Tundu Lissu: Tutathmini kazi tuliyoifanya na matokeo tuliyoyapata. Tupate mafundisho sahihi ya kazi

Anaandika Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu.

Waheshimiwa na makamanda poleni kwa mapambano na hongereni kwa kazi kubwa mliyoifanya kwenye chaguzi hizi. Naona kila mmoja wetu anasikitika jinsi matokeo ambavyo yamekuwa tofauti na matarajio yetu na kazi tuliyoifanya.

Ni rahisi, katika mazingira haya ya kushindwa na kabla vumbi halijaisha, kuanza kulalamika, kunyoosheana vidole na kukatishana tamaa. Hii haitusaidii sana. Badala yake, tunachohitaji zaidi ni 'brainstorming' kuliko 'blamestorming.' Naomba nifanye ya kwanza. Chaguzi ndogo za ubunge au udiwani ni ngumu sana kushinda katika mazingira halisi ya nchi yetu.

Mifano michache inathibitisha ukweli huu. Katika election cycle ya '05-'10, tulishinda Jimbo la Tarime lakini tukapigwa Biharamulo Magharibi na Busanda. Tarime lilikuwa Jimbo letu tangu Uchaguzi Mkuu wa '05, Busanda lilikuwa la maCCM na Biharamulo Magharibi lilikuwa la TLP. Sikumbuki vizuri kama tulishinda Kata hata moja katika mzunguko wa uchaguzi wa kipindi hicho.

Katika election cycle ya '10-'15, tulipigwa Igunga licha ya kazi kubwa tuliyofanya, lakini tukashinda Arumeru Mashariki iliyokuwa chini ya maCCM. Vile vile tulishindwa Kalenga, Chalinze na Ulanga Magharibi yaliyokuwa ya maCCM tangu Uchaguzi Mkuu wa '10.

Kwenye chaguzi za Kata za '12 kama mnakumbuka, licha ya kazi kubwa na rasilimali nyingi, tulipata Kata tatu tu kati ya 26 zilizokuwa zinagombaniwa. Ukiachia Ifakara Mjini ya Mh. Juakali, Kata nyingine mbili - Kiboriloni na Iseke - zilikuwa zetu tangu Uchaguzi Mkuu wa '10.

Kwa mantiki hii, matokeo ya jana sio ya kushangaza sana. Kata ya Duru ilikuwa ya kwetu na tumeitetea, nyingine zote tulikopigwa zilikuwa za maCCM. Hatujanyang'anywa iliyokuwa yetu, hatujanyakua zilizokuwa zao. Hata hivyo, funzo kubwa zaidi la historia ya chaguzi hizi ni hili hapa: licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo hizi, tumeendelea kufanya vizuri zaidi katika kila Uchaguzi Mkuu uliofuatia kipigo cha chaguzi ndogo.

Mwaka '10 tulifanya vizuri zaidi licha ya kupigwa Busanda na Biharamulo Magharibi katika mzunguko wa '05-'10. In fact, tulichukua Jimbo la Biharamulo Magharibi mwaka huo. Na tulipata Kata nyingi zaidi '10 kuliko ilivyokuwa '05. Mwaka '15 tulipata ushindi mkubwa zaidi katika Kata na majimbo licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo za mzunguko wa '10-'15.

Hoja yangu hapa ni kwamba uchaguzi wa marudio hauna direct and negative bearing kwenye matokeo yetu ya Uchaguzi Mkuu unaofuatia. On the contrary, uchaguzi wa marudio unatupa fursa ya kupanda mbegu ambayo, ikitunzwa vizuri, inakuwa na mazao bora kwenye chaguzi zinazofuatia.

Kwa upande mwingine, chaguzi za marudio - kwa sababu ya udogo au uchache wa maeneo yanayogombaniwa - yanawapa maCCM fursa ya kutumia nguvu kubwa za rasilimali na za kidola ukilinganisha na tunazotumia sisi. Kwenye Uchaguzi Mkuu unaofuatia, nguvu hizo zinasambazwa nchi nzima na kwa hiyo effectiveness yake inapungua.

Ndio maana tumefanya vizuri zaidi kwenye Uchaguzi Mkuu kuliko kwenye chaguzi ndogo za marudio. Hili, kwa maoni yangu, ndilo fundisho kuu la chaguzi hizi za marudio. Hatuna sababu kubwa ya kushangilia kutokana na matokeo ya jana. Hata hivyo, hatuna sababu yoyote ya kuomboleza pia. Obviously, maCCM na wapambe wao wataandika 'wasifu wa marehemu' wa CHADEMA/UKAWA na kuutangaza dunia nzima na kwa sauti kubwa. Hilo lisitupofushe macho yetu, hata kama linakera sana.

