Tundu Lissu: Tutanyolewa bila maji suala la mchanga wa madini, tusikurupuke

Hivi tunafahamu lissu ame specialize katika nini???Ninavyojua lissu alifanya utafiti katika mgodi wa Bulyankulu miaka ya 1996 na kuwahi kufunguliwa kesi akitetea wachimbaji wadogo waliodhaniwa kufukiwa wakiwa hai ili mwekezaji apewe mgodi. Eneo hili alilifanyia kazi vya kutosha kabla ya kuendelea kufanya kazi marekani, akiendelea na tafiti za namna hii.Kwa hiyo Lissu anafahamu hii mikataba ya madini na consequences zake kisheria
That has nothing to do with contract law for all you know based on the activities explained labda alikuwa human right lawyer.

Lissu kwenda marekani kusomea anachojua sio jambo la kushangaza the guy has been everywhere mimi nishawahi kumuona kwenye BBC documentary for their UK audience akiwa kijana kama mtaalamu wa mambo ya asili na somo la ukoloni tena alitoa somo zuri kuhusu mambo ya mbuga za wanyama na geography yake.

Lakini linapokuja swala la knowledge or expert opinion kinachoangaliwa is how valid is the argument principally; sasa hapo mtu awe na Phd awe na nini kama na wewe unazijua you can apply them to evaluate his argument. Nadhani ndio hapa kama jamii elimu inatupiga chenga utakuta mtu ana quote tu maneno ya mtu au kitabu alichosoma as if the person has unquestioned authority.

In short anachoongea lissu hapo ni aspect ndogo sana ya mkataba kwenye kuweza kuuvunja principally.
 
Kwani amevunja mkataba. Pili huoni makonda alivyookoa vijana wengi dhidi ya madawa kwa approach hiyo hiyo uliyoana mbaya kwa mtazamo wako.hivi unajua kama dutete rais Wa ufilipino anaua kabisa?
Kwa akili kama za kina Lissu Magufuli angemuazima Durtete kwa mwezi mmoja masaidie kusafisha hizi takataka.
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.

Wizara, taasisi na wakala kadhaa za serikali ndo wanazibariki hizo data..
Funguka akili.. Think outside and behind beyond the box!
 
Hata vichaa huwa wanakumbuka kipindi kabla hawajawehuka!! Tundu Mughwayi Antipas Lissu South Africa ya Zuma anatandikiwa zulia jekundu kwa heshima ya mwanasheria bora africa: Haya google -@tunduantipaslissu
Kwani hayo maelezo huko Google anaweka roho mtakatifu?
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.

..Lisu anamaanisha kua Tanzania itashtakiwa ktk mahakama ambapo zitawapendelea Akashia ...
 
issue ni....je, ni chombo gani independent kimeleta hizo findings? in the context of international commercial contracts, ile kamati ya Rais haina credibility yoyote kwani iliteuliwa kwa 100% na serekali ambao ni upande mmoja tu wa mkataba (aka mlalamikaji).

kwa taarifa yako, zile findings za ile kamati ziko technically skewed (wale wataalamu wa statistical computations mtanielewa).
Sawa!
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.

Hapo ni mpaka uprove kuwa walikuwa wanapewa taarifa Fulani ya Lab lakini wao wanaibadirisha kisha wanaficha baadhi ya Taarifa!. Otherwise wakienda mahakamani, ni lazima Lab huru itajayokubalika na pande zote itatafutwa ili kucomfirm findings za pande zote mbili!
 
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu

Huyu jamaa kila kitu ni kupinga tu eti kwa sababu ni upinzani.

Moja: kama hiyo MIGA iko chini ya bank ya dunia, unadhani Tanzania kama engeenda kujiondoa kwanza ingebaki salama?. Kwa kujiondoa huko, hata hawa ACACIA wasingekuwa na mashiko ya kisheria kuendeleza shughuli zao hapa nchini na hivyo hawa jamaa wangetuwekea vikwazo tu.

Pili: kama tukijitoa kwenye hizi bilateral agreements tutabaki salama kiuchumi? Jibu ni hapana

In either ways as long as tuliingizwa mkenge tangu 1998 tungesafa tu.

Tuna mambo mawili tu yakuchagua, aidha tuwaache waendelee kutunyonya au tuchukue actions ambazo tunaona Zitatetea rasilimali zetu zisiibiwe tena.

Robert Mugabe alijaribu, akawatimua wazungu huko Zimbabwe, aliwekewa vikwazo, sawa watu wamepata shida ktk kipindi cha mpito na sijasikia kwamba wananchi wa nchi hiyo wamepatwa na kitu cha ajabu sana kivile baada ya maamuzi hayo.
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
Taratibu zinaongizwa na kanuni , ambazo mawaziri wajiwekea na zilikuwa zinatumika.mm nimesafirisha sana shaba ufi, kikanuni ulikuwa unadeckre unachosafirisha na si kila element, inayolipiwa mrabaha ilikuwa ni unachosafirisha, na ndo mawaziri wote na mamishina wa madini walikuwa wakizingatia.
Hivyo kama ni kulifabya liwe kisa tubadirishe kanuni na taratibu na si hivi ilivyo sasa.
 
