsiri ya sheria. 'Natural justice', misingi ya haki ya asili, inamtaka mtoa maamuzi yeyote yanayoweza kuathiri haki ya mtu mwingine, kumpa mtu huyo fursa ya kujitetea kabla ya uamuzi utakaomwathiri kutolewa"
 
Anaeleweka Vipi? Nassari barua yake hata haionyeshi yuko hospital gani Wala ushahidi wa refferal toka hospital ya muhimbili porojo tu Kama za Lisu Niko ubelgiji kwa matibabu hamna ushahidi wa refferal porojo tu
Sasa Unataka vyeti vya hospitali au referral aambatanishe kwenye barua huko uliko ndo ukiandika barua unaandika na unavyoondoka, hospitali uliyopo na wodi ndo barua ya hudhuru inavyotakika?? Hizo reference zingine kuhusu uthibitisho kama kweli akifungua kesi atavileta mahakamani na siyo mitandaoni japo kuwa mm siamini kama kweli Nasari hajawachezea wenzie ngoma ya ukae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimshangae huyo mgonjwa hana kazi huko Belgium kwahiyo kazi yake ni hiyo,kushinda na laptop kuandika upuuzi.
Mange Kimambi na huyu hawapishani,
Tofauti ni yule aliandika udaku huyu anaandika sheria ambayo hata yy haijui anaotea.
Ni kawaida kwa majobless wote Ulaya.
Kwa Sheria za kazi mgonjwa mwenye ED hatakiwi kufanya kazi Lisu anachapa kazi Kama kawaida kitu inayoonyesha wazi ni mzima wa Afya anayeendelea na kazi zake za kisiasa Kama kawaida huku akipunga upepo wa ubelgiji na akipenda tour anaenda zake London na Amerika kisha anarudi tena ubelgiji
 
ha

kuna mtu makini kama ndugai anafuata sheria vizuri sana tangu suala la lisu mpaka huyu nasari sasa nyie hebu fikiria katiba inasema mbunge asipohuzuria viakao vitatu mfululizo amekosa sifa ya kuwa mbunge hapa lisu anatuambia kwanini hakumtafuta nasari amwambie hatua atakayo mchukulia kwani kwenye katba kunakipengele kinaeleza hivyo? sasa awe anambembeleza kwa lipi?/ huoni kama ni upumbavu namba moja anaomshauri huyu dogo aliye uza jimbo kirahisi huyu ameunga mkono juhudi wala hakuna kingine subiri muone kama ataenda mahakamani

Sheria za kazi zinasema usipohudhuria kazini kwa siku tano mfululizo utafukuzwa kazi, is it automatic kwamba ukiibuka siku ya sita unakutana na barua ya kufukuzwa kazi? Si ni lazima usikilizwe kwanza?
 
tatizo sheria au katiba haijaweka wazi kama kunautaratibu wa kukusikiliza yenyewe inasema ukifulluliza kutega mara tatu basi umekosa sifa labda wafanyie marekebisho hapo lakini tayari nasari ameshakosa sifa si mbunge hata aende mahakamani
 
Kama mbunge alitoa taarifa za kuuguza mke wake na bado anaadhibiwa kwa kufutiwa ubunge, basi viongozi wa nchi hii sana roho mbaya kama shetani.

Viongozi wa awamu hii wanakosaje utu kuliko wa awamu zingine zote zilizopita?

Katika awamu ambayo imeua watanzania wengi sana moja kwa moja au kwa njia nyingine tofauti ni hii ya 5.

Hivi wanatakiwa kutoa taarifa au wanatakiwa kuomba ruhusa ???...tuelimishwe hapa...
 
Back
Top Bottom