Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,985
- 20,263
Mmoja ya wakufunzi wangu Mis Pam Overend juzi alinifunza mada ngumu sana katika uwanja wa mapambano (Module: Psychology GCSE). Alisema uwanja wa mapambano haumilikiwi na mtu mmoja au kikundu kimoja, inapofika uwanja umezingirwa na adui, pigana vita ukitokea nje, akakazia kuwa nje utaungwa mkono na wabia wa umiliki wa uwanja wa vita, hawa wana kura ya turufu kumshinda adui...
Nataka kusema kwamba, upinzani Tanzania uko katika vita takatifu na utawala huu, kwa miezi zaidi ya 36 sasa, sisi wapinzani tumwekwa katika tanuru la moto wa makaa ya mawe tunapambana usiku na mchana na huyu ndugu yetu wa damu kabisa aliyeamua kutubatiza kwa moto na aliahidi kutufuta Tanzania akiamini sisi ni kikwazo kwake kupeleka maji Nkasi, Nyakanazi na maeneo mengine, kwaujumla anaamini upinzani ni kikwako cha maendeleo ya nchi, hakika ahadi yake si ya maneno ni ya vitendo hasaa, mahabusu zimejaa wakosoaji dhidi ya utawala, mahakama zimejaa kesi za uchochezi..
Amefunga kila mwanya wa sisi kupambana nae kwa hoja, amefunga mikutano ya hadhara, amefunga uhuru wa kutoa maoni, amefunga vyombo vya habari visitumulike bali vimmulike yeye tu, amefunga mitandao isimkosoe, na sasa anakwenda kufunga kabisa uweko wa vyama vya siasa kwakuweka sheria ya jehanamu rasmi.
Awali nguvu ya wanaharakati ilipata ahueni baada ya gurudumu la nje kuendeshwa na Bi Mange Kimambi, huyu bahati mbaya yeye si mwanasiasa, akachoka kuwasemea waswahili. Tulifikiri tufuate nyayo za wazee wetu wapigania uhuru akina Nyerere, Nkurumah, Machel, Neto, Mandela nk, Tukaona sasa tutafute nguvu ya kidunia tukiungwa mkono na mataifa huenda ahueni itakuwepo kupunguza kibano hiki, maana kila siku mahabusu au mahakamani, Mataifa wanawasikiliza pale mtakapoeleza masahibu yenu kwa wazi, hata kama wao wanajua kinachoendelea, lakini hawakemeagi au kuchukua hatua kama hamtapaza sauti kutoa kelele za vilio vyenu...
Bahati mbaya viongozi wetu wako jela mwezi wa tatu huu, Mungu si Magufuli wala si Makonda, Kiongozi wetu aliyechakazwa risasi zaidi ya 38 mchana kweupe Tundu Lissu huyooo kasimama na katulia katika uwanja sahihi wa kimataifa wa kuieleza dunia masahibu yaliyomkuta na hali ya mambo nchini,
Ni lazima aeleze, hana sababu ya kunyamaza, kungekuwa na kesi mahakamani dhidi ya washukiwa wa kushambuliwa kwake hakika angenyamaza kutoingilia mahakama, Sasa hakuna aliyekamatwa wala kuhojiwa mwaka wa pili unaenda tangu ashambuliwe, Serikali yenye wajibu huo ilidhani ni upepo utapita, Sasa ni wakati wa kuadhibiwa, amini nakuambia kitakachotokea watajilaumu mara mia heri lisingetokea la Lissu.
Tunaoijua dunia na siasa yake, tunawaeleza kwamba hasara ya wahalifu kwa afanyacho Lissu ni kubwa kuliko kumfunga Mbowe na Matiko, Kuliko mswada wa vyama vya Siasa, Kuliko Membe kugombea urais na kuliko kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa, Lissu yupo kwenye laiti traki, anapiga utosini tu na msumari wa nchi sita. Hana cha kupoteza, ati ubunge?? Miezi 18 tu imesalia akachukue fomu, nini kigumu au cha maana mtakachomkwamisha yeye? Anaweza kuzungumza jukwaa lolote duniani bila nembo ya ubunge bali kama manusura wa risasi 38 au Mwanasheria wa Chadema. Anayewashauri anawadhalilisha na kuwachora zaidi...
Hana hasara yoyote, nanyi waharifu hamna faida yoyote kwake, Faida kubwa anayopata Lissu ni kuimarisha upinzani mara mia, na kuongeza mgawanyiko wa ccm mara mia.
Lissu ni silaha muhimu ya upinzani kwa sasa kupambana na hali ya mambo nchini, Songa mbele Lissu umma uliokutibu na unaokuombea siku zote uko nyuma yako, sisi huku home tumewekwa mtu kati, hatupanui hata pua tu sero kumekuwa sebule zetu, segerea kumekuwa kijiweni kwetu, kisutu ndio usiseme kumekuwa kama taarifa ya habari kila siku tuko huko, Sasa hivi kuna mtindo tunaambiwa kama tunabisha tujifanye tunajikuna...
Zingatia kesho jumatatu, 21 Januari 2019 TUNDU LISSU atakuwa BBC katika kipindi maarufu duniani cha HARDTalk, dunia itasinamama kwa dakika 30 mwanamume akizungumza kushambuliwa kwake na hali ya mambo ilivyo Tanzania
Heri ya kuzaliwa kamanda Tundu Lissu.
Na Yericko Nyerere
Updates 21/01/2019.
BBC HARDtalk 21/01/2019 Tundu Lissu MP via YouTube