Lissu huyuhuyu wa mwembeyanga na list of shame au mwingine?!!!
Eee,halafu anajiita mwanasheria msomi,sasa yeye badala ya kutoa mawazo ya nini,kifanyike baada ya kukamata mwizi,ili turudishiwe mali yetu,yeye amekazania kutu tisha tu.
Je alitaka tusikamate,?Au na yeye kashahongwa?.
Huyu jamaa mweupe kwelikweli,
anaTetea kuibwa?
mbona tulipopopigwa rada
baadae serikari yao wenyewe walitudishia chenji?
Acha kushindana na akili kubwa, halafu acha kuharibu majina ya watu kwa kuwa unatumia jina bandia. Mh Lissu ni mbunge, ni mbobezi wa sheria, anapotoa ushahuri kwa serikali wewe nyang'au unaelipwa buku 7 unaleta mafi yako hapa ***** zako.
we mbobezi hani huyo.
Mwambie aonyeshe .paper alilo tunga yeye.
 
Hivi huyo lissu anaweza,hata kugusa elimu ya profesa kabudi?
Nchi ipo kwenye vita yeye bado analets mambo ya kichama chama hspa?
kwani yeye kama mbunge di aende
kwa wenzake atoe maoni na ushauri maalum kuliko kututisha. hapa
 
HII NI VITA KATI YA TANZANIA NA MWEKEZAJI.
TUNDU LISSU NI ASKARI WA TANZANIA. KWA SABABU NI NI MIONGONI MWA WAPIGANAJI WAZURI NA HODARI WALIYEKO UPINZANI AWEKWE MSTARI WA MBELE KATIKA VITA HII.
TUNAMWOMBA RAIS AREJEE MISAHAFU.
HAPO ZAMANI KATIKA INCHI YA MISRI KULIKUWA NA MFUNGWA MOJA MWIISRAEL ALIYEITWA YUSUFU.
FARAO ALIOTA NDOTO AMBAYO HAKUWEZA KUITAFASIRI. WASHAURI WAKE WAKAMWAMBIA KULE GEREZANI KUNA MFUNGWA ANAITWA YUSUFU AMBAYE ANAWEZA KUTAFASIRI HII NDOTO.
FARAO ALIMTOA YUSUFU NA AKATAFASIRI HIYO NDOTO KUWA KUTAKUWA NA MIAKA SABA YA MAVUNO MENGI NA BAADAYE KUTAKUWA NA MIAKA SABA YA NJAA.
FARAO ALIAGIZA YUSUFU ATOLEWE GEREZANI, AKAMTEUA KUWA WAZIRI MKUU ILI AKUSANYE CHAKULA KWA MIAKA SABA YA SHIBE ILI KITUMIKE MIAKA MINGINE SABA YA NJAA.
HUYU YUSUFU HAKUWA MTU WA MISRI LAKINI KWA SABABU YA SHIDA FARAO ALIANGALIA TATIZO ZAIDI KULIKO MFUNGWA AU KABILA AU URAI AU DINI AU RANGI.
RAIS, HII NI VITA KAMA VITA ZINGINE KUSANYA MAJESHI BILA KUJALI CHAMA, DINI, KABILA AU RANGI ILI TUWEZE KUSHINDA AU KUMWAGA DAMU KIDOGO.
KAMA ULIVYOUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI, UNDA KAMATI YA KUTAFUTA SULUHISHO NA USHINDI.
 
Huyu jamaa kila kitu ni kupinga tu eti kwa sababu ni upinzani.

Moja: kama hiyo MIGA iko chini ya bank ya dunia, unadhani Tanzania kama engeenda kujiondoa kwanza ingebaki salama?. Kwa kujiondoa huko, hata hawa ACACIA wasingekuwa na mashiko ya kisheria kuendeleza shughuli zao hapa nchini na hivyo hawa jamaa wangetuwekea vikwazo tu.

Pili: kama tukijitoa kwenye hizi bilateral agreements tutabaki salama kiuchumi? Jibu ni hapana

In either ways as long as tuliingizwa mkenge tangu 1998 tungesafa tu.

Tuna mambo mawili tu yakuchagua, aidha tuwaache waendelee kutunyonya au tuchukue actions ambazo tunaona Zitatetea rasilimali zetu zisiibiwe tena.

Robert Mugabe alijaribu, akawatimua wazungu huko Zimbabwe, aliwekewa vikwazo, sawa watu wamepata shida ktk kipindi cha mpito na sijasikia kwamba wananchi wa nchi hiyo wamepatwa na kitu cha ajabu sana kivile baada ya maamuzi hayo.

Kusoma na kuelewa huwezi, kuona na kusikia nako ni shida mkubwa ?

Lissu hajapinga lolote, ila ametahadharisha kuwa kinachofanyika ni sawa na hakuna unless itanguliwe kwanza na....

