Tundu Lissu: Tutanyolewa bila maji suala la mchanga wa madini, tusikurupuke

Ujinga na upumbavu wa Lissu ni kujiona anaakili kuliko mtu yeyote Tanzania!!!
Haturudi nyuma, kama anawashwa atangulie yeye huko kwenye hizo mahakama anazoziogopa!!!
Yaani watu wanadeclare uongo afu tuwachekee kisa sijui mikataba gani huko tumesaini!!!?! Huu ujunga hautafanyika awamu hii!! Subirini awamu dhaifu zije

Yaani una maana kuwa Tundu Lissu ni mpumbavu na wewe ni mwerevu, siyo ?

It's likely 120% the opposite......kwamba, wewe ndiye hasa mpumbavu, kwa sbb umeshindwa ku - counter attack hoja ya Lissu simply kwa sbb, you know nothing !!

Wana declare uongo ? Ukweli ni upi eti ? Wa kamati ya kumfurahisha Mr Misifa, Mfalme Mtukufu Uchwara ?

Aisee, please, jaribu ingalau kuwa serious kiogo, basi !!
 
Nimesoma tamko na ushauri wa kaka yangu Tundu Lissu. Ni mzuri lakini amesahau kuwa sheria za kimataifa ambazo Lissu ana hofu nazo kuwa tutanyolewa bila maji ZINAPINGA UONGO WA WAWEKEZAJI. HII NDIO HOJA KUU YA RAIS MAGUFULI. MIKATABA YA KIMATAIFA INASISITIZA INTEGRITY. WAWEKEZAJI WA MADINI NCHINI ESP HAWA WA MCHANGA WA MADINI WAMEANGUKIA KWENYE UONGO. WAMELIDANGANYA TAIFA HURU LA TANZANIA. GO ON TANZANIA. LINDA RASILIMALI ZAKO

Lete mfano wa huo uwongo wa wawekezaji hapa., otherwise utuletee mkataba wa serikali na hawa wawekezaji kwamba Tanzania iliwatuma na kuwapa kazi wachunguze huo mchanga kama una madini halafu wapeleke mrejesho serikalini.

Shida kubwa tz kila kitu ni hahe-hohe mnakumbuka shuka tayari kumekucha. Lissu alichoongea ni sawa kabisa mtapambana tu na sheria za kimataifa hakuna namna.
 
U
Lete mfano wa huo uwongo wa wawekezaji hapa., otherwise utuletee mkataba wa serikali na hawa wawekezaji kwamba Tanzania iliwatuma na kuwapa kazi wachunguze huo mchanga kama una madini halafu wapeleke mrejesho serikalini.

Shida kubwa tz kila kitu ni hahe-hohe mnakumbuka shuka tayari kumekucha. Lissu alichoongea ni sawa kabisa mtapambana tu na sheria za kimataifa hakuna namna.
mfano ni taarifa ya kamati iliyochunguza ule mchanga
 
Du
Watanzania siku zote, tumekuwa watu wa kulaumu tulipoangukia badala ya kulaumu tulipojikwaa. Haya mambo tunayachukulia juu juu tu.

Wakati watu wanalalamikia sheria za madini zikipitishwa kwa muswada wa dharura, wabunge wa ccm hawakujali wakapitisha kichama kwakuwa muswada umeletwa na Serikali yao. Hawakutaka hata kujiuliza kwa nini hawaruhusiwi kuona hiyo mikataba.

Haya ya sasa ndo matokeo ya hizo sheria walizopitisha, tuache kutafuta mchawi.

Mi naona Lissu yupo sahihi, wakitupeleka, mahakamani tutashindwa tena mchana kweupe. Acacia hawahusiki katika kupima kujua gold concentration ya mzigo. Wao wanapimiwa na Wakala wa madini TMA wanatakiwa kuthibitisha. Sasa kama TMA walipima wakathibitisha wakapitisha, accacia wanahusikaje katika kudanganya?

Yaani walishatubana tukasaini mikataba ya Kimataifa, tukawatungia na sheria za ndani za kuwapendelea na kuwamilikisha hayo madini. Tukaenda kusaini hiyo mikataba ya madini yenye makurasa kibao bila hata kusoma, tena tunaenda kusainiana kwao, unategemea nini? Wazungu wajanja sana.

Utapelekwa mahakamani unaoneshwa kipengele, unatoa macho hiki nacho kilikuwepo unakuwa kituko.

Tulipaswa kushikamana wakati wa kupitisha hizo sheria za madini, tuwe wamoja tusingekubali Bunge kupitisha sheria muhimu hivi zinazohusu hatma ya mamilioni ya watanzania kwa muswada wa dharura bila kusoma vipengele.
. Wao hawapimi? Wanapimiwa?.... Na ela wanapokelewa wakishayauza? So mwizi ni mpimaji au mchakatuaji? Nani huyo anaye wapimia? SGS? Cha msingi serikali isubiri ripoti ya pili ya kiuchumi na kisheria before kutoa maamuzi zaidi. Ili tukwepe ujanja ujanja wa sheria kandamizi. I am sure hawa wa ripoti ya pili wako wanasoma mikataba kuona ubovu na ukiukwaji ili tujue nini cha kufanya bila kuingiza taifa hasara kubwa.
 
