Tundu Lissu: Sitarudi tena Tanzania hadi nihakikishiwe Usalama wangu

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Akihojiwa na Sauti ya Amerika kutoka Marekani, mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na mbunge wa Zamani wa Singida Mashariki amesema hawezi kurudi tena Tanzania kwani wasiojulikana bado hawajapatikana.

Pia amesema ametishwa na mwandishi Cyprian Musiba kwenye mitandao.

Nilichopenda leo hajaongea kwa kufoka foka na mikwara km tulivyozoea labda ameanza kubadilika kimtazamo

 
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Mwanasheria Tundu Lissu amesema hatorudi Tanzania hadi apate uhakika wa usalama wake
 
Viongozi wake wamwakikishie usalama pindi ataiapotaka kugombea uenyekiti au akitaka kwenda kwa wazalendo uchwara
 
Hakuna mtu mwingine yeyote atakayehoji uamzi huo. Huo ni uamzi unaomhusu Tundu Lissu mwenyewe, familia yake na ushauri toka kwa ndugu na marafiki wa karibu zaidi naye wanaojali zaidi maslahi yake binafsi na mipango ya maisha yake atakavyo yawe.

Sidhani kwamba kuna mtu anaweza kuhoji uamzi wa namna hiyo.
 
Hakuna Jambo limefanya niwachukie watz Kama ishu ya lisu ishu ya lisu imenifanya niwachukie Sana wenye mamlaka na praise power team yao yani msemakweli na mtetea haki ya kidemokrasia mnamtwanga risasi mnampokonya ubunge halafu mnafurahia na kumkejeli ushetani ulioje?
 
Hakuna Jambo limefanya niwachukie watz Kama ishu ya lisu ishu ya lisu imenifanya niwachukie Sana wenye mamlaka na praise power wait yani msemakweli na mtetea haki ya kidemokrasia mnamtwanga risasi mnampokonya ubunge halafu mnafurahia na kumkejeli ushetani ulioje?
Nani kakuaminisha kuwa Tundu ni msemakweli? Huyo ni vuvuzela hata ukoo wake wanamjua hivyo!
 
Maneno ya Tundu Lissu siku zote yanaonekana kuwa mepesi lakini kwa watu wenye uelewa watatambua kuwa Tundu Lissu hajawai kukosea katika comments zake. Huwa anaongea huku akifahamu fika impacts za kile anachokisema. Sasa usipokuwa makini unaweza kumwelewa kiwepesi wepesi tu wakati yeye akimaanisha matokeo makubwa mbeleni.

MUNGU AKUBARIKI TUNDU ANTIPAS LISSU
 
Back
Top Bottom