Tutathmini kazi tuliyoifanya na matokeo tuliyoyapata. Tupate mafundisho sahihi ya kazi hiyo na matokeo yake. Tutumie mafundisho hayo kwa kujipanga vizuri zaidi kwa ajili ya 'the real prize': 2020.
Uchambuzi wa Mh. Lissu ni unatoa dira na mwelekeo wa uchaguzi wa 2020. Kwa weledi na uzoefu wake katika siasa za Tanzania na chaguzi zake na baada ya UKAWA factor Mh Lissu angetoa uchambuzi kuhusu maeneo yafuatayo
1. Ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA namna vilivyoshurikiana katika uchaguzi huu hasa kuachiana Kata (Nani alimwachia mwezeka kata na matokeo halikuwa je)
2. Kulikuwa na ushuriakiano wa kimkakati au chama x akiachiwa kata basi y,x na t hawajishirikishi)?
3. Kwenye uchaguzi wa 2012 wa kata 26 CHADEMA ilipata kura 03 sawa na 11.5%. Kwenye uchaguzi huu CHADEMA kimepata Kata 01kati ya 20 sawa na 5%. kitakwimu imeshuka. Inahitajiwa "postmortem" ya kina kuangalia wapi chama kilijikwa na sio kilioangukia? Kama matokeo haya ni "litmus test" they do not speak well for the Party
4. Nguvu ya UKAWA iko imara kama 2015 au imepanda ni heri lakini kama imeshuka shughulikieni "killer assumptions zake"
5. Chama kitaenda kwenye uchaguzi wa chma na serikali za mitaa ikiwa na nguvu ya pamoja kama 2015 au itakuwa na makovu na maumivu ya uchaguzi mdogo wa 2017?
 
Uchambuzi wa Mh. Lissu ni unatoa dira na mwelekeo wa uchaguzi wa 2020. Kwa weledi na uzoefu wake katika siasa za Tanzania na chaguzi zake na baada ya UKAWA factor Mh Lissu angetoa uchambuzi kuhusu maeneo yafuatayo
1. Ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA namna vilivyoshurikiana katika uchaguzi huu hasa kuachiana Kata (Nani alimwachia mwezeka kata na matokeo halikuwa je)
2. Kulikuwa na ushuriakiano wa kimkakati au chama x akiachiwa kata basi y,x na t hawajishirikishi)?
3. Kwenye uchaguzi wa 2012 wa kata 26 CHADEMA ilipata kura 03 sawa na 11.5%. Kwenye uchaguzi huu CHADEMA kimepata Kata 01kati ya 20 sawa na 5%. kitakwimu imeshuka. Inahitajiwa "postmortem" ya kina kuangalia wapi chama kilijikwa na sio kilioangukia? Kama matokeo haya ni "litmus test" they do not speak well for the Party
4. Nguvu ya UKAWA iko imara kama 2015 au imepanda ni heri lakini kama imeshuka shughulikieni "killer assumptions zake"
5. Chama kitaenda kwenye uchaguzi wa chma na serikali za mitaa ikiwa na nguvu ya pamoja kama 2015 au itakuwa na makovu na maumivu ya uchaguzi mdogo wa 2017?
Hiyo 2020 bado ni uendawazimu kuingia kwenye uchaguzi bila kurekebisha mambo ya msingi, la sivyo unapoteza jimbo waziwazi kama Kafulila David huku ukiwa na matokeo halali lakini sheria inatambua 'mtangaza matokeo'.
Kama Mh. TL anapita hapa nadhani ingekuwa vizuri akatupa ufafanuzi kama ile kesi iliyotupwa na DPP juu ya wale vijana waliokuwa wanafanya tallying ya matokeo ya 2015 inaweza 'kutafutiwa mwelekeo' mwingine tofauti ili isikilizwe mpaka mwisho. Hii itatusaidia sana kujua kuwa wale vijana walikuwa na makosa au la mpaka tukaju kilichopelekea kuwekwa ndani zaidi ya masaa 48 bila dhamana.
Nimetoa rejeo hili kwa maana uchaguzi uliopita Uganda ulikuwa na mazingira ya aina hii lakini M7 'akawazidi' ujanja akina Besigye, huko Ghana 2016 nusura nao wapigwe changa la macho lakini wakakomaa wakisaidiwa na sheria zao ambazo ziko wazi kuzidi zetu na mwishoni tumeona Gambia. Issue ya Gambia hata kabla ya ECOWAS kuingilia wananchi wenyewe walikuwa tayari (wajanja) kuonyesha ulimwengu kuwa Adama Barrow kashinda, mbali na hapo ni ngumu jumuia za kikanda na kimataifa kukusaidia kama huna cha kukusaidia kuonyesha ushindi wako!
 
Nadhani zile propaganda za CCM na serikali yake inachukiwa mno kuliko awamu iliyoisha zimekufa rasmi.

Mbowe&Co hawawezi kuupeleka huu upinzani zaidi ya hapo walipoufikisha sababu hata uwezo wa kufikiri umeshagota.

Matukio yanayoendelea huko yanaonesha kwamba wako kwenye omega,imagine watu wazima wanahamasishana kutupa line kwa jambo la kijinga kama lile na inakuwa agenda au mhuni mmoja anajificha ili chama kipate cha kuongea.

Watakachokuwa wanakifanya kwa sasa ni kuhakikisha hakuna chama kingine cha upinzani kinaibuka na kuwa na nguvu zaidi yao ili waendelee kuwa chama kikuu cha upinzani.

Hata ACT ikianza kuimarika wataungana nayo ili kuidhibiti.
 
Mtaangaika sana mlioaminishwa neno tume huru-hizo nafasi za ubunge, udiwani na serikali za mtaa ni tume ipi iliwatangaza? tuwe wazi upinzani wa tz ni wa maigizo na wa kuvizia-kama huna maandalizi hata ya mgombea wa nafasi ya uraisi-je tume kosa lake ni lipi? wakiacha kupiga harakati naamini mambo yao yatanyooka vizuri na kama wataendelea kupiga harakati, hata wakipewa tume huru-bado watakwambia si huru sana.
 
Yani kwa jinsi ilivyo ata itokeee CCM kashinda kwa kura 99 kwa 100 kura yangu itakuwa iyo Moja , pia nashukuru family yangu nayo haijawai kuipa kura CCM. wao washinde tu kwangu hawapati kura yangu
 
Back
Top Bottom