Tundu Lissu: Tiketi mkononi, ulemavu mwilini, uimara moyoni. Anarejea uwanja wa mapambano kutimiza haja ya moyo wake!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Messages
12,919
Points
2,000

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2016
12,919 2,000
Anarejea terehe 7 Septemba, mwaka huu. Jumamosi ijayo. Tayari, tiketi ya kurejea nyumbani Tanzania i mkononi mwake. Kila kunapokucha na anapotafakari kurejea nyumbani, Lissu huitoa tiketi yake kutoka katikati ya nyaraka zake na kuitazama huku akitabasamu. Anatamani kuwaona tena wale ambao hawakuweza kumuona akiwa Nairobi na Ubelgiji (namshukuru Mungu kuwa nilikwenda kote huko).

Lissu si yule yule kimwili. Amepata ulemavu wa mwili. Sasa anachechemea na kuchapia mguu. Ulemavu ameupata tarehe ya kurudi kwake mwaka juzi. Ameupata ulemavu akiwa kwenye mapambano ya kisiasa kwenye viunga vya Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lissu survived to accomplish his mission. Ulemavu wa mwili alioupata ni alama ya mapambano yake na harakati zake za kuusema ukweli hata kama ni mchungu kama shubiri. Au sifongo kwenye kidonda.

Kwa kilichomtokea na alichojionea kutoka kwa watanzania na wasio watanzania; marafiki na wasio marafiki wake; wanasiasa na wasio wanasiasa; wanachama wa chama chake na wasio wanachama wa chama chake kimemuimarisha moyoni na kumjaza ujasiri mkuu. Nilipozungumza naye Naironi na Ubelgiji, alinitisha kwa ujasiri wake kuimarika kuliko mwanzo. Yuko imara kuliko mnara na kuliko chuma cha pua.

Lissu anarejea na ukweli wake; lugha yake; Uwakili wake; utu wake na watu wake. Atawahutubia; atawaambia; atawatetea; atawaombea na kuwapigania katika nafasi atakayojaaliwa kuipata. Lissu anarudi kwenye mapambano ya kisiasa na ya kisheria. Atakapotua tu nchini, hata Nguvu ya Kisheria ya Kaka yake Alute itakoma na Lissu ataichukua kesi yake ya Ubunge. Ataanza na hiyo kesi kwenye mapambano yake. Kwa ajili ya Ubunge wake.

Karibu nyumbani Tundu Antiphas Mughwai Lissu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma, Tanzania)
Unasemajee?mbona "kaingia mitini"
 

Forum statistics

Threads 1,343,537
Members 515,077
Posts 32,787,984
Top