Kitu ambacho hata Lissu japo hajasema japo ndivyo ilivyo ni kuwa, hatuwezi kujichomoa huko !!!

Na ili ionekane tuko serious kweli, basi tuanze kujitoa kwanza kwenye mikataba hiyo kimataifa tuliyosaini kama nchi....

Lakini kinachofanyika sasa ni purely polictical gimmicks kwenye ishu ambayo ina sura ya kimataifa......

Nina hakika, akina Jakaya Kikwete na Ben Mkapa wanamsikilizia jamaa anavyojaribu kuparangana kisha wauone mwisho wake... I am sure wanatazama na kutikisa vichwa tu......

Ishu ya Zimbabwe na mashamba ya walowezi wazungu iko quite different na hii ishu yetu mkubwa, amka acha kupotosha huku ukiwa umelala uongozi wa kukosa ufahamu...!!

Na Lissu yuko précicely clear kwa kusema "....tutanyolewa bila hata maji.... ", kwa sbb cha mtoto IPTL, Songas na Richmond tu ilishashinda na kutunyoa kisawasawa huku tukigugumilia maumivu...

Na, I think, laiti Magufuli angeanza kwanza kwa kuvunja mikataba ya kinyonyaji ya ufuaji umeme ya hivi vikampuni vidogo i. e Richmond a. k. a Symbion, Songas na IPTL ningemuona mwanaume.....

Lakini kaparamia eneo gumu mno, hakika ajindae kuingiza kichwa kwenye oven tunyolewe bila maji......
 
subiri matokeo,au umesahau sakata la samaki tuliwalipa kiasi gan wale jamAaa...no research no right to speak.
Nafikiri tatizo ni competent lawyers. Meli imeshikwa katika eneo letu la bahari bila kibali akina "Lissu wetu" (wanasheria) wameshidwa kujenga hoja wahalifu wameachiwa. Kama unavyoona, makontena ya mchanga yameshikwa kwa kuhisiwa na baadae kuthibitika kuwa na kiwango tofauti na kile kilichoelezwa. Sasa kamanda wetu, Rais wa TLS kesha shindwa kesi nje ya mahakama kwa kigezo kuwa mwizi ni mtoto wa tajiri na anaona kheri hayo makontena yaendelee kusafirishwa mpaka hapo mikataba itakapolekebishwa. Sikubaliani na hilo. Hapa ni suala la wizi ambalo acacia wao wanadai hawajaiba. Kama wakina Lissu wetu hawawezi kulitetea hilo kwenye hiyo mahakama ya kimataifa mimi sikubali serikali ikubali kuyaachia hayo makontena. Kama serikali imejiridhisha kuwa acacia wameforge, ikomae na hayo makontena. Nyerere alitaifisha mabenki makubwa ya kimataifa, majumba ya jumuia kubwa duniani ya H.H. The Aga Khan na hatukusikia Mtanzania au vyombo vya Tanzania kupigwa marufuku Ulaya, sasa ndio tumshauri Rais wetu aufyate kwa hili la wizi wa mchana kweupe kisa mwizi ni mtoto wa mataifa makubwa. Cowardness.
 
Kaswali kadogo kwa mwanasheria TL, huo mkataba wa MICA unamlinda muwekezaji mwenye tuhuma za kutokuwa mwaminifu/ tuhuma za udanganyifu? Hilo tu.

Na washawasha!​
 
Nafikiri tatizo ni competent lawyers. Meli imeshikwa katika eneo letu la bahari bila kibali akina "Lissu wetu" (wanasheria) wameshidwa kujenga hoja wahalifu wameachiwa. Kama unavyoona, makontena ya mchanga yameshikwa kwa kuhisiwa na baadae kuthibitika kuwa na kiwango tofauti na kile kilichoelezwa. Sasa kamanda wetu, Rais wa TLS kesha shindwa kesi nje ya mahakama kwa kigezo kuwa mwizi ni mtoto wa tajiri na anaona kheri hayo makontena yaendelee kusafirishwa mpaka hapo mikataba itakapolekebishwa. Sikubaliani na hilo. Hapa ni suala la wizi ambalo acacia wao wanadai hawajaiba. Kama wakina Lissu wetu hawawezi kulitetea hilo kwenye hiyo mahakama ya kimataifa mimi sikubali serikali ikubali kuyaachia hayo makontena. Kama serikali imejiridhisha kuwa acacia wameforge, ikomae na hayo makontena. Nyerere alitaifisha mabenki makubwa ya kimataifa, majumba ya jumuia kubwa duniani ya H.H. The Aga Khan na hatukusikia Mtanzania au vyombo vya Tanzania kupigwa marufuku Ulaya, sasa ndio tumshauri Rais wetu aufyate kwa hili la wizi wa mchana kweupe kisa mwizi ni mtoto wa mataifa makubwa. Cowardness.
Alikuwa ni moja ya wakili wa Serikali? au ajenge hoja gani? Tendea haki basi huo ubongo wako
 
Back
Top Bottom