Tundu Lissu: Tunataka mafaili ya Muungano siyo picha za Nyerere na Karume

Ivi hii referendum ni ngumu sana kufanyika? Mbona znz walifanya ya serikali ya umoja kirahisi ivyo?
 
despite of whaever LISU said. Who makes good ideas in the House of Representatives to become things or actions? notwithstanding who particularly said (CCM/CDM/...)
Nimejaribu kusoma tena na tena lakini sijaambulia kitu!!vp kama ungetumia kiswahili?
 
Mm nataka huu muungano ufe hauna manufaa yoyote kiuchumi utaskia mbunge anasema faida za muungano ni kuoana
Right, imagine that, eti "faida ya kuoana," how preposterous is that?

Kuna silly faida nyingine ya "faida ya watu kuishi freely kule na huku." Well, kama hiyo ni faida mbona tumewachomolea Wakenya waliotaka kuishi freely huku na kule katika EAC? Ni wiki iliyopita tu Tanzania imetoa msimamo mpya against fast paced EAC unification, sasa kama Muungano siku zote una faida, kwa nini tumeamua kwenda taratibu na EAC, hatutaki faida za kuoa Wakenya, Wanyarwanda, Waganda, Warundi?

Sidhani kama li muungano litapona Katiba mpya. Sasa hivi kuna Bunge la jamhuri na baraza la wawakilishi yanaendelea at the same time. Nikamwona Vuai Nahodha kaenda baraza la wawakilishi badala ya Dodoma, nchi ina ma ishu kibao ya mambo ya ndani, mauaji, ujambazi, etc. etc, Nahonda yuko Zanzibar, sasa si abaki huko huko, na ubunge wake wa kupewa. Eff the Muungano.

 
Lissu ameongea jambo la msingi sana..kuna walalkini katika huu muungano..yaonekana hakukuwepo maridhiano baina ya viongozi na wananchi wao kwa pande zote mbili..Hata katika harusi ambayo ni muungano wa watu wawili mke na mume,familia za pande mbili huonana na kuridhia na wawili wanaooana hukiri kwa vinywa vyao makubaliano yao katika kuungana kwao..Sasa katika huu Muungano hakukuwepo maridhiano ya wananchi wa pande zote mbili..Na hili ni tatizo kubwa
 
Hongera sana Lissu,
Tatizo la watu wengi na hasa baadhi ya viongozi ni kushindwa kusema ukweli,tukiweza kusema ukweli matatizo mengi ya nchi hii yataondoka yenyewe.
 
Tupate maoni ya wana forum kuhusu Muungano.

Je Unafaa kuwepo? Na kama unafaa; Wa Aina gani? Serikali Ngapi.

Wapenda Afrika tulisikitika kwa habari ya kugawanyika kwa Sudan; lakini ni jambo lisiloepukika, je na huu wa kwetu hivo hivo?
 
Kweli kabisa mkuu; he was very clear and to the point. Hakumung'unya maneno; yaani ni mtu ambaye ukisikiliza maneno yake ukalinganisha na jinsi anavyoji-behave wakati anapotoa lecturer yake huna shaka kwamba ni mtu makini na anamaanisha anachokisema pasi na unafiki wowote - hata magamba wengine wakiongozwa na Sitta, Werema, Lukuvi, na Vita Kawawa niliwaona wakisikiliza lecture ya Lissu kwa umakini wa hali ya juu. Kwa uchache ameongelea yafuatayo:-

(i) Muungano ulifanywa kwa usiri mkubwa, siku 100 tu tangu Mapinduzi ya Znz ukawa tayari.
(ii) Hakuna chombo chochote cha uwakilishi wa wananchi kilichoshirikishwa katika kuundwa kwake.
(iii) Uliundwa kwa dharura hasa kwa shinikizo la mataifa makubwa ya wakati huo pamoja na hali tete iliyokuwepo Visiwani mara baada ya mapinduzi.
(iv) Mambo ya awali ya muungano (Articles of the Union - ambayo kimsingi ndio Muungano wenyewe) yalikuwa 11 lakini baadaye yakaongezwa kinyemela hadi kufikia 22 hivi sasa likiwapo suala la fedha.
(v) Muungano sio kama suala la Musa (pengine hapa akimaanisha maandiko) ambayo hayahojiwi popote bali ni suala la Kaisari (pengine akimaanisha Sheria za nchi) ambao tuna haki ya kuhoji kila kitu na kwa uwazi.
(vi) Mafanikio ya NYERERE na KARUME ni yetu sote vivyo hivyo na madhaifu yao hivyo tusione shaka wala aibu kuhoji na/au kukosoa.

Sasa, ili kuondokana na kinachoitwa kero za Muungano na manung'uniko ya kila uchao; ameshauri mambo MAWILI ya msingi yafanywe kwa WANANCHI kuulizwa yafuatayo:-

(i) JE, TUNAHITAJI MUUNGANO?
(ii) KAMA NDIO, MUUNGANO WA AINA GANI (muundo)?

Kimsingi amepasua jipu. Asante sana Mh. Lissu.


Na ukisoma kwa makini sana kijitabu kuhusu muungano kilichoandikwa na Sheikh Aboud Jumbe kimebainisha wazi kuwa JK Nyerere ndio alilazimisha muungano kwa maslahi binafsina nchi yake Tanganyika lakini vile vile ukisoma kijitabu kuhusu muungano cha Prof Issa Shivji kimeweka wazi kabisa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar hauna uhalali kwa aina yoyote iwe kisiasa au kisheria. Hivyo muungano huu ni batili. Na aliendelea zaidi kwa kusema Muungano huu si Muungano bali ni Mvutano.


Sasa Mimi nashauri WaTanganyika hapo mna nafasi kubwa kudai utaifa wenu na hilo litapelekea kuwe na taifa huru la Tanganyika kama ilivyo Zanzibar ndipo mengine yafuatwe.

Sioni sababu kuona aibu kuu discuss huo muungano kwa uwazi na upana wake wote ili kuondoa malalamiko ya pande zote.

Ahsantum Sana Tundu Lissu kupasua jipu. Wengine kazi kwenu
 
Na ukisoma kwa makini sana kijitabu kuhusu muungano kilichoandikwa na Sheikh Aboud Jumbe kimebainisha wazi kuwa JK Nyerere ndio alilazimisha muungano kwa maslahi binafsina nchi yake Tanganyika lakini vile vile ukisoma kijitabu kuhusu muungano cha Prof Issa Shivji kimeweka wazi kabisa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar hauna uhalali kwa aina yoyote iwe kisiasa au kisheria. Hivyo muungano huu ni batili. Na aliendelea zaidi kwa kusema Muungano huu si Muungano bali ni Mvutano.


Sasa Mimi nashauri WaTanganyika hapo mna nafasi kubwa kudai utaifa wenu na hilo litapelekea kuwe na taifa huru la Tanganyika kama ilivyo Zanzibar ndipo mengine yafuatwe.

Sioni sababu kuona aibu kuu discuss huo muungano kwa uwazi na upana wake wote ili kuondoa malalamiko ya pande zote.

Ahsantum Sana Tundu Lissu kupasua jipu. Wengine kazi kwenu

Exactly! Hakuna sababu ya kuficha au kuona aibu kujadili mambo ya Muungano. Mwenyekiti wa kikao cha jana ambapo Lissu alimwaga washawasha alikuwa Mh. George Simbachawene (Kibakwe - CCM) na baada ya mjadala ali-comment:

"Nadhani Katiba Mpya itaangalia yote hayo (aliyozungumza Lissu na wengineo)".

LAKINI shida ya wana-CCM ni UNAFIKI, japo Simbachawene ni bora by far pengine kuliko hata Madam Speaker, alisahau DRAFT ya Muswada wa Sheria ya uundwaji wa Katiba Mpya (ambao hata hivyo umekataliwa na wengi) Serikali ya CCM, pamoja na mambo mengine, imezuia suala la Muungano kuwa mojawapo ya mambo ya kujadiliwa na wananchi. Jamani, unafiki utatufikisha wapi wajameni?
 
muungano tunaoutaka ni wa kuungana tuwe kitu kimoja, atakae leta choko choko achukuliwe na kupigika vibaya sana, kwa mfano waZenji wakileta chokochoko wapigike vibaya sana. Yaani ni ubabe ubabe kama Marekani, hivyo ndo life litasonga vizuri sana! Bora punda afe lakini mzigo ufike. Bora lawama kuliko fedheha.
 
Wabunge wengi wa ccm wababaishaji sana maana kazi yao ni kupiga makofi tu hata kama hajaelewa maana usipopiga makofi utajibu nini mbele ya NEC. Lisu mbele kwa mbele...!
 
Hatuhitaji kabisa muungano. Muungano uvunjwe upesi kila mtu achukue chake na kujijua kivyake
 
Poteza....tunaweza tukawa tunauihitaji Muungano, lakini si muungano na Zanzibar....
 
Zanzibar na Tanganyika tangu zama za zama; ni kitu kimoja; tumetenganishwa na wakoloni. Wazanzibari ni ndugu zetu, na Sisi ni ndugu zao. Hivyo suala la Muungano ni muhimu uendelee. Kwanza itakuwa tunawaenzi viongozi wetu na kudumisha umoja wetu. Tukujitenganisha tu, tumekwisha na laana ya Viongozi wetu itatutafuna. 'Tanzania Tanzania, mimi nakupenda sana'. Kuuvunja muungano ni kumtusi Baba wa Taifa na Karume. Ni kuutusi utawala wote tangu Uhuru.

Kuna matatizo, ambayo yanaitwa kero za muungano; hizo kero zifanyiwe kazi ili pande zote mbili za Muungano ziridhie. Hakuna pande moja kuridhika na nyengine kunyong'onyea, HAPANA; pande zote ziridhike. Ila ijulikane kwamba there is give and take in such negotiations / arrangements.

Ifanywe referendum kupata maona ya Tanzania Bara na ya Tanzania Visiwani kuhusu aina ya Muungano na Serikali ngapi? 2? 1? 3? 5? ba baada ya hapo Iundwe 'Constitutional Assembly' ili ituandalie Union Costitution.

Tulipofika hatupaswi kurudi nyuma ' Nasi hatutorudi nyuma, Sote mbele tutaendelea'!
 
Zanzibar na Tanganyika tangu zama za zama; ni kitu kimoja; tumetenganishwa na wakoloni. Wazanzibari ni ndugu zetu, na Sisi ni ndugu zao.
Hata Wakenya tumetenganishwa na Wakoloni, lakini mbona tumewaambia heeey, slow your role with this EAC thing. Kama kuungana ungana na majirani ni poa Wakenya sio ndugu zetu?


Tukujitenganisha tu, tumekwisha na laana ya Viongozi wetu itatutafuna.
Laana ya Viongozi wetu ndio nini bana wewe!?? Mtoto mdogo ndio anatishiwa "laana." Muungano tunauvunja na hakuna cha laana.

Ifanywe referendum kupata maona ya Tanzania Bara na ya Tanzania Visiwani kuhusu aina ya Muungano na Serikali ngapi? 2? 1? 3? 5?
Tuulizwe kwenye referendum ni aina gani ya Muungano tunataka, umejuaje tunautaka? Kwanza kabisa tuulizwe: Je Tunataka Muungano? Mkilazimisha lazimisha matokea yake ndio haya, Muungano unakuwa hauna legitimacy na watu wanau question kila uchwao. Acheni Watanganyika na Wazanzibari, kama wanataka, waungane kwa utashi wao, au kama hawataki, Muungano out the window!
 
TASO

Si tumeambiwa tutoe maoni? mimi nimeweka maoni yangu kwamba kuuvunja muungano ni:-

1. Kurudi Nyuma, tunatakiwa tuwe na United Africa (Angali EU; kumbuka wakati tunapigania uhuru; mpaka BOB ALIIMBA AFRIKA UNITE)
2. Kutukana uongozi ulioingia kwenye muungano.\
3.Kukana asili ya umoja na udugu wetu.

I am a panafricanist and I believe in a Strong, Unified, and Politically United Africa; sio watu wanatetea ukubwa wa madaraka ya dola na kuangamiza maslahi ya wengi.

Sikusema kwamba LAANA namtisha mtu; lakini UNION imekuja out of vision ya kwenda towards a United Africa. Kwenda kinyume na hapo kuna dire consequences.

I believe in the decision of the people, na hata leo naamini watanzania wakiulizwa kama wanautaka au hawautaki muungano; WENGI WAO hawatoukana muungano. Tatizo ni kuuweka katika sura nzuri. pasiwe na manung'niko. Unataka kuwanyima Wazanzibari watoto wa Kinyamwezi? Au unakusudia kuwanyima wasukuma watoto wa Kipemba?

TANZANIA TANZANIA, JINA LAKO NI TAMU SANA!

Hata Wakenya tumetenganishwa na Wakoloni, lakini mbona tumewaambia heeey, slow your role with this EAC thing. Kama kuungana ungana na majirani ni poa Wakenya sio ndugu zetu?


Laana ya Viongozi wetu ndio nini bana wewe!?? Mtoto mdogo ndio anatishiwa "laana." Muungano tunauvunja na hakuna cha laana.

Tuulizwe kwenye referendum ni aina gani ya Muungano tunataka, umejuaje tunautaka? Kwanza kabisa tuulizwe: Je Tunataka Muungano? Mkilazimisha lazimisha matokea yake ndio haya, Muungano unakuwa hauna legitimacy na watu wanau question kila uchwao. Acheni Watanganyika na Wazanzibari, kama wanataka, waungane kwa utashi wao, au kama hawataki, Muungano out the window!
 
Back
Top Bottom