Mnasingizia wazungu ndio waliotudanganya...visingizio tuu kwani nani aliyewaleta na kuwaonyesha njia za kutupiga na wengine wapo kwenye bodi za wakurugenzi zao....tumewaleta wenyewe kwa mbwe mbwe na kugonga meza na sauti za NDIOooooooooo... sasa hivi tunajifanya wanatuibia! Pathetic!
 
issue ni....je, ni chombo gani independent kimeleta hizo findings? in the context of international commercial contracts, ile kamati ya Rais haina credibility yoyote kwani iliteuliwa kwa 100% na serekali ambao ni upande mmoja tu wa mkataba (aka mlalamikaji).

kwa taarifa yako, zile findings za ile kamati ziko technically skewed (wale wataalamu wa statistical computations mtanielewa).
I thought the best way to challenge it is to come up with scientific data. They have been using SGS and so forth...sio maneno maneno hayasaidii
 
Unajua kiukweli tunakiuka mikataba so tutalipa fidia kubwa yale yale ya escrow....,bravo lissu
 
Hatuwezi nyonyolewa kwa kuwa tunaye Wakili Msomi na Mzalendo wa Nchi take.


Naye ni T.Lisu hatuna shaka mh.JPM endelea na kazi
 
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu




Sawa ushauri ni mzuri, ila kwa nini hakuutoa kabla ya matokeo ya hii ripoti? Wakati tume inaundwa, wakili TL alikua na nafasi ya kupendekeza hayo maoni yake ila hakuona umuhimu, alisubiri hadi kamati itoe ripoti ndo nae aseme alichokuwa anawaza. Hii sio sahihi. Mi nafikiri, ushauri wa maana ni ule utakaolenga kutatua kilichopo kwa sasa na sio ule ambao ulitakiwa ufanyike kabla ya kilichopo. Imeshatokea kama ilvyo, TL atoe ushauri kuwa tufanye nini kwa maslahi ya Taifa na asione kuwa ni kwa ajili ya CCM. CCM imeshachoka, inahitaji ushauri kutoka nje ya makada wachumia tumbo. Please, Lisu tuambie nini kifanyike kwa sasa kuondoa kadhia hii.
 
Ushauri mzur sana lkn nadhan pia kwa huu wizi waliokuwa wakiufanya tuna sababu za msingi za kuwashitaki pia ikiwa na kushikilia mali zao wkt tukitafuta suluhu
 
Kwakuwa wametuibia basi tuna haki ya kuvunja hiyo mikataba lasivyo watulipe hicho walichotuibia kwanza, vinginevyo tutajifidia kwa kuchukua Mali zao
Mali zao Kama zipi mkuu?nawa hakikishia ule mgodi wa bulyanhulu ata mkiachiwa leo wa tz hamuwezi kuu endeleza ata kwa mda wa miezi3.labda muandae wachina
 
Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
Elewa kuwa acacia wamesaini mkataba wa kuchimba dhahabu. Kikawaida hata ukiokota jiwe mtaani ni composition ya minerals nyingi mno. Hivyo uwekezaji hutegemea what is your mineral of interest. Sidjani kama hayo madini yote yalioorodheshwa ni muhimu katika biashara ya dhahabu. Otherwise walipaswa kuzuia usafirishaji from day one
 
Upinzani wa nchi hii, ukiongozwa na chadema wameleta mshituko mkubwa kwa wananchi baada ya kuanza kupinga maendeleo ya wananchi!!

Tangu kuanza kwa awamu ya Tano, imeonekana kasi ya Rais Magufuli imewaacha mbali mno wapinzani kiasi kwamba hata waliyoahidi kuyatatua leo wanayapinga!!!

>Chadema ya leo wanapinga >Elimu bure
>Ujenzi flyover

>Ununuzi wa ndege <Ujenzi wa reli
Bei ya zao lá korosho kupanda />Serikali kuhamia Dodoma />Wakwepa kodi kufukuzwa />Wauza madawa ya kulevya kukamatwa. Hali hii imewaacha njia panda wananchi wasijue wapinzani wa nchi hii hasa wanasimamia nini.

Labda leo tuwaulize, nyie wapinzani uchwara wa nchi hii kwenu neno maendeleo huwa mnaelewaje??
Alie pinga ninani kuhusu hili jambo?hebu zbitisha yaelekea hujui tofauti ya ushali na kupinga.
 
Alie pinga ninani kuhusu hili jambo?hebu zbitisha yaelekea hujui tofauti ya ushali na kupinga.

Tatizo la Vijana hawa wa ccm kitengo cha Jamii forums/facebook/whatsup & Instagram, ni Kufuata upepo yaaani kusifia tu hata sehemu ya kutoa ushauri wanasifia tu.

Mimi sipotezagi muda wangu kuwajibu
 
Sawa ushauri ni mzuri, ila kwa nini hakuutoa kabla ya matokeo ya hii ripoti? Wakati tume inaundwa, wakili TL alikua na nafasi ya kupendekeza hayo maoni yake ila hakuona umuhimu, alisubiri hadi kamati itoe ripoti ndo nae aseme alichokuwa anawaza. Hii sio sahihi. Mi nafikiri, ushauri wa maana ni ule utakaolenga kutatua kilichopo kwa sasa na sio ule ambao ulitakiwa ufanyike kabla ya kilichopo. Imeshatokea kama ilvyo, TL atoe ushauri kuwa tufanye nini kwa maslahi ya Taifa na asione kuwa ni kwa ajili ya CCM. CCM imeshachoka, inahitaji ushauri kutoka nje ya makada wachumia tumbo. Please, Lisu tuambie nini kifanyike kwa sasa kuondoa kadhia hii.
kabla ya mikatba ya madin kusainiwa na kupitishwa bungen wapinzani walionesha waz kutordhika na kupaza saut wakapuuzwa sasa huu ushaur wa Lisu angeutoa mwanzon unfikir angeeleweka?? hata sahv hmtamuelewa baada ya matokeo ya alichokisema mtaanza kutafta pa kujishikilia
 
52 Reactions
Reply
Back
Top Bottom