Tundu Lissu: Tutanyolewa bila maji suala la mchanga wa madini, tusikurupuke

Tundu lisu tatizo kajiweka ku critisize kila kitokacho chama tawala hata kama kina tija.kwa hili lissu umekengeuka hata kama ni gwij wa sheria jaribu kupitia hiz allegations za serikal na mikataba tulioingia na hawa watu waliokosa intergrit
 
Jamani Serikali haijanyang'anya mali ya muwekezaji yeyote, serikali ilisimamisha usafirishaji ili uchunguzi wa kilichomo ufanyike, wawekezaji wenyewe walikubaliana na hilo wakidai ni vema ukweli ujulikane. Maneno ya serikali imenyeng'anya mali za wawekezaji yanatoka wapi?

Wawekezaji wameonyeshwa ukweli, WALIKUWA WANATUDANGANYA sasa ni hatua. Walilpe au waache
 
Lissu hana JIPYA
Hata walipokua wanatoka bungeni kupinga miswada ya madini na gas kuingia kwa hati ya dharula, mliwabeza na kuwatukana.

Leo hii mnawaona mashujaa walioshiriki kupitisha hiyo miswada.

Kamwe hatutayafikia maendeleo ya kweli kwa akili kama zako za kuamini kila wasemacho usiowapenda ni kibaya. Ila kumbuka nao ni watanzania kama wewe na huenda wanalitumikia taifa kukuzidi wewe
 
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu

Huyu na mikataba yake, wamempa Rushwa ili ajaribu kuitisha Serikali. HATUTISHIKI.
 
Tundu lisu ni tobo haelewi lolote. Akina prof kabudi wameshaliona na kumshauri vyema jpm. Halafu anapaswa kujua kuwa kudeclare kiasi tofauti kilichomo ndani ya mchanga ni kuvunja mkataba automatically. Mi niliwaambia tundu lisu ni mweupe Wa Sheri anashindaga vi case vya kitoto sana.
Hata hili anatetea wezi mana ingekuwa yeye angeshindwa mchana kweupe mana anaona maluweluwe. Kilaza.
Mbona husemi hicho walichomshauri maana ushauri wa Lissu tunauona
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu

Kusoma na kuelewa huwezi, kuona na kusikia nako ni shida mkubwa ?

Lissu hajapinga lolote, ila ametahadharisha kuwa kinachofanyika ni sawa na hakuna unless itanguliwe kwanza na....

Kitu ambacho hata Lissu japo hajasema japo ndivyo ilivyo ni kuwa, hatuwezi kujichomoa huko !!!

Na ili ionekane tuko serious kweli, basi tuanze kujitoa kwanza kwenye mikataba hiyo kimataifa tuliyosaini kama nchi....

Lakini kinachofanyika sasa ni purely polictical gimmicks kwenye ishu ambayo ina sura ya kimataifa......

Nina hakika, akina Jakaya Kikwete na Ben Mkapa wanamsikilizia jamaa anavyojaribu kuparangana kisha wauone mwisho wake... I am sure wanatazama na kutikisa vichwa tu......

Ishu ya Zimbabwe na mashamba ya walowezi wazungu iko quite different na hii ishu yetu mkubwa, amka acha kupotosha huku ukiwa umelala uongozi wa kukosa ufahamu...!!

Na Lissu yuko précicely clear kwa kusema "....tutanyolewa bila hata maji.... ", kwa sbb cha mtoto IPTL, Songas na Richmond tu ilishashinda na kutunyoa kisawasawa huku tukigugumilia maumivu...

Na, I think, laiti Magufuli angeanza kwanza kwa kuvunja mikataba ya kinyonyaji ya ufuaji umeme ya hivi vikampuni vidogo i. e Richmond a. k. a Symbion, Songas na IPTL ningemuona mwanaume.....

Lakini kaparamia eneo gumu mno, hakika ajindae kuingiza kichwa kwenye oven tunyolewe bila maji......
Kujitoa ni wazo zuri tu lakini nalo pia linamadhara yaleyale. Maana mikataba hiyo ipo kulinda maslahi yao wazungu. hivyo hawawezi kukubari kirahisi kujitoa lazima walete zengwe la kuwekewa vikwazo, kukata misaada et al. Either ways, being Lissu's approach or magufuli's will bring us consequences
 
Tatizo ni kuwa kwasasa kama ukitoa mawazo ya kitaaluma na kitaalamu juu ya hili utaonekana sio mzalendo, na hasa pale unapoonyesha kuwa lazima tuwe makini wakati wa kuwashughulikia hawa wawekezaji. Anyway, ngoja tuone.
 
Kujitoa ni wazo zuri tu lakini nalo pia linamadhara yaleyale. Maana mikataba hiyo ipo kulinda maslahi yao wazungu. hivyo hawawezi kukubari kirahisi kujitoa lazima walete zengwe la kuwekewa vikwazo, kukata misaada et al. Either ways, being Lissu's approach or magufuli's will bring us consequences

Na hii ndiyo logic behind ya Tundu Lissu's comments.....

Kwamba, either this way or that, kote Magufuli atanyolewa bila maji !!
 
Usiogope kuitwa majina mkubwa, wewe ongea kile unachokiamini, baaaasi.....

Si yeye mwenyewe Magufuli na CCM yake ndiyo hasa chanzo cha matatizo haya bwana ?.....

Waache unafiki wa kuliakulia hapa wakati "Dude"walilisimika wenyewe na sasa wanajifanya hamnazo eti.....

Do not afraid, speak up your mind !!!
 
Kwa hiyo hawa wezentu ina maana wanataka tusifanye lolote kwa sababu ya kuogopa kuchukuliwa hatua na wakubwa? Kama tunatiwa vidole machoni tuendelee kukodoa tu kwa sababu tulisema wanaruhusa kucheza usoni!?
 
Na hii ndiyo logic behind ya Tundu Lissu's comments.....

Kwamba, either this way or that, kote Magufuli atanyolewa bila maji !!
Akinyolewa magufuli bila maji, madhara Yake yatasambaa kwa watanzania wote, na hivyo wote tutakuwa tumenyolewa bila maji. Kama tunaogopa kunyolewa bila maji basi tuwaache waendelee kutuibia na kila mtanzania aufyete.
 
Kazi yetu ni moja tu, tutamwambia kuwa tulikuambia na kukuonya lakini ukajifanya mjuaji, baasi !!
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
Ujifunze kupembua vitu vizuri unakurupuka tu kama Rais wako.. Subiri uone jtatu wanafungua kesi mahakama ya, biashara.. Swali la kwanza wameuliza maabara zilizotunika ziko cerfified kimataifa kufanya hiyo kazi? Tayari gumi la pua round ya, kwanza tu..
 
mimi ni mpinzania kwa hili nampongeza Raisi Magu. Lakini pia,nathani tunakuwa wepesi sana kusema wao watafanya hili na lile kwa vitisho. Ikumbukwr hatukukubaliana kuuza nchi namna hii.
Huu ni wakati wa kulinda nchi na kuachana na ushenzi uliokuwa unafanywa na watu wachache.
Labda nimkumbushe Lissu kuwa ni bora tumwage ugali tuone bei ya gold itakavyokuwa na makampuni watakaona kuwa wanataka kufanya kazi nasi watakuja hapa,lakni sio kuwaogopa wazungu. They can go to hell.
 
Back
Top Bottom