Tundu Lissu shujaa wa kota na stori ya chura ndani ya kidimbwi

May 3, 2019
53
144
TUNDU LISSU SHUJAA WA KOTA NA STORI YA CHURA NDANI YA KIDIMBWI.

Leo 13:15pm,08/09/2019.

Tundu Lissu anasema angependa kupokelewa na watu wengi iwezekanavyo, baada ya yote ambayo amepitia, na ambayo nchi yetu imepitia, tangu Septemba 7, 2017.

Nianze na neno "Nchi yetu" Lissu hana uhalali wa kusema nchi yetu baada ya kupanda kwenye mimbali ya television ya bbc na cnn na kuitukana Serikali ya Tanzania ambayo leo anataka kurudi anasema nchi yetu,ili iwe nchi yake,Lissu anapaswa kuomba radhi kwa Wananchi wa Tanzania kwa kuitukana Tanzania akiwa kwenye Television ya bbc na cnn.

Niongelee pia sentensi ya Lissu "yote aliyopitia na nchi iliyopitia" Lissu hana mamlaka ya kufananisha matatizo yake na matatizo ya nchi,Lissu ni mtu mbinafsi sana,yaani matatizo yake anayafanya ni matatizo ya nchi kwa faida yake ya kutaka kuonewa huruma na Wananchi!?

Tundu Lissu anataka vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa vije kumpokea ili marafiki zake wa Tanzania na katika jumuiya ya kimataifa waweze kufuatilia tukio la kurudi kwake kwa kuwa yeye ni muhimu hivyo rafiki zake wamfuatilie kwa ukaribu zaidi.

Tundu anasema wawakilishi wa taasisi za kidini na kijamii, ndani na nje ya nchi yetu; wanadiplomasia kutoka nchi rafiki na mashirika ya kimataifa, pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari vya kimataifa,wamsindikize kwenye ndege katika safari yake ya kurudi nyumbani na wengine wajiandae kumpokea Uwanja wa ndege.

-Chura ndani ya Kidimbwi.

Kwa lugha ya kibeberu unaweza kusema,Tundu has always been kind of a frog in the well.Chura ndani ya kidimbwi anaona ukubwa wa anga uliosawa na kidimbwi kama Ulimwengu mzima na baada ya hapo anapiga mbizi akishangilia,Chura hajui kama kuna mito,maziwa na bahari ambayo imepita bara moja kwenda lingine.

Chura akiwa chini ya kidimbwi anaona sehemu ndogo tu ya uso wa dunia katika upenyo wake na kwa namna hiyo ufahamu wa chura utakuwa sawa na anavyoona kwa namna yake tokea chini ya kidimbwi alichopo,Mabeberu wanasemaga "You are like a frog who can see a small part of the sky through the opening" hii ni kwa vile tu unavyoyachukulia matatizo yako kama matatizo ya nchi nzima.

Adui wa Uzalendo kwa upande wangu ni kutoka nje ya mipaka ya nchi na kuitukana nchi yako,nasema hivi kwa maslahi ya Taifa ambalo limedhamiria kupiga hatua mbele lakini mtu mmoja anaenda kusema kwenye bunge la Ulaya,Umoja wa Ulaya na kama haitoshi anapanda kwenye mimbali ya television ya bbc na cnn na kulitukana Taifa la Tanzania,Je mtu huyu si adui wa Uzalendo!?

Busara ni pamoja na kuona nyuma ya Mlima, kwa kuwa tundu haoni ya nyuma ya mlima kuwa ndio yaliyo ya busara basi anapoteza hekima kubwa ya kuwa Mzalendo katika Taifa la Tanzania,Ni vyema kumwamini Mzalendo mpenda nchi lakini si msaliti anayepanda kwenye mimbali ya bbc na cnn na kuitukana Tanzania, kuwakilisha nchi kwenye taifa kubwa namba wani duniani halafu unalitusi taifa lako baada ya kupewa lunch na dinner na kukaribishwa kuwa mkimbizi,hii kamwe si busara.

-Ziko wapi busara za Tundu Lissu!?

Miaka ya nyuma kabla ya kuwa mwanaharakati wa kisiasa,Tundu Lissu alipata kutetea wachimbaji wadogo waliofukiwa huko Bulyanhulu miaka kadhaa kabla hajaingia kwenye siasa,lakini alipoingia kwenye Siasa akaanza kulipiwa lunch na dinner na mabeberu kwa kuwatetea kuiba madini,Siasa zikamfanya Tundu Lissu kupoteza busara.

