Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.
Tundu Lissu
Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu
"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu
Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini
Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.
"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu
Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati
Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...
"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu
Muwache kukurupuka na kupoteza kodi zetu kwa kulipia fidiaTunaye AG kikatiba
Wakurupukaji mmejaa ccmHawezi!!?Soma post uelewe usikurupuke
Wakati mikataba hii inasainiwa, hatukuwa na AG?Tunaye AG kikatiba
Umfano ni taarifa ya kamati iliyochunguza ule mchanga
Embu jiulize kwanza kabla ya kukataa ushauri .mfano enzi ya Nyerere alikamata Mali na mashamba ya mzungu tajiri mkoani Arusha kwa jina Stein maharufu kwa jina bwana ugoro alikuwa anamiliki mashamba ekari laki 3 na 60 elfu.alikamatwa kwa kosa lakukutwa na shilingi milioni 24 ndani ya ndege yake alipotua nchini Kenya.wakati huo 24 milioni ni pesa mengi sana.bajeti ya Mwaka wakati huo ni 580 milioni.Nyerere alipopata habari hiyo kutoka polisi Kenya.mzungu alipo rudi Tanzania akakamatwa akawekwa ndani uhujumu uchumi .na Mali zake zote zika zuiwa .mfano ya haya makontena ya mchanga Leo.baada ya masiku kadha wakampa dhamana wakazuia na pass yake.lakini mzungu alitoraka nchi wakati huo huo.akaenda kwao holand .akafungua kesi kwenye mahakama hi hii Lisu anayosema .Nyerere kwa ubabe huu huu unao jidai nao.akaongeza zaidi akataifisha Mali zote mashamba ,ndege ,magari akafanya shamba la serikali .wakati huo mzungu anaendelea na kesi huko majuu.huku Tanzania tumegomea ataa tulipoitwa mahakani utukwenda tuligoma.kesi ikawa inaendelea huko majuu .mfano Wa kesi ya Iptl kwa Leo,mahakama huko majuu wakatoa hukumu mzungu alipwe pesa zake zote.serikali ikataarifiwa kulipa ikagoma.Mahakama huko ikatoa amri serikali ya Tanzania ikamatiwe Mali zake popote zilipo duniani .Wakati huo Tanzania hawana habari nikama waliamua hakuna kitu watatufanya ikapita na muda ikawa tumesahau hivi.Mara ghafla ikaja taarifa meli ya Tanzania na shehena ya sukari imekamatwa ikipita kwenye pwani ya uholanzi na inapigwa bei mnadani na sukari yake meli ya takoshili wakati huo kama sijakosea jina na ilikuwa ni Mali ya ubia kati ya China na Tanzania.Ndio Mara ghafla Tanzania ikajikuta inanyolewa bila maji.Ghafla Warioba wakati huo Waziri sheria.akatumwa haraka uholanzi .matokeo yake mzungu alipidi abembelezwa akarudishiwa shamba lakini wakati huo tayari serikali ilishagawa baadhi ya mashamba kwa wananchi kutoka ekari laki 3 na 60 elfu mpaka kubakiwa na ekari 60 elfu .ikabidi wambembeleze mzungu apoke hiyo elfu 60 ambayo mpaka Leo hii ni Mali ya huyo mzungu.pamoja mabilioni taslimu na kuombwa kuendelea kulipwa pole pole na riba kila Mwaka tena kwa makubaliano deni liingizwe kwenye bajeti Tanzania likilipwa kila Mwaka.na hili deni limekuwepo kwenye bajeti Enzi ya Nyerere,Mwinyi,na Mkapa .kwa Kikwete sikupata kusikia labda itakuwa deni limekwisha ,kwa hiyo ushauri ushauri Wa Lisu niwakuzingatiaTundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
Stick to the point you fool. Kama hujui namna ya kujenga hoja za mada husika kuna majukwaa ya size yako pia humu kama la photos na celebrities. Tunahitaj hoja za je hii hatua ya pendekezo la lisu inaweza kutatua tatizo? Je madhara yake kitaifa na kimataifa ni yap? Je kuna mbadala? Tunachokubaliana wote ni ..lazima tuondokane na unyonyaj huu. Next is HOW?Lissu huyuhuyu wa mwembeyanga na list of shame au mwingine?!!!
Mkataba unakutaka uniambie percentage ya madini fulani katika mchanga,wewe kwa ujanja wako ukaniambia yaliyopo ni 10% wkt ukweli ni 30%,mimi nilivyoshituka nikazuia huo mchanga,sasa hapo nani alianza kuvunja mkataba!?Elewa kuwa acacia wamesaini mkataba wa kuchimba dhahabu. Kikawaida hata ukiokota jiwe mtaani ni composition ya minerals nyingi mno. Hivyo uwekezaji hutegemea what is your mineral of interest. Sidjani kama hayo madini yote yalioorodheshwa ni muhimu katika biashara ya dhahabu. Otherwise walipaswa kuzuia usafirishaji from day one
Haya chief Mangungo,naona uko mstari wa mbele kuwatetea wafadhili wako!Ujifunze kupembua vitu vizuri unakurupuka tu kama Rais wako.. Subiri uone jtatu wanafungua kesi mahakama ya, biashara.. Swali la kwanza wameuliza maabara zilizotunika ziko cerfified kimataifa kufanya hiyo kazi? Tayari gumi la pua round ya, kwanza tu..
Wewe ulikuwa unadeclare amount sahihi!?Taratibu zinaongizwa na kanuni , ambazo mawaziri wajiwekea na zilikuwa zinatumika.mm nimesafirisha sana shaba ufi, kikanuni ulikuwa unadeckre unachosafirisha na si kila element, inayolipiwa mrabaha ilikuwa ni unachosafirisha, na ndo mawaziri wote na mamishina wa madini walikuwa wakizingatia.
Hivyo kama ni kulifabya liwe kisa tubadirishe kanuni na taratibu na si hivi ilivyo sasa.
What are you trying to say!?Wizara, taasisi na wakala kadhaa za serikali ndo wanazibariki hizo data..
Funguka akili.. Think outside and behind beyond the box!
Unataka kusema kuwa km TMAA walihongwa then the gvmnt haipaswi kuchukua hatua?Mheshimiwa, kwa mujibu wa mkataba wao declaration halali ni ile inayotokana na assaying iliyofanywa na chombo cha serikali kiitwacho TMAA, kwa hiyo hadi sasa Acacia hawajasema uongo, kisheria. Ingekuwa TMAA wametoa jibu halafu Acacia wakafoji, au kama TMAA wakikana viwango vilivyoandikwa kwenye containers, hapo kwa mujibu wa mkataba ndipo watakuwa wamedanganya. Lakini hadi sasa, reference figure ambayo kimkataba ni halali ni ile iliyoandikwa na TMAA na kukubaliwa nao kabla ya kufunga (seal) container. Na mkataba wao unasema kama hiyo figure inabishaniwa, basi kuna arbitration sample ambayo inapaswa kupelekwa kwa independent lab, in the presence of representatives from both Tanzania Government and Acacia. Kilichofanyika hadi sasa ni kuwa mlalamikaji (serikali yetu) amejichukulia sheria mkononi akachukua samples zake bila kuwepo uwakilishi wa mlalamikiwa, na amezifanyia analysis kwenye lab yake mwenyewe, siyo independent, kinyume na mkataba. Sijui mnanielewa wakuu?
Wametuibia kweli, lakini tumechukua hatua ambazo zitatuumiza zaidi. Tumempa mwizi wetu nafasi ya kutupiga zaidi badala ya sisi kumpiga.
Prof Kabudi and associates lazima wapange timu nzuri hapoSheria ni mchezo kwa sehemu kubwa. Wezi wanaijua hii michezo kuliko 'watakatifu'...
Sijui 'kliarensi reti' ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu, kama iko ninavyodhani basi ushauri wa Rais wa TLS kwa Rais mwenzake sio wa kubeza hata kidogo.
Mkataba ni tatizo ndio bt haiwezi kuwa ndio ukuta wa kuzuia haki yetu,km haikuwa sawa its high time now kunegotiate better dealsTatizo Wise Comedian,mwenzio anajua kilichopo ndani ya hiyo mikataba ni upupu mtupu ndiyo sababu anaeleza hivyo.Mikataba yetu imejengwa katika UOVU mtupu wa kujilimbikizia mali kwa wachache.Anachoshauri kifanyike mengine yanaendelea.
All are possible options, but the later suits the situation betterKwanini msiwashitaki badala ya kujichukulia sheria mkononi ?
Lisu anapaswa kuwa real patriot kwa kuonyesha way forward kwa hapa tulipofikia na sio kujifanya mamlaka ya hali ya hewa kwa kubashiri yajayo!Lisu amesema anayo mikataba ya bulyankulu kwa hiyo anajua inasema nini. Pia anauelewa wa hiyo mikataba ya kimataifa inasema nini kuhusu hilo. Wakoloni huwa wanajua wanachokifanya. Kabla hawajaja kuwekeza miaka mingi nyuma walikuja na mradi wa reforms za sector ya madini. Mradi huu waliuleta kama msaada ambapo ulirekebisha sheria zetu nyingi kwa kisingizio cha kuvutia wawekezaji humo humo ndio waliweka mitego.
Kama hawajui, na warudi vyuoni, tutaishia na wahimu wa namna gani?Kwao hao maprofessor na Phd zao hawajui? Kama hawajui bora warudi chuoni wakafundishe, sioni umhimu Wa kuongozwa na wasomi katika hii nchi !!