Tundu Lissu: Tiketi mkononi, ulemavu mwilini, uimara moyoni. Anarejea uwanja wa mapambano kutimiza haja ya moyo wake!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Anarejea terehe 7 Septemba, mwaka huu. Jumamosi ijayo. Tayari, tiketi ya kurejea nyumbani Tanzania i mkononi mwake. Kila kunapokucha na anapotafakari kurejea nyumbani, Lissu huitoa tiketi yake kutoka katikati ya nyaraka zake na kuitazama huku akitabasamu. Anatamani kuwaona tena wale ambao hawakuweza kumuona akiwa Nairobi na Ubelgiji (namshukuru Mungu kuwa nilikwenda kote huko).

Lissu si yule yule kimwili. Amepata ulemavu wa mwili. Sasa anachechemea na kuchapia mguu. Ulemavu ameupata tarehe ya kurudi kwake mwaka juzi. Ameupata ulemavu akiwa kwenye mapambano ya kisiasa kwenye viunga vya Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lissu survived to accomplish his mission. Ulemavu wa mwili alioupata ni alama ya mapambano yake na harakati zake za kuusema ukweli hata kama ni mchungu kama shubiri. Au sifongo kwenye kidonda.

Kwa kilichomtokea na alichojionea kutoka kwa watanzania na wasio watanzania; marafiki na wasio marafiki wake; wanasiasa na wasio wanasiasa; wanachama wa chama chake na wasio wanachama wa chama chake kimemuimarisha moyoni na kumjaza ujasiri mkuu. Nilipozungumza naye Naironi na Ubelgiji, alinitisha kwa ujasiri wake kuimarika kuliko mwanzo. Yuko imara kuliko mnara na kuliko chuma cha pua.

Lissu anarejea na ukweli wake; lugha yake; Uwakili wake; utu wake na watu wake. Atawahutubia; atawaambia; atawatetea; atawaombea na kuwapigania katika nafasi atakayojaaliwa kuipata. Lissu anarudi kwenye mapambano ya kisiasa na ya kisheria. Atakapotua tu nchini, hata Nguvu ya Kisheria ya Kaka yake Alute itakoma na Lissu ataichukua kesi yake ya Ubunge. Ataanza na hiyo kesi kwenye mapambano yake. Kwa ajili ya Ubunge wake.

Karibu nyumbani Tundu Antiphas Mughwai Lissu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma, Tanzania)
 
"Rudi mwanangu nyumbani ufanye na kurekebisha yale yanayo nitia simanzi huku niliko. 1995 niliposema siwezi kuikabidhi nchi kwa mbwa watu hawakunielewa wakasema nawatukana, lakini natumaini sasa wameelewa nilimaanisha nini. Muumba alizuia usije huku ili ukamilishe kazi anayotaka uifanye na wazee waliotangulia huku wote wanakutaka ukaifanye hasa mzee Kingunge anasema Tanzania sio barabara ya kuhitaji nyapala bali ni nchi inahitaji Rais"
Akisikika Mwalimu akizungumza na washiriki wenzake wa kikundi cha matarumbeta kumsifu Mungu.
IMG-20190902-WA0002.jpeg
 
Kwanza nikupongeze sana kwa ujasili wako kwa kitendo chako cha kwenda Nairobi kumjulia hali mh Lissu na hata kwenda huko ughaibuni kumjulia hali ndugu yetu Lissu.

Uamuzi ulio ufanya naelewa ungekuingiza matatizoni kulingana na msimamo wa viongozi wa chama chako.
Ina uma sana kuona hata baadhi ya wabunge wanao toka mkoa mmoja na mh Lissu walishindwa kwenda kumjulia hali kwa kuogopa kupoteza kibarua chao.
 
"Rudi mwanangu nyumbani ufanye na kurekebisha yale yanayo nitia simanzi huku niliko. 1995 niliposema siwezi kuikabidhi nchi kwa mbwa watu hawakunielewa wakasema nawatukana, lakini natumaini sasa wameelewa nilimaanisha nini. Muumba alizuia usije huku ili ukamilishe kazi anayotaka uifanye na wazee waliotangulia huku wote wanakutaka ukaifanye hasa mzee Kingunge anasema Tanzania sio barabara ya kuhitaji nyapala bali ni nchi inahitaji Rais"
Akisikika Mwalimu akizungumza na washiriki wenzake wa kikundi cha matarumbeta kumsifu Mungu.View attachment 1195569
Umekosea sana kuchanganya picha ya Nyerere na post ya Lissu.
Hawa watu wawili hawaivi.
 
Karibu sana Kamanda,Mungu azidi kukulinda dhidi ya wasiojulikana.Ikiwezekana safari hii uwe unatembea na bodyguard kama yule wa Diamond.

You are missed,Jimbo langu umenipora kama Lissu alivyoporwa!!!
 
Back
Top Bottom