Tundu Lissu: Sitarudi tena Tanzania hadi nihakikishiwe Usalama wangu

Sasa kama wasiojulikana wameweza kumfuata huko aliko ataogopaje kurudi?? Shetani sio dudu fulani ni binadamu ambaye ni wewe!
 
Kufuatia taarifa za wasiojulikana kumfuata Lissu ughaibuni ashtuka aaihirisha kuja nchini ajipanga zaidi kwa siku zijazo. Shetani hana rafiki. Mungu atamlinda dhidi ya wabaya wake. Source idhaa ya Kiswahili BBC, India.
Semeni aliopanga kwenda kuzuga nao kw kupiga picha wamemshtukia na kupiga chini ombi lake.
 
Huyu jamaa si alijimwambafayi kuwa atakuja tena mchana kweupe baada ya madaktari wake kutoa taarifa kuwa amepona.....what happened to wakili msomi TAL?mara ka change gear angani
 
Akihojiwa na Sauti ya Amerika kutoka Marekani, mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na mbunge wa Zamani wa Singida Mashariki amesema hawezi kurudi tena Tanzania kwani wasiojulikana bado hawajapatikana.

Pia amesema ametishwa na mwandishi Cyprian Musiba kwenye mitandao.

Nilichopenda leo hajaongea kwa kufoka foka na mikwara km tulivyozoea labda ameanza kubadilika kimtazamo



hahahaaaa kula matapishi yako . Jifunze kuwa na Kiasi cha maneno.Nani akuhakikishie usalama!
 
Kusema kwamba ahakikishiwe usalama yeye masaa 24. Tafsiri yake kisomi ni kwamba Watanzania wote hatuna usalama ukijumuisha na Famila yake yeye. Ni fedhea sana kutoa kauli hiyo. Huku tuna elimu bure tunakula tunafanya kila kitu cha kibinadamu .....
 
Hana umuhimu wowote katika nchi, wacha aendelee kuzurula huko siku akichoka atarudi hapa nchini akiwa masikini wa kutupwa
 
Ngoja tumsikilize kwanza mbowe na mange kimambi ili tujue maandamano yetu yataanzia wapi..
 
My brother TL, uamuzi ulioufanya ni sahihi kwa 100% kwa kuwa usalama wako ndicho kitu muhimu mno ktk maisha yako. Kwa mtu yeyote yule mwenye kujali, anatambua bayana juu ya kiu ya damu yako isiyokuwa na hatia kutoka kwa mahasimu wako.

Ukweli wako na msimamo wako unawafanya maadui zako kutokulala vyema, na hata waliposhindwa kutekeleza mpango wao wa kifedhuli dhidi ya maisha yako, bado wana "plan B" kwako.

TL, "God's time is the best" na hatima ya maisha yako ipo mikononi mwake. You survived that conspiracy, lkn wahusika wote ktk ile "evil scheme" nao hatima yao ni lazima wengi wetu tutapata kuishuhudia. Mungu awe pamoja nawe, na azidi kukuangazia njia zako njema ktk maisha yako. Amen.
 
Maji ya shingo lazima akubaliane na hali, maana hakuna jinsi. Alikuwa akijikaza tu wakati ule ila huu ndio uhalisia.
 
Kwan mabeberu hawajamhakikishia usalama, baada ya mda watamtimua huko, na akirud analikuta Jiwe kuu la pembeni walilolikataa waashi , linamwangukia na kumsaga saga
ingekua ndo ww sasa umekung'utwa risasi km 20 hv,zingine zimekuchakaza hadi matak*ni na sasa umepona kiasi flani japo bado huwez kutembea fresh,waliokumwagia risasi hawajapatikana na bado kuna watu wanasema ukirejea tu wanakumalizia,,,tuweke ushabiki maandazi wa vyama pembeni na tuangalie utu na usalama wako ,,,je ??ungerudi???
 
Hakuna Jambo limefanya niwachukie watz Kama ishu ya lisu ishu ya lisu imenifanya niwachukie Sana wenye mamlaka na praise power team yao yani msemakweli na mtetea haki ya kidemokrasia mnamtwanga risasi mnampokonya ubunge halafu mnafurahia na kumkejeli ushetani ulioje?
tuna nafsi ngumu sana
 
Nilipata shida kuhusu kufika kwake Tanzania ,wakati Fulani nilifikiri hawezi hawezi kuwaza vizuri ,kwa hili LA kuamua kusitisha kuja kwanza ,nalipongeza

Ukweli lisu kapitia jehanamu ya moto kwa yeyote anaye fikiri sawasawa ,hakuunga mkono kuja kwa lisu

Lisu umesema unasubiri viingozi waamue halafu uje mie nasema lisu utashi ni wako ww sio viongozi

Ww ndo ulipigwa lisasi sio hao viongozi

Pia unaweza uzwa na viongozi wakakuhakikishia usalama kumbe sio kweli

Kumbuka yesu aliuzwa ,je ww unaaminije hao wafuasi wako,akasema yupo musaliti wangu bado akawa Yuda

Niseme basi Mungu alikuokoa ndiye anaye weza kusema uishi.

Mimi ninan?i alihusika kwangu ni ndoto,nakiri chuki ipo kwa wasio jua maana ya chuki

Hawajulikani ndio usemi ila hakuna siri chini ya jua ,nanikweli mitume walisha sema

Tulia ubeligiji Mungu akujalie upone kabisa na Mungu ashukuriwe


Kuhusu u Raisi unaweza gombea makwani i au la,waswahili walisema ,subira yavuta heri

Subiri au usisubiri ,najjua upinzani utakuwepo 2025 iwe kweli au si kweli

Subirili ,Lisu ni kweli wa Tanzania bado wanataka mabadiliko

Tunacho taka wa Tanzania ni amani na sio Visasi

Tanzania itabaki ,watu wataondoka na kuja ,Amen
 
Ameen, Lissu ameshinda, Nilimwombea sana kwa Mungu ampe utashi wa kuamua alichoamua, Hakuna anayeweza kupinga kuwa Lissu sio Jasiri lakini Maombi tetu Mungu kayasikiliza. Lissu bado tunakuhitaji hata baada ya miaka 20mbele umeonesha uwezo kuliko hawa washamba wa Colomije.
 
Tumshukuru Mungu amepona Hakuna anayefurahia mtu kuumizwa

Ila kwa ushauri wangu akirudi Nchi Tanzania aombe msamaha kwa watanzania kwa kumtusi Nyerere
 
Siku hizi mabingwa wa Facebook wamehamia mpaka Jamiiforums!

Jamiiforums kwa sasa imekuwa kama jalala au dodoki!

Ni bora mtu ajue kama ni mjinga lakini ni hatari sana kuwa na mtu ambaye ni mjinga lakini hajui kama ni mjinga!
 
Back
Top Bottom