Tundu Lissu: Sitarudi tena Tanzania hadi nihakikishiwe Usalama wangu

Hapo kuna point, mtuhumiwa Mkuu ni serikali. ..kuna hatari akirudi kichwakichwa tu

Ni kweli, nakumbuka kulichompata Benino Acquino wa Philippines, alishauriwa asirudi nyumbani lakini akakataa na kweli yakamkuta mchana kweupeee, RIP Benino
 
Ni jambo jema ameamua Lissu kwa kweli, tukio limetokea na hakuna alietiwa hatiani kuna wasiwasi mkubwa kurudi na usalama wake
 
Lissu yuko smart
Arudi nchini kufanya nini wakati hata ubunge wameshamnyang'anya?

wamemuondolea hata platform ya kuongea ya bungeni

kama wangekuwa smart, wangemuacha arudi then wakamnyang'anya ubunge akiwa ndani ya nchi

Sasa hivi atakuwa huru hata kuandika kitabu dhidi ya Jamaa
 
Kuna vitu watu tulisema humu, tukabezwa...
P
 
Kuna baadhi ya watu wamekasirishwa kwa hili walitamani kuona akirejea ili apigwe risasi live na wakiona anakufa.

Mioyo yenu imesinyaa kwa taarifa hii.
 
Mlivyotaka kumuua mliona ni sawa?
Akihojiwa na Sauti ya Amerika kutoka Marekani, mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na mbunge wa Zamani wa Singida Mashariki amesema hawezi kurudi tena Tanzania kwani wasiojulikana bado hawajapatikana.

Pia amesema ametishwa na mwandishi Cyprian Musiba kwenye mitandao.

Nilichopenda leo hajaongea kwa kufoka foka na mikwara km tulivyozoea labda ameanza kubadilika kimtazamo

 
Mi nilijua ile mitusi na kashfa alizomwaga ilikua mbinu tu ya kuomba ukimbizi.
Karibu kwenye box mheshimiwa huko nako miaka 5 tu utanyooka.
Hamna longolongo huko.
 
Nani kakuaminisha kuwa Tundu ni msemakweli? Huyo ni vuvuzela hata ukoo wake wanamjua hivyo!
Nawe nimmoja wa wanaukoo wa Lissu? Kama sivyo, Basi punguza ujuaji kwa kushuhudia vya kusikia kwani siyo sifa njema kwa mtoto wa kiume!
 
Tujiulize, Lissu anaisaidia nini Tanzania au hata jimbo lake? Yeye arudi Tanzania au asirudi tupo vile vile.....hatumtaki abakie huko huko analelewa na bwana wake wa kizungu.
na hayo CCM wametusaidia nini zaidi ya miaka 55 wako madaraani kuna jipya?
 
Lissu yuko smart
Arudi nchini kufanya nini wakati hata ubunge wameshamnyang'anya?

wamemuondolea hata platform ya kuongea ya bungeni

kama wangekuwa smart, wangemuacha arudi then wakamnyang'anya ubunge akiwa ndani ya nchi

Sasa hivi atakuwa huru hata kuandika kitabu dhidi ya Jamaa
Wakati mwingine na nyie muwe mnajitathmini. Yaani huwa hamueleweki. Upepo ukienda magharibi mpo, ukienda mashariki mpo. Tarehe 4 September aliposema anakuja mlisema arudi, kaahirisha mnasema sawa. Huwa mnasikitisha sana, sijui ni stress au ni ule utafiti wa 32% ya watanzania ni vichaa.

Mwalimu nyerere aliwahi kusema "MTU Mwenye akili akikuambia jambo la kipumbavu na wewe ukilikubali atakudharau"
 
Back
Top Bottom