Kabla ya kuingia kwenye siasa busara za Lissu zimempelekea kutetea bure bila malipo watu waliopokonyea ardhi na beberu kama Steyn,lakini leo busara za Lissu zinamtuma kwenda kuikamata ndege ya Tanzania nchini Afrika ya kusini.

Kabla ya kuingia kwenye siasa busara za Lissu zilimtuma kutetea rasilimali madini za nchi hii kwa kupiga kelele juu ya mikataba mibovu ya madini miaka mingi kabla ya kuingia katika siasa,leo hii Tundu Lissu amekiri kutoa siri ya ndege yetu ya Bomberdier iliyokamatwa nchini Canada kwa ajili ya deni hewa na fundi aliyevurunda ujenzi wa barabara ya Dar-Bagamoyo.

-Usia wangu kwako Tundu Lissu.

Nikiwa Shule ya Msingi Bungo,mjini Morogoro miaka ya 1990, nilichaguliwa kuwa kiranja au mgonga kengele nikiwa na sifa ya kuwa na nidhamu, usafi, na mwenye kuwahi kufika shuleni mapema kabla ya wengine.

Ni sawa wakati mwingine, vigezo vilikuwa vinawekwa kando na kuchaguliwa wanafunzi ambao walikuwa kinyume na sifa nilizozitaja, wanaochelewa kufika shuleni, wachafu na wasio na nidhamu. Lengo la kuwapa nafasi hiyo ni kuwafanya wabadilike.Sasa ndugu yangu Tundu Lissu unataka uingie kwenye kundi la kubadilika!?

Siku zote ukiwa kiongozi ni lazima uwe tofauti na wengine hasa kwenye matendo yako, kila unachofanya kinapaswa kuwa chenye manufaa kwa jamii, ikizingatiwa kwamba kiongozi ni kioo cha kila mtu kujitazama, ni mfano wa kuigwa kwa lugha ya beberu "role model" kwenye jamii inayokuzunguka.Sasa ndugu yangu Tundu Lissu unakwenda kuitukana nchi ukiwa Marekani kwenye mimbali ya television ya cnn na bbc,Je unawatakia nini Wananchi wa Tanzania!? ebu twambie,halafu bado unaita Tanzania ni Taifa lako,hapana,Uzalendo wako kwa Taifa la Tanzania ni mdogo sana.

Mungu mpe rehema Tundu Lissu aweze kuona sawa sawa na Wazalendo katika Taifa la Tanzania,Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki Rais wetu,John Magufuli.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
 
..kijana unatia aibu unavyotumika.

..Lissu akiwa na umri kama wako alikuwa akitetea wachimbaji wadogo-wadogo wa bulyankulu walioporwa mgodi na wawekezaji walioungwa mkono na serikali.

..wewe badala ya kutetea mambo ya maana uko tayari kutetea uovu na dhuluma dhidi ya mtu asiye na hatia.


..huyo aliyekutuma muulize amepewa nini kiasi kwamba akaachana na madai yetu ya usd 190 billion na kukubali kishika uchumba cha usd 300 million.

..muulize aliyekutuma kwanini hakupinga dhuluma ktk sekta ya madini toka wakati Buylankulu inaporwa miaka ya 90? Kwanini hakuwaunga mkono wananchi wa Kusini gesi yao isiporwe mwaka 2015?
 
Dogo Leo makanisa yote ulimwenguni yamesali kumwombea lisu na waumini wametoa sadaka ya shukrani kwa Mungu kwa kumponya,
Labda kama unaumizwa na kupona kwake ujinyonge tu
 
Nimefikiria weee, nikaona bora tu niseme ukweli! "Yule anayeweka maji ndani ya nazi ni mimi"
 
Yaani ukiisema vibaya SERIKALI umeisema vibaya NCHI? Hivi Polepole umekuwa wa ovyo kiasi cha kuokoteza vijana wa kiwango cha chini kama huyu Zuzu na kumleta mitandaoni?
 
Mtu anayeandika "mimbali" badala ya "mimbari" mpaka hapo kanionesha hana sifa za kujadili mambo makubwa ya siasa.

Ajifunze herufi za Kiswahili kwanza.
 
Wewe ni mpumbavu akili zako ni nyepesi kama gunia la pamba na ndo maana utumiwa shoga mkubwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom